Maswali kwa Waziri Mkenda kupata ufafanuzi sababu za kuunda combinations mahususi za dini Sekondari

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,620
46,264
Naamini Waziri Mkenda au msemaji wa Serikali wanaona mjadala mkubwa kuhusu combinations mpya za masomo ya kidato cha tano na sita kujumuisha masomo ya kidini. Sasa wasikae kimya, kama wanaona jambo hili lina maslahi mazuri ya nchi basi wajitokeze hadharani kutoa ufafanuzi, kujibu maswali na kuwaeleza wale wanaohoji.

Waziri aeleze,

1. Kwanini waliona ni vyema kuunda tahasusi rasmi za kidini badala ya kuyafanya masomo ya dini kuendelea kuwa options tu au masomo ya ziada ambayo mwanafunzi anayependa anaweza kuongezea?

2. Kwanini ni dini mbili tu ndizo zimeundiwa tahasusi maalumu? Kwa nini dini za Uhindu, Uhamadiya, Ubudha, za Asili n.k hazijaundiwa tahasusi zao?

3. Kwanini hakuna tahasusi mahususi ya dini inayojumuisha dini mbili? Yani tahasusi ya wale wanaotaka kusoma Divinity na Islamic Knowledge kwa pamoja.

4. Kwanini haikuundwa tahasusi ya "religious studies" kutoa fursa ya wanafunzi kusoma kwa upana zaidi kuhusu dini na imani nyingi zaidi za duniani kadri ya uwezo wao?

5. Walimu watakaokuwa wanafundisha haya masomo ya kidini watakuwa waajiriwa wa serikali wanaolipwa kwa kodi za raia? Upatikanaji wao utazingatia nini hasa tukizingatia dini zote mbili kubwa zina madhehebu mengi yenye muelekeo tofauti?
 
Mbona kuna vyuo vikuu vingi hapa Tanzania vinafundisha shahada na astashahada za dini?
Cha msingi isiwe Kwa kulazimishana mi ninachoona ni kwamba serikali inaweka mazingira mazuri kila mtu aweze kupractise dini yake atakavyotaka
 
Hizi tahasusi (combinations) mpya zimeundwa ili kujibu mahitaji ya nyakati hizi. Kuna mfumko mkubwa sana wa huduma za kiroho (ministries ). Mtu akiachika tu kama Shusho na Mwamposa, au akiwa maarufu kama Bonnie Mwaitege, Masanja na Bukuku, ama akiota ndoto tu kama Geo Davie, ama akipigika kimaisha kama Nabii Tito anaanzisha kanisa.

Ndiyo maana waziri ameona ni bora wanafunzi wa sekondari wapigwe msasa ili watakapokuwa wakubwa halafu wakaingiwa na pepo la kupata faraja, ama kupata kipato kupitia kanisha, basi wawe na A,B,Cs za dini.
.
 
Maswali yaelekezwe kwa MKWE, Profesa mtamwonea bure hahusiki na hili japo lipo chini ya wizara yake. Anapenda nae kutumia V8 ya kujaziwa mafuta na serikali.
 
wanasema wahenga ukitaka kuona nyeti za kuku subili upepeo upulize
 
Hii nchi wizara ya elimu haijawahi kujua kazi inayoifanya!...

Wanatangisha tangisha tu watoto wetu!

Elimu yetu ni kama vile iko jangwani!, Kisiwani! Ama hewani inaning'inia!...

Kubadili badili mifumo na mitaala kila mara.... inaonyesha ni jinsi tusivyojua nini tunataka.

Miaka kadhaa nyuma I think 2014 kama sikosei... Walibadili tena kipimo cha ufaulu toka Div 1,2,3,4 kwenda Distinction, merits na sijui takataka Gani zingine!

Mfumo wetu wa elimu ni Mfu! Kuanzia ngazi ya wizara, vyuo, shule hadi nursery!

Mwl. Nyerere hakukosea aliposema "TUJISAHIHISHE!"
 
