Matumizi ya Bible App Kanisani na mitazamo hasi

Matumizi ya Bible App Kanisani na mitazamo hasi

mtu akipandwa pepo sogea na simatphone yako yenye APP ya biblia uanze kukemea huku unamwekea sim kichwani uone utamu wa YESU
Mkuu naheshimu mawazo yako lakini sidhani kama hii kitu ni kweli maana Mungu anafanya kazi popote pale nafahamu watu wenye magonjwa ya kutisha waliombewa kupitia simu wakapona wengine picha zao tu ziliombewa wakapona so sioni connection kati ya material inayotumika na maombezi kufanya kazi.

Ni maoni tu
Cc MTAZAMO
 
Bible app ni nzuri sana kama utaitumia vizuri na ukiamua kutulia na kujifunza,binafsi imenisaidia sana kukua kiroho, kuna app moja kwangu ni bonge la faida huwa namshukuru sana Mungu kwaajili ya hiyo app na Mungu azidi kuitunza na kuibariki,hiyo app kiasi kwamba hata nikipoteza simu huwa nakonda kabisa,app ya YOUVERSION ni bonge la Bible app,kwanza ina version mbalimbali na katika lugha mbalimbali karibu zote hata ukitaka the Bible yenyewe ya kiyahudi,hii imekuwa ikinisaidia sana kama sijaelewa mstari Fulani unamaanisha nini huwa na jaribu kusearch katika Version mbalimbali hadi napata maana kamili, pili imekuwa ikinisaidia sana kwa reference kama nahitaji maandiko mengine yafananayo na hayo,tatu imekuwa ikinisaidia sana kuupata mstari Fulani ninaouhitaji kwa haraka,kuna wakati unakumbuka maneno ila umesahau yako wapi ,NNE app hii ina masomo mbalimbali katika kila sekta ya hapa duniani utakuta Devotional mbalimbali kuna za mwaka mzima,wiki,mwezi,siku kadhaa n.k,kwahiyo huwa nafaidika sana na devotional hizo,mfano labda nataka kujua maswala fulani yahusuyo uponyaji nitasearch neno healing zitakuja devotional mbalimbali basi nitachagua ile niipendayo,kwa kweli sijutiii kuijua hii app.

Nije kwa kanisani huwa napenda kutumia Biblia ya kawaida offcoz kwasisi wazazi Biblia ya kawaida ni somo zuri sana kwa mtoto,ila kadri anavyokuwa ni vizuri kumfundisha pia mambo mazuri yaliyopo kwenye Bible app,yaani hii app ukiitumia vizuri kwakweli hata Insta utajikuta huna muda nayo,pia unapobeba Biblia yako inakutambulisha wewe ni mtu wa aina gani, pili kibongo bongo bado sana unapotumia Simu kanisani unaonekana mtu usiyejitambua hata Paulo alifundisha alipoenda kwa wenye hekima naye alikuwa mwenye hekima,alipoenda kwa wapumbavu naye alijifanya hivyo na alipoenda kwa watoto wadogo naye alijifanya ni mtoto mdogo,so si vizuri kuwa kwazo kwa watu wengine tumeamriwa tuheshimu mamlaka zilizopo,ole wake akwazikaye na aletaye makwazo, kwako inaweza kuwa fresh tu ila kuna jirani yako hapo unaweza kumpotezea concentration kabisa akatoka uweponi akabaki anakufikiria wewe na simu yako,ila wakati mwingine tunapokuwa Bible study sometime kunatokea kujifunza mbalimbali na mabishano labda kwahiyo nikitaka reference ya neno Fulani basi huwa nachomoa simu na kusearch fasta tu. Ila bado hivi vyote ni muhimu sana Biblia ya kawaida na App nakushauri uwe navyo vyote tu,hizi ni technology chochote chaweza tokea na shetani pia hapendi neno la Mungu lisambae kwa haraka Kwa watu wote na shetani tukumbuke hujifanya kama malaika wa nuru so humu humu anaweza kupita,kuna kipindi Fulani hata hizi za kawaida zilitoka na kiswahili kibaya kabisa wakaona bora waziondoe sokoni wazirudishe za zamani.

Ila sasa hasara kubwa ya kutumia Bible app ni Memory capacity inakufa kabisa yaani ule uwezo wa kukariri umepotea,najikuta maneno najua au habari Fulani naijua ila iko kitabu gani ni shida.
Ubarikiwe mama wewe.
Kutoa muda wako kujulisha hayo.

Mwenye kutaka kuyafikia maneno ya Mungu lazima atakua kakuelewa, lakini kwa asiye taka hato elewa ulicho eleza hapa.

Tupo pamoja mm ni mtumiaji mzur sana pia mm nimeimarika kiroho zaidi kupitia bible app.
 
Mi nilishawishiwa nikaenda kawe kwa mwamposa. Eti kukanyaga mafuta.
Aisee!!!, Watu wanaselfika balaa. Yaan ni mwendo wa kutwanga photo. Hata nikasahau kilichonipeleka.
Hahahaaaaa
 
Tatizo la vijana wa sasa, hawawezi kujizuia. Kama ulivyosema meseji ikiingia katikati ya sala, lazima isomwe wakati huo huo. Ni mwiko kwao kusubiri hata kama anaendesha gari ataanza kusoma huku akiendesha!
message ikiingia unajibu........ushapoteza concetration
 
Wangapi wanakumbuka hata kuweka silent mode? Simu zinaita katikati ya divine service kila juma. Makanisa mengine yameweka hata matangazo ya kuomba waumini wazime simu lakini watu wanaona sawa tu.
Unapaswa kuweka flight mode ili laini za simu ziwe off.
 
Ubarikiwe mama wewe.
Kutoa muda wako kujulisha hayo.

Mwenye kutaka kuyafikia maneno ya Mungu lazima atakua kakuelewa, lakini kwa asiye taka hato elewa ulicho eleza hapa.

Tupo pamoja mm ni mtumiaji mzur sana pia mm nimeimarika kiroho zaidi kupitia bible app.
Asante sana nawe pia ubarikiwe zaidi.
 
Hata biblia tunazozitumia leo ni zao la teknolojia. Zamani kulikuwa na magombo ambayo yalikuwa makubwa. Maandiko yalikuwa juu ya ngozi au magome ya miti.Sioni tatizo la kwenda na bible iliyo kwenye simu janja yangu hiki ni kizazi cha kidijitali.
 
Wakuu,

Nimeona nilete hili hapa kwa mjadala mpana. Naona kuna wachungaji, mapadre na watumishi wa Mungu mbalimbali wakiponda waamini wanaotumia Bible App kwenye ibada badala ya bible yenyewe.

Je ni mchakato wa mabadiliko ambao pengine hawajauelewa lakini nguvu ya teknolojia inawaacha nyuma?

Kuna ubaya gani mtu kutumia Bible app kwenye ibada tofauti na kutumia Bible? Binafsi naona inarahisisha sana usomaji na kufatilia ibada vizuri.

Inawezekana kanisa linahofia kushuka kwa mauzo ya kitabu hicho ambacho ndicho kinachoongoza kwa kununuliwa zaidi duniani?

Kwa mtazamo wangu, Kanisa liwekeze kwenye kuweka version zao za Bible kwenye App ili kuepusha waamini kupakua matangopori ili kupotosha maana kila mtu anajiwekea tu. Kwa mfano kupata Catholic bible swahili version kwenye app ni tatizo hivyo Wakatoliki wengi wanapakua version ya vitabu 66.

Kama matumizi ya Bible App si sahihi ni vizuri tukapigwa shule badala ya makatazo yasiyojengewa hoja vizuri na sometimes inaweza kuwa ni kushindana na wakati tu.

