Matokeo ya Uchaguzi mdogo Igunga (matokeo ya awali)

Matokeo ya Uchaguzi mdogo Igunga (matokeo ya awali)

Status
Not open for further replies.
nothing in head littlex! a great idealist like zitto can not post stupid thread like that, may b nape! shame on u ccm!u lost already!what is plan b!
 
Genius brain-CCM ''Mpenzi Igunga kazi imeisha CCM wametubwaga ! tujipange tena 2015'' KAMA NI MWANACHAMA WA CCM KITU GANI KINAKUFANYA UJIFICHEFICHE NA KUWEKA POST ZA KINAFIKI???DON CALL URSELF A GENIUS COZ U DONT EVEN DESERVE TO BE CALLED SO UNLESS STUPID BRAIN, GENIUS CHARATERS ARE WELL DEFINED, GENIUS THEY BELIEVE IN THEMSELF, IF U DONT HAVE A CONFIDENCE HOW CAN U CALL URSELF A GB?SHITS!CDM HADI SASA WANAONGOZA NA MOJA YA SABABU ZA KUCHELEWESHA MATOKEA NI HOFU YA WALIYOWAKUTA WASISINGIZIE MVUA HATA KIDOGO! SHAME ON U MAGAYANE!
 
KAMA KWELI KAKANA KITU BASI HICHI KIJITOTO CHA MZEE NNAUYE HAFAI HATA KUSHIKA NAFASI YA UKATIBU KATA!!!!!!!!!!!

Ni Jana usiku tu ambapo kiongozi mmoja wa ngazi ya juu sana kwenye Chama Cha Mapinduzi alipoibuka na orodha ndefu ya takwimu alioita MATOKEO RASMI YA UCHAGUZI WA IGUNGA na kutumwagia hapa jamvini huku akitamba na maneno ya kejeli kwa watu aliowaita 'PEOPLE'S POWER sasa kwishni', leo hii akaikane kama vile anachezea akili watoto wadogo???????????

Kwa kweli inashangaza mno kusikia eti kakana ile THREAD alioanzisha na baadaye MOD wa zamu kuanza kuikimbiza hovyo kwenda kuificha uvunguni ambapo tayari tumeshaunyonya yote.

Ripoti ya Nape ilinisababishia usumbufu mkubwa, kunipunguzia sana imani kwa Tume ya uchaguzi kana kwamba ni chombo geresha tu hivyo hata chochote watakachokitangaza, mimi kama mpiga kura wa nchi hii, si imani nayo hata kidogo kwa kuwa afisa mkubwa sana ndani ya CCM alinifanya niamini vinginevyo.

Ninaamini wapo watu wengi sana wanaojikuta katika hali hii nilionayo hivi sasa kote nchini hivyo zoezi zima Igunga haina tena any legal credibility and democratic legitimacy pindi mshindani anapojigeuza refarii.

Ukigeugeu kwa kiongozi wa ngazi ya juu kiasi hicho cha Nape kwa Wana-CCM ambaye kauli yale yoyote ile, in publi or private, huchukuliwa kuwa ni OFFICIAL POSITION ya chombo anachokiwakilisha, ni jambo la hatari mno!!!

Kama kweli anadiriki kukana waka
THREAD yake nzima tulishaihifadhi mbali kabisa kutokana na hiyo BLANDER YA KISHERIA aliyoifanya basi huyu kijana wa Mzee Nnauye HAFAI hata kushika nafasi ya UKATIBU KATA - ovyo kabisa hamna kitu pale.

Nape na CCM kweli mnaleta 'mzaha za akina Rage na bunduki kuwarukia viunoni bila kutambua' katika masuala nyeti kama haya ya uchaguzi.

Kama haujui maana ya kosa la KIUFUNDI ulilolitenda basi nenda ukamuulize Mzee Mukama atakuelewesha pengine kwa kukulambisha kibao cha uso maana mpaka hapa
KUNA KILA DALILI uchaguzi wa Igunga kuingia DOSARI KUBWA hivyo kuhitaji tafsiri za hali ya juu kisheria.

NB: Na mpaka hapa ni vema ikaeleweka wazi kwamba KITU CHOCHOTE MATANGAZO YA MATOKEO YA UCHAGUZI kwa jina la Jimbo la Igunga KAMWE HAYAWEZI KUAMINIKA tena na mtu yeyote mwenye akili timamu na ufahamu wa sheria za uchaguzi.

Nape na CCM tayari mmeingiza taifa kwenye HASARA kubwa katika hili.
Kwa mpango huu bora CDM ishinde, usije choma mtu sime huko ofisini.
 
UPIGAJI kura katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Igunga jana ulimalizika kwa amani na matokeo ya awali wakati tukienda mitamboni yalionesha mchuano mkali kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Ilipofika saa mbili usiku jana, CCM ilikuwa ikiongoza katika kata 9 kati ya 26 za Jimbo la Igunga ikiwa na kura 8,421 dhidi ya kura 6,197 za Chadema.

