Mkuu Topical, nadhani kuna kitu watoa mada wanakosea kidogo. Jamani maisha magumu mbona yanatugonga wote waislamu kwa wakristo na tusokuwa na dini? umeme ukikatika..unakatika nyumba za waislamu tuu? umaskini wa kutupwa ni kwa waislamu tuu? Wakuu mnahitaji kujipanga kwa upya Hizi hoja zenu hazina mashiko kabisa. Sasa hivi Raisi ni muislam, Makamu wa Rais, Jaji Mkuu, IGP nk! Sasa hamuoni kwamba hoja zenu zimekosea timing? BASI KAMA MNAWEZA WAITENI HAO VIONGOZI AMBAO NI WAUMINI wenzenu muwape msimamo wenu.
Harafu niwaulize....kama mnasema mnadhurumiwa waislamu...mbona hamsemi hivyo kwenye sanduku la kura? Kwa nini wote msingempigia kura Lipumba? (Maana JK ni muislamu ila ni uzao wa mtakatifu Nyerere kwenye CCM!).
I strongly believe all moslems dont share this kind of nonsense! Mbona kuna waislamu wako so successful ndani na nje ya nchi..na wamefanya hivo on merit? Watu kama mnaendekeza ujinga..msitake kutugombanisha watanzania. Mnalalamikia shule za wakristo..jamani..kuna Muislamu alishabaguliwa kwa kunyimwa nafasi ya shule kwenye shule ya hao "maaskofu"? Kama yupo..ajitokeze hapa..kesi yake tutaigharimia mahakamani.....Naamini..waliotoa hili tamko ni ma-opportunist tuu....na wanataka kutumia migongo ya watu kujinufaisha..siwatofautishi na wakristo ambao wametuibia kodi zetu. Kuna waislamu wanahangaika kujitafutia mkate wa kila siku kama wengine hapa....sema tuu nyingi mnataka mlete vuguvugu na machafuko hapa...muweze kuonekana wa maana huko Saudia na kwingineko... HATUDANGANYIKI! HUU WARAKA NI WAJINGA WACHACHE WANAOJIITA WAISLAMU NDO WANATAKA KUTUGHILIBU!