Mkuu Ami, nimeisoma mara kadhaa mada iliyowekwa hao juu, ila kila nikiisoma naona ina mapungufu makubwa. Naomba usaidie kuyataja hayo madai ya waislam. Maana hoja kuu katika waraka huu ni lawama tu na wivu wa wazi kwa wakristo kuwa ndio wanaofaidi matunda ya uhuru na waislam kunyanyaswa. Ningependa sana kujua, ni kivipi hasa wananchi wa nchi hii, hususan waislam wanavyonyanyswa na watawala tangu uhuru.
Nia yangu ni kuelimika zaidi ya kubishana. Maana, si vizuri kupuuzia malalamiko kama yana msingi. Ila kama nia ni kuweka vipengele vya dini kwenye Katiba, sidhani kuwa ni sahihi. Si vipengele vya kuhusu waislam tu, bali hata wakriston na wanaoamini makabila mengine. Katiba ni lazima itoshe kwa kila kipengele na kwa kila mwananchi.