Kata hizo ni Ntobo, CCM 730, Chadema 302; Nguvu Moja CCM 694, Chadema 284; Nkinga ambako Rais Mstaafu Benjamin Mkapa alifunga mkutano wa kampeni wa CCM Jumamosi, chama hicho kimepata kura 1,479 na Chadema ikipata kura 1,085.

Nyingine ni Itumba CCM 1,079, Chadema 590; Nanga, CCM 897, Chadema 645; Igulubi CCM 925, Chadema 592 wakati katika Kata ya Mwisi anakotoka Mbunge aliyejiuzulu Rostam Aziz, CCM imeanguka kwa kupata kura 926 dhidi ya 992 za Chadema.

Rostam alijiuzulu wadhifa wake huo alioushikilia kwa miaka 17, akidai amefanya hivyo kutokana na siasa uchwara ndani ya chama hicho tawala.

CCM imeanguka pia katika Kata ya Mbutu ambako imepata kura 1,186 dhidi ya 1,426 za Chadema wakati katika Kata ya Kinungu imeongoza CCM kwa kura 505 dhidi ya kura 263 za Chadema.

Aidha, hadi kufikia saa mbili usiku, katika vituo 53 vya Kata ya Igunga Mjini, tayari vituo 22 vilikuwa matokeo yake yako tayari na CCM ilikuwa ikiongoza kwa kura 1,388 dhidi ya kura 1,287 za Chadema. Jimbo zima lina vituo vya kupigia kura 427.

Kutokana na Chadema kuongoza katika baadhi ya vituo vya mjini, vijana na mashabiki wa chama hicho walikuwa wakishangilia na kuandamana kukisifu chama hicho.

Matokeo ya mjini yalionesha kuwa kwenye Kituo cha Shule ya Msingi Igunga, kituo kidogo cha kwanza Chadema ilipata kura 216, CCM
(201) na CUF (3).

Katika Kituo cha Chipukizi, kituo kidogo cha kwanza Chadema ilipata 98, CCM (87) na CUF (7). Kituo kidogo cha pili Chadema 108, CCM 71 na CUF 4.

Kituo cha Tarafani Chadema 88, CCM (61), CUF (6), kituo kidogo cha pili Chadema (73), CCM (71) na CUF (4). Kituo kidogo cha tatu, Chadema (90), CCM (83) na CUF (7).

Katika kituo cha Stoo ya Pamba, kituo kidogo cha kwanza Chadema (69), CCM (81), CUF (2), kituo kidogo cha pili, Chadema (91), CCM (70), CUF (2)., kituo kidogo cha tatu, Chadema (82), CCM (86), CUF (3).

Kituo kidogo cha nne katika kituo cha Stoo ya Pamba, Chadema (72), CCM (76), CUF (2), kituo kidogo cha tano Chadema (84), CCM (79) na CUF (1).

Katika kituo cha Chipukizi, Chadema (98), CCM (84), CUF (7) kituo kidogo cha pili katika kituo hicho, Chadema (106), CCM (71) na CUF (4).

Awali, shughuli ya upigaji kura katika uchaguzi huo wa kujaza nafasi ya Rostam aliyejiuzulu Julai mwaka huu, ilianza na kumalizika kwa utulivu ambapo wakazi wa jimbo hilo walijitokeza kwa wingi katika vituo vya kupiga kura huku kukijitokeza kasoro chache.

Baadhi ya kasoro hizo ni pamoja na mpigakura kubadilisha picha ya kitambulisho chake cha kupiga kura kwa madai kuwa haikumpendeza na kuweka iliyompendeza ya rangi.

Pia ipo dosari ya baadhi ya wasio na vitambulisho vya kupiga kura kuruhusiwa kupiga kura katika baadhi ya vituo, huku vingine wapigakura wenye kasoro hiyo wakizuiliwa. Pia kulijitokeza kukosekana kwa majina ya baadhi ya wapigakura katika orodha ya wapigakura.

Katika baadhi ya vituo ambavyo gazeti hili lilitembelea ikiwemo Shule ya Msingi Chipukizi Igunga Mjini, lilishuhudia wasiokuwa na vitambulisho wakishiriki kupiga kura kwa kujaza fomu namba 17 kama uthibitisho.

Hata hivyo, katika kituo cha Stoo ya Pamba nacho cha Igunga mjini, wananchi waliopoteza vitambulisho waliwagomea kupiga kura.

Hali hiyo imezua mtafaruku na kuwavuta viongozi wa vyama katika vituo hivyo huku wakitolea mfano vituo vingine vilivyowaruhusu wasiokuwa na vitambulisho
vya kupigia kura kupiga kura.

Kasimu Mussa Selemani alikuwa ni mmoja wa watu waliokumbana na adha ya kutokuwa na kitambulisho, lakini jina lake lipo katika orodha ya wapigakura
kwenye kituo cha Ujenzi na alikataliwa kupiga kura.

“Tumetangaziwa kuwa hata usipokuwa na kitambulisho unaweza kupiga kura na ndio maana nimekuja hapa tangu asubuhi na nimeshuhudia wenzangu wakiendelea
na uchaguzi, lakini mimi nimekataliwa,” alisema Selemani.

