Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,021
- 2,478
View: https://youtu.be/R1zyTINo6kQ
Rafiki yetu Lord Denning ameuliza maswali kadhaa kuhusu tamko la TEC kwenye uzi unaopatikana HAPA. Nasi kwa hapa chini tumeamua kumjibu point counter point.
1. Lord Denning ameuliza: Wanadai Serikali iachane na Mkataba wa Bandari kwa sababu wananchi wamegawanyika kuhusu mkataba huo. Je, ni jambo lipi nchi hii limewahi kukubaliwa na asilimia 100 ya wananchi wote? Kwenye Mfumo wa vyama vingi, Mbona asilimia kubwa ya Wananchi walikataa mfumo huo ila Serikali wakauunga mkono? Je kwa nini hawakutoa tamko kipindi hicho kutaka nchi iendelee kuwa ya Chama kimoja? Kwa tamko lao walilosema maamuzi ya wananchi yaheshimiwe basi wanataka Serikali ifute maamuzi yake ya kuruhusu mfumo wa vyama vingi na turudi kwenye mfumo wa Chama kimoja?
Jawabu: Kaulimbiu ya tamko la TEC ni "Sauti ya watu (wengi wenye akili timamu) ni sauti ya Mungu." Hawajasema kwamba "Sauti ya watu (wote wakiwemo vichaa) ni sauti ya Mungu." Kanuni ya "mental reservation" iko kazini hapa pia. Tulia sindano ikuingie.
2. Lord Denning ameuliza: Kwenye tamko lao TEC wanadai Mihimili ya dola iheshimiwe. Juzi Mahakama Kuu wametoa maamuzi ya kutupilia mbali maombi ya watu walioshtaki mkataba wa Bandari. Sasa kwa nini wanataka mihimili ya dola iheshimiwe na wao hawataki kuheshimu maamuzi ya Mahakama? Kama Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, hasa ibara ya 107A, inasema Mahakama ndio Mhimili wa mwisho katika kutoa haki sasa kwa nini hawaheshimu maamuzi ya Mahakama halafu wanatoa tamko kusema Mihimili ya dola iheshimiwe?
Jawabu: Walichosema TEC ni kwamba Bunge na Mahakama ni mihimili inayofanya kazi chini ya shinikizo la Ikulu. Rais amekuwa mfalme anayedhalilisha Bunge na Mahakama. Uhuni uliofanywa na Bunge wakati wa kuidhinisha mkataba wa bandari ni uthibitisho. Hukummu ya Kesi ya Mahakama Kuu Mbeya ni ushahidi tosha. "Ukipinga mkataba wa bandari unampinga Mama," ndio kaulibiu iliyo ushahidi tosha.
3. Lord Denning ameuliza: Wao TEC ya Wakristo wanavyotoa tamko kutaka Serikali iachane na mkataba wa bandari; kesho BAKWATA ya Waislamu wanaweza kutoa tamko; na Kesho kutwa Mabuda wanaweza kutoa tamko. Je, wanataka Serikali imsikilize nani katika suala la mkataba wa Bandari?
Jawabu: Kaulimbiu ya tamko la TEC ni "Sauti ya watu (wengi wenye akili timamu) ni sauti ya Mungu (wa watu wote)." Hawajasema kwamba "Sauti ya watu (wengi wenye akili timamu) ni sauti ya Mungu (wa watu ambao ni Wakristo)." Kanuni ya "mental reservation" iko kazini hapa pia. Tulia sindano ikuingie.
4. Lord Denning ameuliza: Kwa hali hii tukiaamini kwamba ilikuwa sawa kwa mapadre wa kanisa katoliki waliohamasisha mauaji ya kimbari Rwanda kushitakiwa tutakuwa tuekosea?
Jawabu: Ni kichaa pekee anayeweza kuamini na kukubali hoja ya Lord Denning ifuatayo: Baadhi ya mapadre katoliki walihamasisha mauaji huko Rwanda. MMapadre Katoliki ni Wakristo. Kwa hiyo, Wakristo wote sio waadilifu.
Kwa ufupi, TEC wamekataa Watanzania kuendelea kusokomezwa chini ya utumwa wa wawekezaji wa kigeni, na hasa Waarabu wa Dubai ambao ni makuwadi wa ukoloni wa kilowezi!
Dawati la Mama Amon,
"Sumbawanga Town"
Sumbawanga.