Maswali ya kijinga na majibu ya hasira. Ongeza na ya kwako

Unaanzisha thread halafu mtu anauliza...thread yako inatufundisha mini? Namjibu kwa upole"kucomment ujinga km wa kwako"
 
Maswali ya kijinga na majibu ya hasira;

1. Mtu anakuona umejilaza na macho umefunga anakuuliza umelala?..... Hapana najaribu kufa.

2. Mvua inanyesha halafu unatoka nje kisha mtu anakuuliza unakwenda na hii mvua?..... Hapana nitakwenda na inayofuata.

3. Rafiki yako anapokupigia simu yako ya mezani afu anakuuliza uko wapi?..... Niko kanisani naombewa.

4. Wanakuona umelowa ukitokea bafuni wanakuuliza umetoka kuoga?...…. Hapana nimeanguka kwenye bakuli la choo.

5. Umesimama nje ya lift kwenye jengo la sakafu ya chini kisha unaulizwa unapanda juu?..... Hapana ninasubiri chumba changu kije kinichukue hapa chini.

6. Unamnunulia mkeo maua anakuuliza hayo ni maua?..... Hapana mke wangu, ni karoti.

7. Uko kwenye foleni ya kulipa tiketi ya kuingia uwanjani kucheki mpira, rafiki yako anakuuliza na wewe unaenda kuangalia mpira?..... Nimekuja kulipa ada ya shule.

8. Ongezea na yako
Hahahahahaaaaa Tashtiti hizo..
 
< "Kijana una umri gani?"
> "Miaka 15"

< "Una uhakika?"
> "Hapana sina nimeuacha nyumbani"

> "Mbona unaonekana ni mtu mzima?"
> "Kwasababu sio mtu nusu"

< "Akili zako zinakutosha kweli?"
> "Ndio zinanitosha,nimeshonewa juzi juzi tu"
 
Back
Top Bottom