Matokeo ya Uchaguzi mdogo Igunga (matokeo ya awali)

Matokeo ya Uchaguzi mdogo Igunga (matokeo ya awali)

Status
Not open for further replies.
Hivi CCM inaposhinda vijijini na kushindwa Vibaya mjini hii ina maanisha nini? Ina maana CCM ina nguvu kwenye " less informed society" au? Hii ni aibu sana kwa Chama Tawala kutegemea "ujinga" au umaskini wa Watanzania kupata madaraka.
 
Kuna shemeji/wifi yenu alikuwa anasimamia vijijini kasema cdm imeaicha ccm kwa mbali. Sitaji kituo magamba msije mkamtido.
 
Bora iwe hivo,maana jinsi walivo paa duh.

Igunga ina wakazi zaidi ya laki nne, 400,000

Na waliojiandkisha kupiga kura ni laki moja na elfu sabini na nne, 174,000 kwa hiyo kura 6,000 bado sana, lakini CDM hamtoki kwa kuwa vijijini mmefanya vibaya sana, kata nyingine mmepata kura 40, 87 etc.
 
Regina mwalekwa;vijana wa chadema wameingia mtaani,vijana wanasema matokeo yanacheleweshwa na huenda yanachakachuliwa,,,,,,,polisi wanawaangalia tu hawawafanyi kitu isipokuwa wanarandaranda,,,,,,maelezo zaidi skiliza clouds

CCM haiwezi kumruhusu mjakazi wake tume ya uchaguzi kutangaza matokeo moja kwa moja kutoka vituoni, ni lazima kwanza wayajumlishe internally na kujitathmini kama wameshinda kihalali au la. Baada ya hapo wataruhusu ila mwisho wa siku tallies zitakuwa upande wa CCM. Watanzania ni watulivu sana ila provocations kama hizi zinaiweka nchi katika hali tete ya kimtazamo. Matokeo ya Igunga ni lazima yawe Chachu ya kupigania uhuru wa kweli watanzania na kwa kuanza tuanze na katiba mpya. CCM IS NOT FOR PRO BONO
 
Jamani the downfall of ccm it has to be done effectively by shown the example in igunga.people power.....chadema timua hao wezi...aka ccm
 
majina ya vituo sija yakamata vizuri
ila:
CDM 93 CCM 63
CDM 75 CCM 80
CDM 56 CCM 31
CDM 21 CCM 69
CDM 84 CCM 79
CDM 16 CCM 7
CDM 73 CCM 63
CDM 62 CCM 47
CDM 91 CCM 71
CDM 106 CCM 37
CDM 95 CCM 48
CDM 73 CCM 63
CDM 86 CCM 65
CDM 90 CCM 80
CDM 115 CCM 79
CDM 104 CCM 78
CDM 31 CCM 40

CUF sijaiweka maana ni uchafu,kura kama unahesabu ngamia tanzania.

Naanza kuipenda Tanzania! Mungu usiache wezi watutawale tena! Amen
 
Clouds FM wametanganza sasa hvi CHADEMA inaongoza na CCM inafuatia,VIVa chadema,ila bado wataendelea kutanganza matokeo
 
Kama kuna propaganda hata kwenye kutangaza matokeo hapo kazi ipo

Habari nilizo zipata hivi sasa, Novatus Makunga anatafutwa kwa kutoa habari za uongo. Hua analala wanapo lala CCM. Akipatikana anakabiliwa na kichapo cha nguvu. Matokeo mengi ya vituo kimoja kimoja yanaonyesha CDM imeshinda. Tusaidiane kuhusu hili.
 
Habari nilizo zipata hivi sasa, Novatus Makunga anatafutwa kwa kutoa habari za uongo. Hua analala wanapo lala CCM. Akipatikana anakabiliwa na kichapo cha nguvu. Matokeo mengi ya vituo kimoja kimoja yanaonyesha CDM imeshinda. Tusaidiane kuhusu hili.

huyu jamaa kapatwa na nini? yule kaka mi..u wameshindwa kumtumia au kagoma hii
 
Mkuu wala usiwe na wasiwasi, kwa kawaida magamba huwa hawako smart kwenye kuchakachua...........mwisho wa siku watafanya mistake ndogo sana ambayo itatia nyongo kwenye matokeo yote.

Mimi nashangaa watu wameshtushwa na amtokeo ya yule reporter uchwala wa ITV aliyetoa matokeo ya kata. Kama kuna matokeo ya kata yametangazwa basi kwa mtazamo wangu ni mbinu ya CCM kuchakachua au kuandaa mazingira ya fujo kwa vile hakuna msimamiz wa uchaguzi kwenye kata. Usimamizi upo kituoni na kisha ni kwenye jimbo. Haiwezekani matokeo ya vituo yaonyeshe CDM inaongoza halafu matokeo ya kata yawe kinyume.
 
Jamani makamanda wetu msichoke wala msifumbe macho hata kwa sekunde,huijui siku wala saa ajapo mwivi wako...kesheni hata kwa kupokezana.
 
Ipo siku uelewa utakuwepo hata vijijini,taratibu wadanganyika watapungua
 
Hivi CCM inaposhinda vijijini na kushindwa Vibaya mjini hii ina maanisha nini? Ina maana CCM ina nguvu kwenye " less informed society" au? Hii ni aibu sana kwa Chama Tawala kutegemea "ujinga" au umaskini wa Watanzania kupata madaraka.
You said it man, siku zote mtaji wa CCM ni umasikini na ujinga wa watanzania. Hapo ndipo ambapo huwa nazifagilia shule za kata. Naamini hizi shule zitaleta mwamko mkubwa sana huko vijijini maana zinazalisha ziro kibao ambazo zinabaki zinahang huko mitaani hazina mbele wala nyuma. Hizi ndizo zitakazoitafuna CCM miaka mitano ijayo.
 
Jamani the downfall of ccm it has to be done effectively by shown the example in igunga.people power.....chadema timua hao wezi...aka ccm

Kama kiingereza kinakupiga chenga kwanini usitumie lugha yako ya Taifa? au na Kiswahili chenga vilevile? Andika hata Kichaga utajulikana tu kuliko kuchafuwa lugha za watu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom