ubongokid
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 2,032
- 3,913
Habari za wakati huu;
Nimeona watu wakitoa maoni yao mbalimbali kuhusu tahasusi mpya zilizotangazwa na TAMISEMI. Katika kufuatilia mijadala, nimekutana na maoni mengi sana ila nalazimika kusimama hapa na kuiunga mkono serikali kwa uamuzi wake huu. Uamuzi huu ni uamuzi sahihi kwa wakati sahihi na kwa sababu sahihi. Nitaelezea sababu zangu hapa kwa kutoa hoja zenye nguvu kabisa.
Kwanza kabisa nataka tutambue kwamba kwa muda mrefu sana elimu ya A-level imeonekana kuwa na elimu ya kupoteza muda. Ndio maana kuna watu wengi sana wanapata Division 1 nzuri o-level ila wakienda A-level wanafeli vibaya sana. Ndio maana tuna watu wengi sana ambao wamesoma PCB na PCM na PGM lakini kwa sasa ni wahasibu, bankers, wachumi, nk., na pia wapo wengine ambao wamesoma HGL na HKL ambao sasa wanafanya kazi za IT na aina fulani za kazi za engineering. Tafsiri yake ni kwamba kwa sasa idadi ya tahasusi na uelekeo wake hauendani na wakti huu.
Sasa hivi tunaishi katika zama za TEHAMA. Lakini zaidi kuna kitu kinaitwa AKILI BANDIA aka AI ambacho kinaleta changamoto mpya kila siku. Hii ina maana kwamba, kwa sasa hivi hakuna haja ya kumfunga mtu katika tahasusi bali ni kuacha uwanja mpana zaidi wa kujifunza na kujikita katika eneo ambalo unalimudu.
Nianze kwa kuzigusa kidogo baadhi ya tahsusi MPYA mfano tahasusi za lugha, dini pamoja na tahasusi ambazo zimechanganya biashara, sayansi na dini, n.k.
Sasa hivi dini nazo ni biashara, dunia imekuwa kijiji na watu wanaofahamu lugha nyingi wanaweza kupata fursa zaidi. Kwa sasa hivi tunafanya biashara kubwa sana na Wachina na Waarabu na sio vibaya tukafahamu lugha zao tukiwa wadogo kabisa ili tuweze kuwasiliana nao. Sasa hivi sio lazima ukiwa daktari basi usiwe na ufahamu wa kuhusu lugha au utaalamu mwingine kwani kwa sasa, daktari anapaswa pia kufahamu lugha ili aweze kuwasiliana vizuri na kuwasilisha utaalamu wake kwa dunia.
Kwa ufupi, hizi tahasusi zinaendana na mahitaji. Na bado zinahitajika nyingine. Binafsi ningeshauri kabisa kwamba sasa mwanafunzi aruhusiwe kuchagua masomo yake kabisa cha msingi yawe katika orodha hiyo na Wizara iendelee kuboresha hiyo orodha kwa kuongeza masomo mengine kadiri rasilimali zinavyopatikana.
Tuachane na hao ambao kwao kila kitu ni siasa na tuanze sasa kuhamasisha specialization katika umri mdogo ili tuhakikishe kwamba tunazalisha jamii ambayo ina hazina ya utaalamu wa kila namna na maarifa ya kila namna.
Pongezi zangu sana kwa timu nzima iliyoandaa tahasusi hizi na ni ushauri wangu kwao waweke pia option ya mtu kupanga tahasusi zake mwenyewe kwa kuchagua masomo kutoka makundi tofauti mfano mtu anataka asome physics, English literature na computer science au na Islamic knowledge anaweza kabisa kusoma.