Naamini nitapata shule hapa ili nibadili fikra zangu juu ya matumizi ya Bible App kwenye ibada. Wahenga walisema, wakati ni ukuta! Nani alijua siku moja tutakuwa na Pope Instagram? Teknolojia ni mbaya ikitumika vibaya lakini ni kitu chema sana kikitumika vizuri.
Wakati was Musa amri kumi za Mungu ziliandikwa kwenye jiwe
Wakati was torati ziliandikwa kwenye magome ya miti na nyingine papyrus
Wakati was Yesu walitembea kwa miguu au kupanda punda kwa sababu hakukuwa na magari.
Wakati baada ya Kristo wanafunzi wake waliandika barua kwenye magome na wala hawakujua kuwa iko siku barua zao zitakusanywa na kuitwa agano
Karne ya 19 kabla ya kuwepo simu umeme wala gari waliweza kuchapisha biblia kwenye karatasi kwa kuwa hiyo ndiyo iliyokuwa teknologia kubwa kwa wakati huo
Sasa karne ya 21 teknologia imebadilika unaweza kusoma hata vitabu 1000 kiganjani kukataa kusoma biblia kwenye simu ni kuturudisha nyuma enzi hizoo lazima twende na mabadiliko
 
Kweli mkuu, ni bora waamini waeleweshe matumizi bora ya hizo App ibadani badala ya kukataza tu. Huwezi kushindana na teknolojia, huu ni ulimwengu wa softcopy.
 
Kwenda na simu yenye app ya bible kanisani..ni sawasawa na kwenda baa na mwanamke mrembo unakunywa pombe na yeye unamnunulia halafu unajipa moyo et mtaishia hapohapo...inahitaji ujasiri sana....Na kwa nink ujipe shida kiasi hicho?
 
Labda tu nikwambie kiufupi ...maswala ya roho usiyaweke kwenye teknolojia ... ROHO na teknolojia ni tofaut teknolojia inatumiwa na ibilis kwa asilimia nyingi hvo kitu chenye roho ya MUNGU mfano biblia hakitaweza kuwa na nguvu ikiwa kikiwekwa sehem ambayo ibilisi ametawala asilimia kubwa

SIMU Inaweza beba video za ngono
simu hio hio umetumia kusema uongo
af baadae uweke biblia my friend hautaielewa

KEY POINT
Ukitaka uone kama biblia ya kwenye simu haina maana ...katika ROHO
Fanya yafuatayo
Siku ukiona mtu amepandwa pepo chukua simu yako yenye biblia ndan kisha sogea karibu yake uanze kusema ushindwe kwa jina la yesu ..na mwingine ashike biblia kama kitabu uone nani atakaekabwa shati na kupasuliwa simu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Acheni kudanganya watu. Kwa taarifa yako shetani haogopi Biblia unayoibeba, na wengine wajidanganya kuweka Biblia mchagoni eti mapepo yasiwakaribie.
Biblia inafanya kazi pale unapoisoma, na sio kuibeba au kumwekea kifuani Mtu aliyepagawa na pepo. Unaweza kumkemea pepo bila kuwa na Biblia mkononi, kwa sababu pepo linaangalia jinsi gani imani yako kumuelekea Yesu Kristo ilivyo kubwa ndipo litaondoka. Kama unakemea kwa kubahatisha, tegemea pepo hilo, kukuvaa wewe kama shati.
Bible app iliyowekwa katika simu, ni nzuri, na haina rofauti na ile ya kitabu hali si. Kinachoangaliwa, ni jinsi unavoitoitumia, na wakati gani unaitumia. Kalagha bahho!!
 
ukifungua bible app unashangaa notification instgram inakuja diamond afunguka mazito baada ya kuchana na zari
utashangaa unaacha kusoma mathayo 7 unazama inst n ukishaingia unapeluz mpaka mb zitakapoisha
Shetani hajali kama una Biblia au una Bible phone app. Hata ukiwa na Biblia ya kitabu, atakuingizia usingizi , mawazo ya madeni unayodaiwa, au hata michepuko yako, wakati unaisoma Biblia na kukutoa katika mstari wa imani .Shetani ana uwezo wa kuingilia mawazo yako wakati wowote ule. Kalaga bahho.
 
