Matokeo ya Uchaguzi mdogo Igunga (matokeo ya awali)

Matokeo ya Uchaguzi mdogo Igunga (matokeo ya awali)

Status
Not open for further replies.
Hivi mnaweza kushinda kwa asilimia ngapi dhidi ya CDM? Kumbuka Igunga ina Waislamu wengi kuliko wakristo, na waislamu walipigwa mkwara na Bakwata wasiipigie kura CHADEMA! Suppose kwamba waislamu walisikiliza amri hiyo ya BAKWATA halafu mkajikuta mmeshinda kwa asilimia let say 50, mtajivunia huo ushindi wenye laani ya udini na sera za kuwagawa wananchi? Ila nawaambieni CHADEMA ikishinda, itakuwa ni aibu sana kwa viongozi wenu wa BAKWATA na CCM na sera zake za udini ambazo inazipandikiza kwa watanzania.
Poor analysis
Wagombea wote wa CDM na CCM wakristo na hamna muislam!
 
Haya, ninachokiona hapa matokeo katika vituo kadhaa vya mjini Igunga yanaonyesha CHADEMA inaongoza na hali ni shwari sasa ila viongozi wengi wa CCM wameondoka hapa mjini igunga kila ukupita mitaani sasa ni CHADEMA mwendo mdundo. Mjini ndio kuna wapiga kura wengi hapa Igunga.

CCM wamekimbia mji hoteli waliyofikia vigogo ipo kimya. Kwa sasa nasubiri vituo vya vijijini.


Other updates:

06:00 PM Misururu ya vijana imeonekana mida ya jionijioni, yawezekana idadi ya waliopiga kura ikaongezeka.

Matokeo ya Igunga vijijini vipi? Maana ni kama matokeo yote ya awali ni Igunga mjini, tujuzeni tafadhali. Huku Sumbawanga kulikuwa na uchaguzi katika ya Kasense, Magamba wameshinda kwa mbinde, wafipa ni pombe ya jero tu wanakusaliti.
 
Hongera wafikishie CCM --- tuna mengi ya kujifunza zaidi ya Igunga. kwa hii trend hata 2015 sidhani kama hawa ccm watatolewa madarakani...need more research kwa nini wanashinda kwenye sehemu nyngi....kuna sababu nyingi twaweza fikiria - uchakachuaji - 10%, watu wanaijua ccm tu basi - 90%
 
CCM Chali!Kwamjibu wa taarifa kutoka eneo la uchaguzi CCM wamepigwa mweleka maana kata nyingi wameshindwa na Chadema inaongoza!Na vijana wamehaidi kulinda ushindi wao!!
 
Ifike mahali swala lisiwe ushabiki wa kisiasa, swala tuangalie nani ana UWEZO wa kutatua kero za wana Igunga. Chadema, CCM wote wanasiasa na wote wapo kimaslah tu. Ucije shangaa hata upinzani ukija kuchukua nchi ikawa worse kuliko ccm. Ni hivi watanzania tuhukumu hawa wanasiasa bila kuangalia wanatoka chama gani. Swala siyo chama gani, swala ni mgombea gan.
walaumu wanasiasa wa ccm mana mpaka sasa hawajaleta maendeleo au chochote chenye manufaa zaidi ya kuhongwa suti
 
Peoples Power.Support ipo kubwa nyuma yenu mkifanyiwa hujuma zozote Igunga will fight by any means Haki itendeke.
 
Tunasubiri matokeo kwa hamu,mbona mnatuficha????
 
Igunga mjini chadema imeongoza sasa hivi ni sherehe tupu,wafuasi wa chadema wanasherekea kila kona ya mji-Radio one
 
Vyama vingi vinavyokuwa mpinzani wa utawa kihistoria vinatokana na tabaka la wafanyakazi. Pamoja na kwamba tabaka la chini walio wengi ndio wanaoishi vijijini, lakani wenye uelewa mkubwa juu ya haki zao ni wale wanaoishi mijini kuliko vijijini. Hali hiyo si kwa Tanzania, na Afrika tu, ila ni kwa dunia yote.

Uchaguzi wa Marekani ambao Obama alishinda, ukiangalia kwa ukubwa wa eneo alishinda eneo dogo sana la state kubwa ambazo zina mfumo wa maisha ya kimjini kuliko state ambazo ni za wakulima ambazo zina wapiga kura wachache. State kama za Califonia, NJ, Pennslivania, New York, Virginia ambazo population ya watu ni mfumo wa maisha ya mijini zaidi kuliko shamba. State nyingine zilizobaki ndizo zenye mfumo wa watu wanaoishi maisha ya shamba na ndiko wakaoshinda Republican.

Mfumo wa ugawanyaji wa majimbo ya uchaguzi Tanzania hauwiani na idadi ya watu, ila wanaangalia ukubwa wa eneo. Eneo kubwa utakuta linagawanywa majimbo kadhaa ya uchaguzi bila kuangalia uwiano wa idadi ya watu. Hilo nalo ni tatizo ambalo siku za usoni linatakiwa kufanyiwa kazi.

Chadema inaendelea na tatizo lile lile la kuwa na mvuto mkubwa wa watu ambao si wapiga kura kwa hoja ya kutojiandikisha kupiga kura ila kushabikia tu. Hilo ndilo tatizo kubwa ambalo linaiangusha Chadema. CCM inatumia mwanya huo kwa kuimarisha nguvu ya wapiga kura kwa kuanzia shina kuwatumia viongozi wa mashina ufuatiliaji wa wapiga kura, na hivyo kuwa na hakika ya ushindi kutokana na wanachama wao kuipigia kura CCM, ndio maana unaona hata wakuu wa wilaya wako makini kutembelea vijijini na kufanya mikutano ya siri kwa ajili ya kupima upepo na kuhamasisha wapiga kura mtaa kwa mtaa na nyumba kwa nyumba.

Katika hili la Igunga hakuna uchakachuaji wa wazi, na inaweza ikawa ni hali ya kufikiriaka zaidi kuhusu uchakachuaji kuliko kuangalia hali halisi ya mfumo wa CCM kuthibiti wapigakura wake na Chadema kudanganywa na umati wa vijana wasiojiandikisha kupiga kura, hili ndilo tatizo la dhahiri.

Tatizo hili lilitokea tangu uchaguzi mkuu uliopita na hata enzi zile za mzee wa Kiraracha, badala ya kuhamasisha watu mitaani kujiandikisha kupiga kura Chadema wanasimama majukwaani kunadi sera, Kwa siasa mbinu za kuwapata wapiga kura ni muhimu zaidi.

hili nalo neno ngoja tuone mwisho wa siku itakuwaje..
 
Hongera wafikishie CCM --- tuna mengi ya kujifunza zaidi ya Igunga. kwa hii trend hata 2015 sidhani kama hawa ccm watatolewa madarakani...need more research kwa nini wanashinda kwenye sehemu nyngi....kuna sababu nyingi twaweza fikiria - uchakachuaji - 10%, watu wanaijua ccm tu basi - 90%
Tatizo ni sera Mbovu za wapinzani.
Hawana mikakati ya kuimarisha vyama vyao. Wanaangalia wao binafsi wananufaika na nini.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom