KERO Apps za mikopo mitandaoni, serikali ipo wapi?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

john_thesmart

Member
Joined
Jan 20, 2022
Posts
87
Reaction score
293
Habari za kazi ndugu zangu.

Kuna kampuni mbalimbali zinazodai kutoa mikopo kupitia apps (applications), lakini matokeo yake zimekuwa zikilalamikiwa kwa kudhalilisha watu, kutoa vitisho, na kutoza riba kubwa kupita kiasi kwenye mikopo wanayotoa.

Sina uhakika kama kampuni hizi zote zimesajiliwa na BOT au mamlaka husika kama watoa huduma za kifedha, au kama kuna baadhi zinafanya kazi kiholela. Kama hazijasajiliwa, swali ni kwanini bado zinaendelea kufanya kazi huku wananchi wengi wakilalamika kila siku kuhusu unyanyasaji wanaoupata?

Pia kumekuwa na taarifa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu baadhi ya apps hizi kutumia lugha za matusi, vitisho, kusambaza taarifa binafsi za wakopaji, na kuwasumbua ndugu pamoja na marafiki zao kupitia simu na ujumbe wa kudhalilisha.

Mfano ni app inayojulikana kama PESA SASA, pia wakijiita Benefit Pesa au SUN Microfinance. Kuna mtu alikopa na kulipa kwa muda hadi kiwango cha mkopo kikafika laki 6, lakini kabla hata siku ya malipo haijafika akaanza kudaiwa zaidi ya milioni 1.1 huku riba ikiendelea kuongezeka kila siku. Mbaya zaidi, baadhi ya watu wanaompigia wanatumia lugha za matusi, vitisho, na wanakataa hata kukutana ofisini kwa maelezo rasmi, badala yake wanasisitiza malipo yafanyike haraka kupitia simu.

Cha kushangaza zaidi, app yenyewe kwa sasa haionekani tena Play Store, lakini usumbufu na madai bado vinaendelea.

Naomba mamlaka husika kama BOT, TCRA, Jeshi la Polisi pamoja na serikali yetu kwa ujumla zifuatilie kwa karibu suala hili ili kulinda wananchi dhidi ya unyanyasaji wa kifedha, ukiukwaji wa faragha, na matumizi mabaya ya teknolojia.

TCRA pia waangalie namna ya kudhibiti apps zenye malalamiko mengi ya unyanyasaji kwa wananchi, kwani zimekuwa zikiongezeka kila siku.

Baadhi ya namba zinazotumika kupiga simu, kutuma vitisho au kusambaza taarifa za watu ni hizi hapa chini:

0699021753
0695544280
0699065333
0681134436
0780577136
0696439372
0685698283
0789035161
0620887778
0791410250
0692657345
0695488192

Ukiangalia vizuri utaona namba hizi ni mpya kabisa, jambo linaloibua maswali kuhusu utaratibu wa usajili wa line na matumizi yake. Je, kampuni zinaweza kusajili line nyingi kwa matumizi ya aina hii bila udhibiti wa kutosha?

Tusaidiane kupaza sauti dhidi ya unyanyasaji huu ili wananchi wasiendelee kuumizwa kwa kisingizio cha mikopo ya haraka, maana tumeskia pia hawa watu wanatumia njia hii kama Money Laundering(utakatishaji fedha haramu).
WhatsApp Image 2026-05-28 at 08.36.51.jpeg
WhatsApp Image 2026-05-28 at 08.36.51 (1).jpeg

WhatsApp Image 2026-05-28 at 08.38.57 (1).jpeg
 
Hao wanaokuoa vitisho ni watoto wa mama ntilie wanatafuta ugali utawalumu bure tu wewe kwanini usilipe deni ili uache kusumbuliwa
Kama deni lina'make sense ni sawa unalipa, sasa kuna mtu alikopa 15,000 tu anakuja kuambiwa alipe 43,500 ni sawa? Na point ya msingi ni uwepo wao kisheria na hiyo mandate ya kutukana watu na kusambaza taarifa mitandaoni ni sawa?
Mtu akiwa na shida haina maana mtu mwingine atumie hiyo kama advantage ya kufanya vitu vya ajabu.
 
Hizi apps zote zinazowanyanyasa Wananchi zimezuiliwa na BOT kufanya kazi hizo za kutoa mikopo mitandaoni ( Ingia wavuti wa BOT utaona) lakini bado zinaendelea kufanya kazi kama Kawa. Hii siyo dharau kweli Kwa serikali? Huu ubabe wanaupata wapi? Au hao watumishi wa BOT ndiyo wamiliki wa hizo apps? Au wanakula ganji? Kwa kweli maswali ni mengi tu na majibu hakuna. Natarajia hii serikali sikivu italifanyia kazi Jambo hili haraka sana.
 
BOT walishatoa muongoza hasa kwa wananchi usiende kukopa sehemu amabayo haijasajiliwa chini yake hizo apps zote ni tofauti ila zote ni kampuni moja na hazina usajili wowote
Kama hazijasajiliwa ni Kwa nini sasa ziruhusiwe kufanya kazi Tanzania? Mamlaka husika kama BOT ,TCRA, Polisi zipo wapi?
 
Kama deni lina'make sense ni sawa unalipa, sasa kuna mtu alikopa 15,000 tu anakuja kuambiwa alipe 43,500 ni sawa? Na point ya msingi ni uwepo wao kisheria na hiyo mandate ya kutukana watu na kusambaza taarifa mitandaoni ni sawa?
Mtu akiwa na shida haina maana mtu mwingine atumie hiyo kama advantage ya kufanya vitu vya ajabu.
Marejesho ni muda gani?
 
Habari za kazi ndugu zangu.

Kuna kampuni mbalimbali zinazodai kutoa mikopo kupitia apps (applications), lakini matokeo yake zimekuwa zikilalamikiwa kwa kudhalilisha watu, kutoa vitisho, na kutoza riba kubwa kupita kiasi kwenye mikopo wanayotoa.

Sina uhakika kama kampuni hizi zote zimesajiliwa na BOT au mamlaka husika kama watoa huduma za kifedha, au kama kuna baadhi zinafanya kazi kiholela. Kama hazijasajiliwa, swali ni kwanini bado zinaendelea kufanya kazi huku wananchi wengi wakilalamika kila siku kuhusu unyanyasaji wanaoupata?

Pia kumekuwa na taarifa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu baadhi ya apps hizi kutumia lugha za matusi, vitisho, kusambaza taarifa binafsi za wakopaji, na kuwasumbua ndugu pamoja na marafiki zao kupitia simu na ujumbe wa kudhalilisha.

Mfano ni app inayojulikana kama PESA SASA, pia wakijiita Benefit Pesa au SUN Microfinance. Kuna mtu alikopa na kulipa kwa muda hadi kiwango cha mkopo kikafika laki 6, lakini kabla hata siku ya malipo haijafika akaanza kudaiwa zaidi ya milioni 1.1 huku riba ikiendelea kuongezeka kila siku. Mbaya zaidi, baadhi ya watu wanaompigia wanatumia lugha za matusi, vitisho, na wanakataa hata kukutana ofisini kwa maelezo rasmi, badala yake wanasisitiza malipo yafanyike haraka kupitia simu.

Cha kushangaza zaidi, app yenyewe kwa sasa haionekani tena Play Store, lakini usumbufu na madai bado vinaendelea.

Naomba mamlaka husika kama BOT, TCRA, Jeshi la Polisi pamoja na serikali yetu kwa ujumla zifuatilie kwa karibu suala hili ili kulinda wananchi dhidi ya unyanyasaji wa kifedha, ukiukwaji wa faragha, na matumizi mabaya ya teknolojia.

TCRA pia waangalie namna ya kudhibiti apps zenye malalamiko mengi ya unyanyasaji kwa wananchi, kwani zimekuwa zikiongezeka kila siku.

Baadhi ya namba zinazotumika kupiga simu, kutuma vitisho au kusambaza taarifa za watu ni hizi hapa chini:

0699021753
0695544280
0699065333
0681134436
0780577136
0696439372
0685698283
0789035161
0620887778
0791410250
0692657345
0695488192

Ukiangalia vizuri utaona namba hizi ni mpya kabisa, jambo linaloibua maswali kuhusu utaratibu wa usajili wa line na matumizi yake. Je, kampuni zinaweza kusajili line nyingi kwa matumizi ya aina hii bila udhibiti wa kutosha?

Tusaidiane kupaza sauti dhidi ya unyanyasaji huu ili wananchi wasiendelee kuumizwa kwa kisingizio cha mikopo ya haraka, maana tumeskia pia hawa watu wanatumia njia hii kama Money Laundering(utakatishaji fedha haramu).
View attachment 3596226View attachment 3596227
View attachment 3596228
Bila shaka na malalamiko yote haya asubuhi yote hii kuna jambo limekukuta na ushadhalilishwa vya kutosha

Anyways... lipa deni tu hilo kijana
 
Kwa ulimwengu tuliopo sasa, ni vigumu kwa mtu/jamaa kukukopesha hela kirahisi, ndipo umuhimu wa hizi apps, microfinances, banks zinakuwa na umuhimu.
Kwa mazingira hayo, tatizo si wao, tatizo liko kwako; umechukua cha watu, warudishie ndani ya muda mlio kubaliana.
Vinginevyo, hao unao waomba wakusaidie kuwafungia hao, ndio ulitakiwa uwafuate mwanzoni ili wakukopeshe.​
 
Habari za kazi ndugu zangu.