Elewa BIBLIA ni kitabu kitakatifu ndiomaana tunaambiwa tukisome lkn hakuna simu takatifu
Wakuu,

Nimeona nilete hili hapa kwa mjadala mpana. Naona kuna wachungaji, mapadre na watumishi wa Mungu mbalimbali wakiponda waamini wanaotumia Bible App kwenye ibada badala ya bible yenyewe.

Je ni mchakato wa mabadiliko ambao pengine hawajauelewa lakini nguvu ya teknolojia inawaacha nyuma?

Kuna ubaya gani mtu kutumia Bible app kwenye ibada tofauti na kutumia Bible? Binafsi naona inarahisisha sana usomaji na kufatilia ibada vizuri.

Inawezekana kanisa linahofia kushuka kwa mauzo ya kitabu hicho ambacho ndicho kinachoongoza kwa kununuliwa zaidi duniani?

Kwa mtazamo wangu, Kanisa liwekeze kwenye kuweka version zao za Bible kwenye App ili kuepusha waamini kupakua matangopori ili kupotosha maana kila mtu anajiwekea tu. Kwa mfano kupata Catholic bible swahili version kwenye app ni tatizo hivyo Wakatoliki wengi wanapakua version ya vitabu 66.

Kama matumizi ya Bible App si sahihi ni vizuri tukapigwa shule badala ya makatazo yasiyojengewa hoja vizuri na sometimes inaweza kuwa ni kushindana na wakati tu.

Naamini nitapata shule hapa ili nibadili fikra zangu juu ya matumizi ya Bible App kwenye ibada. Wahenga walisema, wakati ni ukuta! Nani alijua siku moja tutakuwa na Pope Instagram? Teknolojia ni mbaya ikitumika vibaya lakini ni kitu chema sana kikitumika vizuri.
 
Sometimes wanasema wenye biblia nyanyueni juu, ambao hawana lakini wanatumia za simu nyanyueni simu zenu! Alafu kichambo kinaanzia hapo sasa [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ah ah ah ah ah yan na wanachamba haswaa, ah ah ah uhii
 
Mimi naona Biblia(kitabu kina raha yake kusoma) kama unaenda Kanisani ibadani kabisa umejiandaa kwanini usibebe Biblia yako

Biblia za kwenye simu sio mbaya lakini watu hawana adabu za kujizuia kufungia App Nyingine ktk simu

Mimi mtazamo wangu Biblia ya kwenye simu itumike kama dharura tu umesahau Bible bahati mbaya

Au kama mtu anaweza kuwa mwaminifu kabisa kwa Mungu, aka disable simcard au akaweka flight mode akawa na heshima kwa Mungu hatowasha simu hadi ibada iishe atumie, lakin kama mtu akiona nafsi yake haiwezi yanini kujitia ktk majaribu kwa masaa machache tu ya kumpa Mungu, acha simu tumia Biblia(hard copy)
Ibada ikiisha tumia simu

Na ubaya wa simu mikono itataka tu uwashe kidogo uchungulie kama kuna sms na mitandao ya kijamii ndio kabisaa mikono itawasha shetan atakwambia kidogo tu halafu unazima

Asikwambie mtu simu ina vita yake, ukiweza kuvuka ktk simu umevuka eneo kubwa sana, usitumie simu au zima kabisa na ukamwambia Mungu huu muda wangu na wewe, niamini hutoki bure uwapo maombi, au kusoma neno, au ibadani. Simu weka kando utulivu utaupata tu kadiri siku zinavyo endelea utaona mabadiriko

Kwa upande waku sishauri Biblia za simu ktk nyumba za ibada labda iwe dharura au umeweza kujicontrol
 
Wakuu,

Nimeona nilete hili hapa kwa mjadala mpana. Naona kuna wachungaji, mapadre na watumishi wa Mungu mbalimbali wakiponda waamini wanaotumia Bible App kwenye ibada badala ya bible yenyewe.

