Matukio ya ubakaji yanazidi kuongezeka sana siku hizi?

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Naomba wazazi na walezi kama mimi tukumbushane kuwaelimisha watoto wetu wa kiume na hasa wa kike kuhusu mazingira hatarishi ya kupelekea unyanyasaji wa kingono au ubakaji.

Nimeona mada kule twitter mabinti wengi wakieleza namna walivyobakwa na kuwataja wabakaji wao na kutaka wachukuliwe hatua.

Ni jambo jema kabisa kwa mtoto wa kike kuja hadharani na kutamka wazi kuhusu alivyobakwa au alivyonyanyaswa kingono na kuwataja wabakaji.

Malalamiko ya kubakwa yametolewa hasa na wanafunzi waliosoma shule za mtaala wa Cambridge. Binafsi nilidhani ni kwenye hizi shule zetu za kata.

Je, ni kwanini matukio ya ubakaji yanazidi kuongezeka?
 
Kutokwenda shule kwa sababu ya lockdown kumeongeza matukio mabaya ndani ya familia.
 
Kosa lipo kwa wazazi wenyewe, hawako care..., wanawaachilia kutokatoka wakati wa lockdown...
 
UKWELI HUU HAPA
kwa maisha yalivyo sasa uwezo wa vijana kuoa ni kama ndoto hivyo hitaji la asili la mwili linapozidi wanakosa jinsi ama atavamia binti nyumbani ama house girl ama atavizia njiani, gizani, ktk mapagale nk... Hii ni hatari na madhara ya kutokua na ajira yataleta athari nyingi huko mbeleni ikiwa hakutakuwa na uvumbuzi si kubaka tu hata kukabwa kutaongezeka
 
Back
Top Bottom