MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,639
- 33,414
Wakuu,
Nimeona nilete hili hapa kwa mjadala mpana. Naona kuna wachungaji, mapadre na watumishi wa Mungu mbalimbali wakiponda waamini wanaotumia Bible App kwenye ibada badala ya bible yenyewe.
Je ni mchakato wa mabadiliko ambao pengine hawajauelewa lakini nguvu ya teknolojia inawaacha nyuma?
Kuna ubaya gani mtu kutumia Bible app kwenye ibada tofauti na kutumia Bible? Binafsi naona inarahisisha sana usomaji na kufatilia ibada vizuri.
Inawezekana kanisa linahofia kushuka kwa mauzo ya kitabu hicho ambacho ndicho kinachoongoza kwa kununuliwa zaidi duniani?
Kwa mtazamo wangu, Kanisa liwekeze kwenye kuweka version zao za Bible kwenye App ili kuepusha waamini kupakua matangopori ili kupotosha maana kila mtu anajiwekea tu. Kwa mfano kupata Catholic bible swahili version kwenye app ni tatizo hivyo Wakatoliki wengi wanapakua version ya vitabu 66.
Kama matumizi ya Bible App si sahihi ni vizuri tukapigwa shule badala ya makatazo yasiyojengewa hoja vizuri na sometimes inaweza kuwa ni kushindana na wakati tu.
Naamini nitapata shule hapa ili nibadili fikra zangu juu ya matumizi ya Bible App kwenye ibada. Wahenga walisema, wakati ni ukuta! Nani alijua siku moja tutakuwa na Pope Instagram? Teknolojia ni mbaya ikitumika vibaya lakini ni kitu chema sana kikitumika vizuri.