Alisema kitambulisho chake hakufika nacho katika kituo cha kupiga kura kwa kuwa kimechanika vipande vipande. Hata hivyo, aliruhusiwa kupiga kura mara baada ya kupeleka vipande vya kitambulisho cha kupigia kura.

Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo, Protace Magayane, alisema mtu yeyote ambaye hana kitambulisho haruhusiwi kupiga kura na hiyo ni kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi.

Alisema masharti ya mpigakura yalibandikwa katika vituo vyote na kuongeza kuwa fomu namba 17 si tamko kwa ajili ya mtu aliyekosa vitambulisho vya wapigakura.

Kuhusu changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi huo, alisema kutokana na mvua kubwa katika baadhi ya maeneo jimboni humo hasa Kata ya Igurubi,
magari yalikwama na kusababisha vifaa kuchelewa kufika vituoni na kusababisha watumie baiskeli kuvibeba.

Kuhusu hali ya usalama katika uchaguzi magari ya Polisi yalionekana kila kona ya jimbo hilo huku yakiwa yamefungwa vitambaa vyekundu na mengine kuegeshwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ambako ndiko matokeo ya uchaguzi huo yatakapotangazwa.

Katika Kituo cha Shule ya Msingi Chipukizi, Mzee Rashid Sultan aliyekuwa na kitambulisho cha kupiga kura, alizuiwa baada ya jina lake kukosekana katika orodha ya wapigakura wa kituo hicho.

Hata hivyo, Sultan alipozungumza na gazeti hili alisema yeye tangu 2007 alihamia Nzega na hakuwahi kufanya mabadiliko ya kitambulisho chake hata huko Nzega.

Sultan alisema alikwenda kupiga kura kwa kuwa ameshiriki katika uhamasishaji wa kupiga kura na yeye kuhamasika lakini anahisi aliondolewa katika daftari
hilo labda kwa dhana kuwa alishakufa kumbe yuko hai.

Mzee Salum Mteka (86), alisifu utaratibu wa kuwapa kipaumbele wazee ili wasipange foleni kama vijana na kuongeza kuwa utaratibu huo umemsaidia kupata haki yake.

Hata hivyo baada ya kuzungumza na gazeti hili, alidhani kuwa ni kama wakati wa kupiga kura na kutaka mwandishi ampe sehemu ya kusaini baada ya kumhoji.

Katika Kituo cha Stoo ya Pamba nako, mmoja wa wapiga kura alizuiwa kupiga kura baada ya kubadilisha picha ya kitambulisho chake iliyokuwa haina rangi
na kuweka picha ya rangi inayomuonesha vizuri.

Mkuu wa Tathmini na Ufuatiliaji wa Polisi Makao Makuu, Isaya Mngulu, alisema mpigakura huyo, Zakaria Reuben alizuiwa kupiga kura baada ya kuharibu kitambulisho chake cha mwaka 2009 kwa kuondoa picha inayodhaniwa haikumpendeza na kuweka aliyodhani imempendeza.

Mgombea wa CCM, Dk. Dalaly Kafumu alipiga kura yake katika Kituo cha Lugubu, Kata ya Itumba saa nne asubuhi huku mgombea wa Chadema, Mwalimu Joseph
Kashindye akipiga kura katika Shule ya Msingi Chipukizi Kata ya Igunga Mjini saa mbili asubuhi.
 
kuna jitu (siyo wassira) moja la ccm huko lina roho mbaya, silipendi maana lenyewe linajua ushindi kwa ccm tu hata kama watu wafe. Hili ni jitu baya sana ambalo kwa kweli linatakiwa kupelekwa the hegue likabanwe naniliu na plaizi.

si ulitaje? Nakusaidia, linaitwa li nape
 
Seriously am speakin' hiki kinachofanywa na National Election Committe ni uhuni mtupu...Nilifikiri labda Prof Chaligha ni mtu makini..Kumbe hayuko hivyo.Liwalo na litakalokuwa lakini still watanzania tuna safari ndefu sana kuelekea katika maendeleo ya kweli ktk njanja za siasa, kiuchumi na kijamii kwa ujumla...Tumezoea sana ubabaishaji..ushabiki wa kipumbavu..Excuses za kitoto na mambo mengi yanayofanana na hayo..MUNGU IBARIKI TANZANIA NA IBARIKI PIA FAMILIA YANGU ILIYOJIVUA UTANZANIA.
 
Kweli hawa NEC wahuni sana yote hyo nikufanya ghilba ili waibe kura,hili lichama hili linauzi sana
 
(zittokabwe) We have lost the election. Chadema conceded NOT. Contemplates
petition.
From his twitter page
 
mbona kwenye vituo cdm inaongoza halafu kwenye ujumla wameachwa mbali cdm..
kweli nimeamini wanasiasa wote ni vigeugeu..
 
mbona kwenye vituo cdm inaongoza halafu kwenye ujumla wameachwa mbali cdm..
kweli nimeamini wanasiasa wote ni vigeugeu..
wenzako tayari wameshakubali matokeo...
Umebaki mwenyewe ndio unasua sua!
Kubali tu yaishe bro
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom