Matokeo ya Uchaguzi mdogo Igunga (matokeo ya awali)

Matokeo ya Uchaguzi mdogo Igunga (matokeo ya awali)

Status
Not open for further replies.
CDM msiwe na papara, matokeo rasmi yatattolewa na Magayene, kata zilizotoa matokeo ni chache sana kati ya kata 26 . Mwisho mtakimbia matokeo CCM ni washiindi tu
 
Haya, ninachokiona hapa matokeo katika vituo kadhaa vya mjini Igunga yanaonyesha CHADEMA inaongoza na hali ni shwari sasa ila viongozi wengi wa CCM wameondoka hapa mjini igunga kila ukupita mitaani sasa ni CHADEMA mwendo mdundo. Mjini ndio kuna wapiga kura wengi hapa Igunga.

CCM wamekimbia mji hoteli waliyofikia vigogo ipo kimya. Kwa sasa nasubiri vituo vya vijijini.


Other updates:

06:00 PM Misururu ya vijana imeonekana mida ya jionijioni, yawezekana idadi ya waliopiga kura ikaongezeka.

mkuu vipi orijino kopi ya matokeo ipo au ndo unasikilizia mkuu hakikisheni mawakala wenu wapo makini maana kuna vituo vitaibuka ili mtu apigwe chini..
 
Kituo cha Ziba CCM 420 Chadema 390
Nkinga 1479 CCM, Chadema 1087

Itumba nyumbani kwa Dk Kafumu wa CCM
Chadema 560 CCM 1078

Kata ya Itobo CCM 730 Chadema 362
Haya tayari tunayo, tupe mengine
 
Kutoka kwa source ya uhakika Igunga: mpaka sasa CCM wameshachukua kata 16, CDM kata 7 bado mahesabu ya kata 3.
 
Umebaki mwenyewe! CDM wenzako wote wameshakimbia!
CDM aibuuuuuu!
mkuu taratibu.....haya mambo ni ya kawaida...!Kama wana Igunga wana maisha bora mpaka kufikia kuichagua CCM basi ni uamuzi wao!
 
Kituo cha Ziba CCM 420 Chadema 390


KATA nzima ya Nkinga 1479 CCM, Chadema 1087

KATA nzima ya Itumba nyumbani kwa Dk Kafumu wa CCM
Chadema 560 CCM 1078

Kata nzima ya Itobo CCM 730 Chadema 362

source..
 
Kituo cha Ziba CCM 420 Chadema 390


KATA nzima ya Nkinga 1479 CCM, Chadema 1087

KATA nzima ya Itumba nyumbani kwa Dk Kafumu wa CCM
Chadema 560 CCM 1078

Kata nzima ya Itobo CCM 730 Chadema 362
Kazi nzuri sana!
CCM hoyeeeee
 
Hakuna anayewataka??
Igunga wanaitaka CCM!
Dr bado kidogo atangazwe mshindi..ni ishu za formalities tu zimebaki.
Hivi mnaweza kushinda kwa asilimia ngapi dhidi ya CDM? Kumbuka Igunga ina Waislamu wengi kuliko wakristo, na waislamu walipigwa mkwara na Bakwata wasiipigie kura CHADEMA! Suppose kwamba waislamu walisikiliza amri hiyo ya BAKWATA halafu mkajikuta mmeshinda kwa asilimia let say 50, mtajivunia huo ushindi wenye laani ya udini na sera za kuwagawa wananchi? Ila nawaambieni CHADEMA ikishinda, itakuwa ni aibu sana kwa viongozi wenu wa BAKWATA na CCM na sera zake za udini ambazo inazipandikiza kwa watanzania.
 
Vyama vingi vinavyokuwa mpinzani wa utawa kihistoria vinatokana na tabaka la wafanyakazi. Pamoja na kwamba tabaka la chini walio wengi ndio wanaoishi vijijini, lakani wenye uelewa mkubwa juu ya haki zao ni wale wanaoishi mijini kuliko vijijini. Hali hiyo si kwa Tanzania, na Afrika tu, ila ni kwa dunia yote.

