Matumizi ya Bible App Kanisani na mitazamo hasi

Matumizi ya Bible App Kanisani na mitazamo hasi

Labda tu nikwambie kiufupi ...maswala ya roho usiyaweke kwenye teknolojia ... ROHO na teknolojia ni tofaut teknolojia inatumiwa na ibilis kwa asilimia nyingi hvo kitu chenye roho ya MUNGU mfano biblia hakitaweza kuwa na nguvu ikiwa kikiwekwa sehem ambayo ibilisi ametawala asilimia kubwa
SIMU Inaweza beba video za ngono
simu hio hio umetumia kusema uongo
af baadae uweke biblia my friend hautaielewa
KEY POINT
Ukitaka uone kama biblia ya kwenye simu haina maana ...katika ROHO
Fanya yafuatayo
Siku ukiona mtu amepandwa pepo chukua simu yako yenye biblia ndan kisha sogea karibu yake uanze kusema ushindwe kwa jina la yesu ..na mwingine ashike biblia kama kitabu uone nani atakaekabwa shati na kupasuliwa simu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Duh.. wewe upo dunia ya ngapi?
 
Wakuu,

Nimeona nilete hili hapa kwa mjadala mpana. Naona kuna wachungaji, mapadre na watumishi wa Mungu mbalimbali wakiponda waamini wanaotumia Bible App kwenye ibada badala ya bible yenyewe.

Je ni mchakato wa mabadiliko ambao pengine hawajauelewa lakini nguvu ya teknolojia inawaacha nyuma?

Kuna ubaya gani mtu kutumia Bible app kwenye ibada tofauti na kutumia Bible? Binafsi naona inarahisisha sana usomaji na kufatilia ibada vizuri.

Inawezekana kanisa linahofia kushuka kwa mauzo ya kitabu hicho ambacho ndicho kinachoongoza kwa kununuliwa zaidi duniani?

Kwa mtazamo wangu, Kanisa liwekeze kwenye kuweka version zao za Bible kwenye App ili kuepusha waamini kupakua matangopori ili kupotosha maana kila mtu anajiwekea tu. Kwa mfano kupata Catholic bible swahili version kwenye app ni tatizo hivyo Wakatoliki wengi wanapakua version ya vitabu 66.

Kama matumizi ya Bible App si sahihi ni vizuri tukapigwa shule badala ya makatazo yasiyojengewa hoja vizuri na sometimes inaweza kuwa ni kushindana na wakati tu.

Naamini nitapata shule hapa ili nibadili fikra zangu juu ya matumizi ya Bible App kwenye ibada. Wahenga walisema, wakati ni ukuta! Nani alijua siku moja tutakuwa na Pope Instagram? Teknolojia ni mbaya ikitumika vibaya lakini ni kitu chema sana kikitumika vizuri.
Huku mitaani kwa ajili kusoma hakuna shida
Lakini Wakati Wa IBADA sio vizuri sababu simu ina mambo mengi pia haijawekwa WAKFU mbele za MUNGU.
 
Hapa sio swala la teknolojia kuwaacha watu nyuma. Biblia ya kitabu ina tofauti sana na App ya kwenye simu au tablet kwa sababu kadhaa:-

1. Kwenye kitabu ukikutana na mstari unaokugusa unaweza kuuweka alama ya kudumu ilhali kwenye simu huwezi. Kwenye kitabu, unaweza kutumia highlighter au hata kalamu uliyobeba ukachora chini ya mstari unaouona ni muhimu. Ukirudi nyumbani, unasoma tena hiyo mistari uliyoweka alama, na hili litakusaidia uwe na neno la Mungu kwa wingi ndani yako kama Mungu alivyoagiza (Kol 3:16)

2. Kwenye simu yapo matangazo yanaibuka tu ambayo hujayafungua wewe. Ukiwa unasoma mstari likiibuka tangazo linalokuvutia au kukushtua, (na mengi yanahusisha picha za wanawake au mambo ya ngono), mawazo yako yanahama. Hapo huangalii ya Mungu tena bali ya shetani.

3. Hata kama utakuwa una-save kwenye simu yako mistari fulani unayokutana nayo kwenye mahubiri, simu yako inaweza siku moja ikaingia virusi kila kitu kikapotea. Biblia haiwezi kuingia virusi.

4. Kwa namna fulani watu wanakwepa kubeba Biblia kwa sababu, unamkuta mhusika, ndani ya moyo wake HATAKI KUJULIKANA NI MKRISTO ANAYEENDA KANISANI. Mwingine anajua akitoka kanisani atapita baa kwa hiyo itakuwa noma kama amebeba Biblia. Mwingine hata amepanga na mchepuko kabisa kwamba wakitoka church wanaenda gesti. Ataingia gesti na Biblia?

5. Kama unataka mtoto wako akue anaheshimu dini yako, na yeye anajua wewe kwako wewe Mkristo msingi wa dini yako ni Biblia, basi ni lazima umfundishe kuheshimu Biblia. Uonyeshe ujasiri wa kuibeba hadharani. Yesu alisema:- Mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.(Mt 10:33) Kama wewe unaogopa kujitangaza kwamba uko upande wa Yesu kwa kubeba Biblia, basi umemkana Yesu hivyo na Yeye atakukana siku ya hukumu ya mwisho. Utaishia jehanum.

6. Biblia nyingi za ku-download zina makosa kwenye uandishi wa maneno fulani maana program ya spelling kwenye Biblia inabadilisha maneno ya Kiswahili yawe kama ya Kiingereza. Nyingine zina tasfiri za kupotosha kwenye baadhi ya mistari. Biblia za kitabu ndizo zinazofaa.
 
Back
Top Bottom