Naamini Waziri Mkenda au msemaji wa Serikali wanaona mjadala mkubwa kuhusu combinations mpya za masomo ya kidato cha tano na sita kujumuisha masomo ya kidini. Sasa wasikae kimya, kama wanaona jambo hili lina maslahi mazuri ya nchi basi wajitokeze hadharani kutoa ufafanuzi, kujibu maswali na kuwaeleza wale wanaohoji.

Waziri aeleze,

1. Kwanini waliona ni vyema kuunda tahasusi rasmi za kidini badala ya kuyafanya masomo ya dini kuendelea kuwa options tu au masomo ya ziada ambayo mwanafunzi anayependa anaweza kuongezea?

2. Kwanini ni dini mbili tu ndizo zimeundiwa tahasusi maalumu? Kwa nini dini za Uhindu, Uhamadiya, Ubudha, za Asili n.k hazijaundiwa tahasusi zao?

3. Kwanini hakuna tahasusi mahususi ya dini inayojumuisha dini mbili? Yani tahasusi ya wale wanaotaka kusoma Divinity na Islamic Knowledge kwa pamoja.

4. Kwanini haikuundwa tahasusi ya "religious studies" kutoa fursa ya wanafunzi kusoma kwa upana zaidi kuhusu dini na imani nyingi zaidi za duniani kadri ya uwezo wao?

5. Walimu watakaokuwa wanafundisha haya masomo ya kidini watakuwa waajiriwa wa serikali wanaolipwa kwa kodi za raia? Upatikanaji wao utazingatia nini hasa tukizingatia dini zote mbili kubwa zina madhehebu mengi yenye muelekeo tofauti?
Kweli hapo changamoto kubwa ni kwa Waalimu, kwsbb sasahv kuna somo linafundishwa O level nafikiri inaitwa Elimu ya Dini na Kiislam (EDK) ila halina Waalimu rasmi walioajiriwa na serikali, hivyo kuna Masheikh au Viongozi wa Msikitini wanajitolea kuwafundisha Wanafunzi siku wakitaka...hasa siku ya Ijumaa tu

Nafuu kwa Wakristo kwasababu kuna Waalimu walisoma Divinity huko Advanced level

Itabidi sasa waajiriwe Waalimu wa masomo ya Dini
 
Naamini Waziri Mkenda au msemaji wa Serikali wanaona mjadala mkubwa kuhusu combinations mpya za masomo ya kidato cha tano na sita kujumuisha masomo ya kidini. Sasa wasikae kimya, kama wanaona jambo hili lina maslahi mazuri ya nchi basi wajitokeze hadharani kutoa ufafanuzi, kujibu maswali na kuwaeleza wale wanaohoji.

Waziri aeleze,

1. Kwanini waliona ni vyema kuunda tahasusi rasmi za kidini badala ya kuyafanya masomo ya dini kuendelea kuwa options tu au masomo ya ziada ambayo mwanafunzi anayependa anaweza kuongezea?

2. Kwanini ni dini mbili tu ndizo zimeundiwa tahasusi maalumu? Kwa nini dini za Uhindu, Uhamadiya, Ubudha, za Asili n.k hazijaundiwa tahasusi zao?

3. Kwanini hakuna tahasusi mahususi ya dini inayojumuisha dini mbili? Yani tahasusi ya wale wanaotaka kusoma Divinity na Islamic Knowledge kwa pamoja.

4. Kwanini haikuundwa tahasusi ya "religious studies" kutoa fursa ya wanafunzi kusoma kwa upana zaidi kuhusu dini na imani nyingi zaidi za duniani kadri ya uwezo wao?

5. Walimu watakaokuwa wanafundisha haya masomo ya kidini watakuwa waajiriwa wa serikali wanaolipwa kwa kodi za raia? Upatikanaji wao utazingatia nini hasa tukizingatia dini zote mbili kubwa zina madhehebu mengi yenye muelekeo tofauti?
Aisee uliuliza maswali yaliyopo akilini kwangu na ambayo nilishayauliza. Hongera sana. Hivi ni kwa nini tusipinge hili?
 
Maandalizi ya watoto wetu ni ya kuchekesha kama ukilinganisha na wenzetu
 
Attachments

  • VID-20240325-WA0026.mp4
    3.1 MB
Back
Top Bottom