Matamko ya (baadhi) waislam (Dar na Mwanza) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matamko ya (baadhi) waislam (Dar na Mwanza)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Anold, Jan 17, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Jana nilibahatika kusikiliza majadiliano ambayo kupitia radio imani kulikuwa na majadiliano ambayo ni muendelezo wa tamko la waislamu walilolitoa katika ukumbi wa karimjee.Kilichonivutia kufuatilia majadiliano hayo ni baada ya kusikia kuwa baadhi ya wajumbe waliokuwa studio (Iman Radio)ni maprofesa kutoka chuo kikuu cha Kiislam morogoro. Nilikuwa na uhakika kabisa kuwa kutokana na heshima kubwa waliyonayo maprofesa ni lijua pengine mchango wao ungetosha kutoa au hata kueleza mambo yenye mantiki na manufaa kwa Taifa letu ambalo kwa miezi kadhaa sasa lina kila dalili ya kutoka katika mstari ulionyooka na kama hatua za dhati hazitachukuliwa ni dhahiri hatutaweza kubaki salama tena.

  Katika majadiliano hayo, wajumbe hao (wakiwemo maprofesa) walitoa shutuma kali kwa viongozi wa kanisa hasa kanisa katoliki wakidai kuwa kanisa ndiyo linaendesha serikali na kwamba serikali inafuata maagizo ya kanisa aidha wajumbe hao walilaumu magazeti karibu yote ya jana/juzi kwa kushindwa kutoa habari za kina wakidai kuwa ni hujuma (pengine za kanisa)

  Mashehe hao (wakati wa mjadala) pamoja na mambo mengi walijaribu kumlaumu waziri mkuu Mizengo Pinda pamoja na Mzee John malechela wakidai kuwa kitendo cha kuwaomba radhi maaskofu kwa matamko machafu yaliyotolewa na baadhi ya viongozi wa ccm (mzee makamba na mama chatanda) ni ukiukwaji mkubwa wa katiba na hivyo hawaoni kwa nini waziri Mkuu asijiuzuru (ushauri huo ulitolewa na shehe mwanasheria aliyejiita amebobea katika taaluma hiyo japo alipoulizwa na mtangazaji aeleze kifungu alichokiuka alishindwa kubaini kifungu hicho)

  Lawama nyingine waliitupia serikali kwa kuacha Kanisa liendeshe nchi kwa kuachia Kanisa kuwa na Hospitali nyingi, vyuo vingi, na shule nyingi kitu ambacho vitu hivyo walidai kama vingemilikIwa na serikali kanisa lisingekuwa na nguvu. Kutokana mafanikio haya ya kanisa washehe hao (waliokuwa studio za Iman Radio) walikubaliana kwa pamoja kuwa njia pekee ya kufanya ni kuhamasishana kwa sasa na kudai wapewe eneo lao wajitawale ili kuepuka uonevu wa kutawaliwa na kanisa.

  Naamini kuna wana JF ambao walisikiliza kipindi hicho kwa umakini na kupima hoja za wanazuoni hao. Kimsingi mimi sikushangaa kusikia matamshi hayo maana ndiyo hoja tulizozizoea ila kilichonisikitisha ni kuona kuwa hata wasomi waliobobea wanaliangalia tatizo walilonalo waislam kwa jicho na ufahamu wa mtu wa kawaida kabisa.

  Pili nilishangazwa na taharuki ya hao mashehe kujumuisha sauti ya maaskofu wachache wa Arusha kama tamko la Kanisa la Tanzania kitu ambacho si kweli na hakipo.

  Profesa analaumu Kanisa kuwa na idadi kubwa za Hospitali zinazotibu watanzania wote bila kujali dini katika matibabu hata ajira? mashehe hao walilaumu kanisa kupewa chuo cha Uhasibu Iringa Huku wao wakipewa cha morogoro. Wamesahau kabisa kuwa chuo cha Nskela Iringa kiliuzwa kwa kanisa kwa utaratibu wa kawaida huku chuo cha tanesco wakipewa bureee na Mkapa wala haijasikika mtu akihoji.

  Wanazuoni hao walifika mbali kiasi cha kudai kuwa wabunge wengi kiasi cha 75% ni wakristo, wakati wanajua kuwa mbunge anaingia bungeni kwa kura? kama karne hii kuna watu wanamawazo hayo basi Tanzania ina safari ndefu ya kufikia hapo tunapotaka kufika.

  Nashindwa kuelewa mpaka sasa kuwa tamko hili la mashehe lililoibua taharuki hii miongoni mwa waislam ni kufuatia tamko la maaskofu wa mkoani Arusha au kuna lingine? Nilitegemea tamko lingelenga hayo yaliyotokea Arusha badala yake kumeibuka hoja tofauti kabisa. inawezekana kuna tatizo ambalo sijaliona hivyo nimeona tueleweshane humu JF kuwa taharuki hii yenye hoja hata za kugawana nchi ni hili tu la Arusha au kuna lingine?
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,766
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Utaumia saana mkuu hizo zoote ni mbinu za jk!
  Yaani kweli jk ni hatari kwa taifa hili.
   
 3. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Nadhan huo ulikuwa ni mdahalo wa maprofesa waliokuwa discharged milembe na wameenda field ya kufundisha morogoro!
   
 4. l

  luckman JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  mi sishangai hata kidogo kuona mambo kama haya yanaibuliwa pasipo ulazima wowote, tushazoea na hii inatupa sura ya pili ya ndugu zetu ingawa bado hawajataka kuwa wawazi zaidi ili jamii ya watanzania kwa ujumla wao tukajua!tatizo lililopo mezani ni juu ya matatizo yaliyotokea arusha,lengo ikiwa ni kujua chanzo ni nini na tufanye nini ili yaliyotokea yasirudie tena. kinyume na matarajio ya wengi watu wenye upeo kama hao pamoja na wanazuoni wantoa tamko kama hilo?? tokezeni mtoe dukuduku lenu,

  haya yote ni mazao ya udini aliyoanzisha baba mwenye nyumba,hatutaki nchi yetu iingie katika marumbano na dhambi za kutengana sababu ya udini!tanzania ni moja, tunayo mambo mengi sana ya msingi ya kujadili na sio udini hii ni dhambi ambayo itatufikisha pabaya sana!
   
 5. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Wewe Anold inaonekana ni mbinafsi uliyepitiliza, hii topic ipo humu tangu juzi inajadiliwa kwa nini ukuungana na wengi kuchangia ile thread iliyoanzishwa tangu juzi? badala yake unajaza server bila sababu za msingi, na ndio maana sishangai wewe mpaka sasa umegongewa THANKS 90, lakini wewe hujawahi kumgongea THANKS hata member mmoja, kama wewe sio mbinafsi tukupe jina gani?
   
 6. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kuhusu wabunge kuwa wengi wakristu. Nashauri vianzishwe viti maalum vya waislam maana wako nyumba sana kama....****ban***.
  Kuhusu kugawana nchi nashauri igawanywe fasta halafu sisi wakristu tutajenga ukuta mkubwa kuliko ule waisrael waliowajengea wapalestina. Ukuta huu ni muhimu maana nchi watakayopewa hawa waislam na maprofesor wao hao wa morogoro haitatawalika wala haitakuwa na maendeleo yoyote. Sana sana itakuwa somalia,yemen au hata afghan nyingine. Hivyo nashauri kura ya maoni ipigwe upesi na waislam wepewe maeneo yenye rasilimali nyingi. Baada ya muda utaona ni watu gani watatamani kwenda nchi ya wenzao!
   
 7. N

  Nyota Njema Senior Member

  #7
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hhh! Heunda hawa maprofessor wote ni CUF, ndoa ya mkeka na CCM inaanza kuwashinda, wanataka taraka rejea!
   
 8. M

  Mchili JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hawa wanaogopa kivuli chao. Umande wakimbie wenyewe halafu wanataka kuvuta wenzao nyuma. Hata wakipewa nafasi zote za ubunge na uwaziri bado watalalamika tu. Watanzania tusihangaike nao lakini wanapotupia wakatoliki kila lawama hata kama ni Pinda au Malecela amekosea hiyo haikubaliki inabidi wapewe onyo. Hawajua hata kuwa sio wakristo wote ni wakatoliki.
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Nani alikwambia jiwe usafishwa kwa maji likatakata? ukidhani natania chukua maji lita milioni 4 safisha jiwe uone kama litatakata! Ndivyo walivyo wahadhili wa kiislamu awe wa chekechea au chuo kikubwa (sio kikuu) hawasaidiwi kwa elimu ya darasani. Ndio sababu tuna wakina Kikwete kwenye game!
   
 10. m

  mpingomkavu Member

  #10
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli ukisitaajabu ya musa utaona ya filauni
   
 11. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mi naona kikubwa ni kuwaombea tu hao watu maana kila kukicha wanalalamika tu.
   
 12. N

  Nanu JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  anyway, these are nonissues if they are trashed! when you take them seriously can divide us on religion classes which non matter to us. we are gone over those and now we are forging one way forward as one country and what we lack is only political wilingness. we want a leader who need to say no, regardless of his religion when a group of few individuals try to work on the shade of religion be it muslim or christian.
   
 13. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #13
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Precisely!!hakuna cha kujifunnza!!
   
 14. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hawa jamaa wameathirika kisaikologia!!
   
 15. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #15
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Wanamlalamikia nani wakati serikali inaongozwa na muislamu mwenzao ,akisaidiwa na mwislamu mwenzao!!
   
 16. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #16
  Jan 17, 2011
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mwinyi aliwaasa wasome na kupiga kazi waache malumbano, tena mwenye kulaumiwa kwa sasa ni JK hana aibu kusimamia udini tena jukwaani waziwazi, hivi yupo wapi vile kwa sasa? yani chalii bonge ya msaniii wa kiswahili
   
 17. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #17
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Shule na vyuo vya katoliki vilijengwa kwa fedha za wakatoiliki wenyewe,hakuna fedha za serikali.Wanachotakiwa kufanya ni kujitahidi kujennga shule na vyuo vya na kuwa na usimamizi imara,badala ya kulalamika kama watoto wadogo wasiojua chochote!!
   
 18. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #18
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ila nadhani hao ambao walitoa tamko watakua wametumwa na jk mwenyewe na si mtu mwingine.
   
 19. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #19
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mbona anawatuma kutamka vitu vya kijinga sana!!
   
 20. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #20
  Jan 17, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135


  This is very interesting...!!! Yaani mimi nashindwa kabisa kuwalewa kabisa hawa JAMAA!!! Hivi jamani.... leo hii rais wetu na makamu wake....ni wa imani moja na hawa JAMAA!, lakini wanadirki kusema serikali inaendeshwa na kanisa katoliki???!!! Ingekuwaje basi kama rais angekuwa mkatoliki kwelikweli!!!!
  Jamani ndugu zangu waislam, tumieni basi hiyo elimu dunia mliyopata katika ku-argue jamani!!!....
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...