Je ni mchakato wa mabadiliko ambao pengine hawajauelewa lakini nguvu ya teknolojia inawaacha nyuma?

Kuna ubaya gani mtu kutumia Bible app kwenye ibada tofauti na kutumia Bible? Binafsi naona inarahisisha sana usomaji na kufatilia ibada vizuri.

Inawezekana kanisa linahofia kushuka kwa mauzo ya kitabu hicho ambacho ndicho kinachoongoza kwa kununuliwa zaidi duniani?

Kwa mtazamo wangu, Kanisa liwekeze kwenye kuweka version zao za Bible kwenye App ili kuepusha waamini kupakua matangopori ili kupotosha maana kila mtu anajiwekea tu. Kwa mfano kupata Catholic bible swahili version kwenye app ni tatizo hivyo Wakatoliki wengi wanapakua version ya vitabu 66.

Kama matumizi ya Bible App si sahihi ni vizuri tukapigwa shule badala ya makatazo yasiyojengewa hoja vizuri na sometimes inaweza kuwa ni kushindana na wakati tu.

Naamini nitapata shule hapa ili nibadili fikra zangu juu ya matumizi ya Bible App kwenye ibada. Wahenga walisema, wakati ni ukuta! Nani alijua siku moja tutakuwa na Pope Instagram? Teknolojia ni mbaya ikitumika vibaya lakini ni kitu chema sana kikitumika vizuri.
wengine wanazitumia biblia kama hirizi wanaacha kuamini lile neno ndani yake anataka aiweke sehemu fulani ndo imsaidie (chini ya mto), wanasahau kuwa biblia ni NENO la MUNGU meaning inabidi likae moyoni, kwahiyo ukilieka kwenye app wanaona umeharibu kabisa wanasahau hata vitabu vyenyewe vilivyokusanywa na kuwa biblia viliandikwa kwenye magome na ngozi za mbuzi pamoja na mawe, shetani anacheza na ufahamu wao tu, mtu anakwambia atashindwa kujizuia mara ngapi unajizuia usiangalie porno kwenye simu yako na unasema hii kitu ni mbaya unaweka kando? mbona huangalii porn kanisani?au husikilizi nyimbo unazozipenda za kina mond na alikiba ukiwa kanisani? ni kujiendekeza tu na kutofikiria mbali maana neno linapaswa likae Moyoni...na kingine Mungu hana mipaka katika kufanya mambo yake na kutimiza makusudi yake, kama anamtumia punda ili azungumze kufikisha ujumbe (habari ya balaki na balaamu) , anawatumia makahaba kuokoa taifa lake je si zaidi sana kutumia teknolojia? hawa ndo wale waliokaririsha watu kuwa fedha na dhahabu ni vya kishetani inhali kitabu hicho hicho Mungu anawaambia fedha na dhahabu ni mali yangu!! it's a disease of mind ila pole pole tutapona ( hii naifananisha na zamani watu waliamini Mungu umuombe kwa lugha fulani ili akusikie na kukujibu maombi ila ukitukana kwa lugha yako ni dhambi) kaazi sana
 
Mfano ukiwa unakemea pepo uku ukinyoosha biblia kuelekea kwa mwenye pepo ,ukiwa na simu unafanyaje? Biblia ni silaha ya vita kiroho .
 
Mfano ukiwa unakemea pepo uku ukinyoosha biblia kuelekea kwa mwenye pepo ,ukiwa na simu unafanyaje? Biblia ni silaha ya vita kiroho .
Pepo unalielekezea Biblia eeh!! hahaha dah.. ndo Yesu alivyofanya na mitume wake? au alitumia neno kushindana na Ibilisi kule jangawani ?
 
Maendeleo ya Teknologia hayaepukiki ila kwenye nyumba za ibada kuna etiquette zake ikiwemo kuzuia destruction kwa watu wengine ukizifuta hamna shida watu wanatumia tu mbona
 
Back
Top Bottom