Kila mmoja anatoa matokeo anayoyataka, wengine wanaongea hivi wengine vile Nape Nnauye ametangaza ushindi halafu akaukana. Regia mtema kampa hongera mzee wa wake za watu na chama chake. BBC wamesema matokeo mpaka saa sita mchana. CCM wametangaza ushindi tangia asubuhi.
Je huu ndio utaratibu? Je wananchi wapiga kura wa Igunga hawana haki ya kuujua ukweli.
Mtu yeyote awe mbunge, kiongozi wa chama au serikali anayeleta uzushi ni hayawani na hafai kuongoza hata ngedere. Wananchi waliacha shughuli zao wakakaa kwenye foleni ili kumchagua mtu wanayetaka awaongoze. Hawakufanya hivyo ili kuleta masihara bali walikuwa na nia dhabiti na ya dhati. Kuendelea kuwadhihaki bila kuwapa majibu stahiki ni uhayawani na uhuni mkubwa.
Tunataka matokeo sio vibwagizo wala siasa za vichochoroni.