Kuna kampuni mbalimbali zinazodai kutoa mikopo kupitia apps (applications), lakini matokeo yake zimekuwa zikilalamikiwa kwa kudhalilisha watu, kutoa vitisho, na kutoza riba kubwa kupita kiasi kwenye mikopo wanayotoa.

Sina uhakika kama kampuni hizi zote zimesajiliwa na BOT au mamlaka husika kama watoa huduma za kifedha, au kama kuna baadhi zinafanya kazi kiholela. Kama hazijasajiliwa, swali ni kwanini bado zinaendelea kufanya kazi huku wananchi wengi wakilalamika kila siku kuhusu unyanyasaji wanaoupata?

Pia kumekuwa na taarifa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu baadhi ya apps hizi kutumia lugha za matusi, vitisho, kusambaza taarifa binafsi za wakopaji, na kuwasumbua ndugu pamoja na marafiki zao kupitia simu na ujumbe wa kudhalilisha.

Mfano ni app inayojulikana kama PESA SASA, pia wakijiita Benefit Pesa au SUN Microfinance. Kuna mtu alikopa na kulipa kwa muda hadi kiwango cha mkopo kikafika laki 6, lakini kabla hata siku ya malipo haijafika akaanza kudaiwa zaidi ya milioni 1.1 huku riba ikiendelea kuongezeka kila siku. Mbaya zaidi, baadhi ya watu wanaompigia wanatumia lugha za matusi, vitisho, na wanakataa hata kukutana ofisini kwa maelezo rasmi, badala yake wanasisitiza malipo yafanyike haraka kupitia simu.

Cha kushangaza zaidi, app yenyewe kwa sasa haionekani tena Play Store, lakini usumbufu na madai bado vinaendelea.

Naomba mamlaka husika kama BOT, TCRA, Jeshi la Polisi pamoja na serikali yetu kwa ujumla zifuatilie kwa karibu suala hili ili kulinda wananchi dhidi ya unyanyasaji wa kifedha, ukiukwaji wa faragha, na matumizi mabaya ya teknolojia.

TCRA pia waangalie namna ya kudhibiti apps zenye malalamiko mengi ya unyanyasaji kwa wananchi, kwani zimekuwa zikiongezeka kila siku.

Baadhi ya namba zinazotumika kupiga simu, kutuma vitisho au kusambaza taarifa za watu ni hizi hapa chini:

0699021753
0695544280
0699065333
0681134436
0780577136
0696439372
0685698283
0789035161
0620887778
0791410250
0692657345
0695488192

Ukiangalia vizuri utaona namba hizi ni mpya kabisa, jambo linaloibua maswali kuhusu utaratibu wa usajili wa line na matumizi yake. Je, kampuni zinaweza kusajili line nyingi kwa matumizi ya aina hii bila udhibiti wa kutosha?

Tusaidiane kupaza sauti dhidi ya unyanyasaji huu ili wananchi wasiendelee kuumizwa kwa kisingizio cha mikopo ya haraka, maana tumeskia pia hawa watu wanatumia njia hii kama Money Laundering(utakatishaji fedha haramu).
View attachment 3596226View attachment 3596227
View attachment 3596228
Hawa mbwa wananidai mpaka sio poa.. Siku hizi hawapigi tena simu. Maana ilifika kipindi tukawa tunatukanana
 
lipa deni la watu gentleman acha visingizio bana,

yaani wakati unakopa pesa na kutumia hizo Aps hazikua na tatizo,
ila wanapodai marejesho ndio imekua udhalilishaji etii eee?

ama kwa hakika,
kukopo sherehe kulipa matanga.

Gentleman,
ingekua umekopa benki na umekwepa kulipa na watu wa benki wakaja kuuza nyumba yako kwa kukutoa ndani kwako kwa lazima, nayo ungesema ni udhalilishaji? au hakuna vitu kama hivyo kwa wakwepa marejesho?

ustaarabu ni kukopa na kulipa.
kumbuka usiku wa deni haukawii kulipa,
na dawa ya deni ni kulipa na sio kukimbia na kukwepa kupokea simu kwa makusudi :NoGodNo:
 
Back
Top Bottom