Uchaguzi wa Marekani ambao Obama alishinda, ukiangalia kwa ukubwa wa eneo alishinda eneo dogo sana la state kubwa ambazo zina mfumo wa maisha ya kimjini kuliko state ambazo ni za wakulima ambazo zina wapiga kura wachache. State kama za Califonia, NJ, Pennslivania, New York, Virginia ambazo population ya watu ni mfumo wa maisha ya mijini zaidi kuliko shamba. State nyingine zilizobaki ndizo zenye mfumo wa watu wanaoishi maisha ya shamba na ndiko wakaoshinda Republican.

Mfumo wa ugawanyaji wa majimbo ya uchaguzi Tanzania hauwiani na idadi ya watu, ila wanaangalia ukubwa wa eneo. Eneo kubwa utakuta linagawanywa majimbo kadhaa ya uchaguzi bila kuangalia uwiano wa idadi ya watu. Hilo nalo ni tatizo ambalo siku za usoni linatakiwa kufanyiwa kazi.

Chadema inaendelea na tatizo lile lile la kuwa na mvuto mkubwa wa watu ambao si wapiga kura kwa hoja ya kutojiandikisha kupiga kura ila kushabikia tu. Hilo ndilo tatizo kubwa ambalo linaiangusha Chadema. CCM inatumia mwanya huo kwa kuimarisha nguvu ya wapiga kura kwa kuanzia shina kuwatumia viongozi wa mashina ufuatiliaji wa wapiga kura, na hivyo kuwa na hakika ya ushindi kutokana na wanachama wao kuipigia kura CCM, ndio maana unaona hata wakuu wa wilaya wako makini kutembelea vijijini na kufanya mikutano ya siri kwa ajili ya kupima upepo na kuhamasisha wapiga kura mtaa kwa mtaa na nyumba kwa nyumba.

Katika hili la Igunga hakuna uchakachuaji wa wazi, na inaweza ikawa ni hali ya kufikiriaka zaidi kuhusu uchakachuaji kuliko kuangalia hali halisi ya mfumo wa CCM kuthibiti wapigakura wake na Chadema kudanganywa na umati wa vijana wasiojiandikisha kupiga kura, hili ndilo tatizo la dhahiri.

Tatizo hili lilitokea tangu uchaguzi mkuu uliopita na hata enzi zile za mzee wa Kiraracha, badala ya kuhamasisha watu mitaani kujiandikisha kupiga kura Chadema wanasimama majukwaani kunadi sera, Kwa siasa mbinu za kuwapata wapiga kura ni muhimu zaidi.
 
Kutoka kwa source ya uhakika Igunga: mpaka sasa CCM wameshachukua kata 16, CDM kata 7 bado mahesabu ya kata 3.
Itafaa tupewe maelezo yanayojitosheleza juu ya huyo anayesimamia ujumlishaji wa kura katika kata.
 
sehemu mnapo ibiwa watz ni siri na wakati wakujumlisha basi leo wakati wamajibu pasipo chimbika mpaka nakufa ccm itatawala tu..
 
Ifike mahali swala lisiwe ushabiki wa kisiasa, swala tuangalie nani ana UWEZO wa kutatua kero za wana Igunga. Chadema, CCM wote wanasiasa na wote wapo kimaslah tu. Ucije shangaa hata upinzani ukija kuchukua nchi ikawa worse kuliko ccm. Ni hivi watanzania tuhukumu hawa wanasiasa bila kuangalia wanatoka chama gani. Swala siyo chama gani, swala ni mgombea gan.
 
Wachakachuaji wote wapo bize Igunga, wakasahau kwenye chaguzi za udiwani sehemu zingine za chaguzi ndogo. Huko lazima wapigwe
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom