Doria Mtandaoni
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 362
- 752
ASKOFU MKUU GERVAS NYAISONGA ACHAGULIWA KUWA RAIS MPYA WA AMECEA
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya Mhashamu Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga, amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki (AMECEA).
Uchaguzi huo umefanyika wakati wa Mkutano Mkuu wa 21 wa AMECEA, uliowakutanisha Maaskofu kutoka nchi wanachama kujadili masuala ya kichungaji, uinjilishaji na maendeleo ya Kanisa katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Kuchaguliwa kwa Askofu Mkuu Nyaisonga ni heshima kubwa kwa Kanisa Katoliki Tanzania na kunadhihirisha imani ambayo Maaskofu wa AMECEA wameiweka katika uongozi wake. Kwa nafasi hiyo, ataratibu na kuongoza shughuli za AMECEA katika kuimarisha ushirikiano wa Mabaraza ya Maaskofu, kuendeleza utume wa Kanisa na kushughulikia changamoto mbalimbali zinazolikabili Kanisa na jamii katika kanda ya Afrika Mashariki.
Hongera Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga kwa kuchaguliwa kuiongoza AMECEA. Mwenyezi Mungu akupe hekima, afya na nguvu katika kulitumikia Kanisa lake.
Asante Radio Maria Tanzania kwa chanzo.