Aina za ndoto na maana zake, baadhi ya ndoto na maana zake

Kichuchunge

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
338
891
Hii itakuongezea maarifa, ukiota ujue nini ulichokiota, na maana yake, na namna utakavyoingia kwenye maombi juu ya hiyo ndoto.

1.WANYAMA:Kuota unakimbizwa na wanyama wakali inaasshiria mashambulizi ya kipepo,yaaani nguvu za giza zimejizatiti dhidi ya maish yako.

2. DAMU:Kuota/kuona damu kunaonesha kuna hatari mbele.Inaashiria kifo na ajali.Kwa mama mjamzito huashiria kuharibu mimba.

3. .NYUKI:Kujiona au kumuona mtu amezingirwa na nyuki ni ishara ya shambulizi la kiroho na kutofanikiwa kimaisha.

4. KUOGA:Inaonesha/inaashiria utakaso wa rohoni(utakatifu).

5. BIBLIA:Kuipoteza biblia yako inaashiria kurudi nyuma kiroho na kukosa imani.

6. PAKA:Kuota paka ndotoni huashiria kuwa wachawi wanafuatilia maisha yako.

7. KUIBIWA TAJI:Inaonyesha kupoteza umaarufu na kurudi nyuma .pia inaweza kuashiria kushushwa cheo au wadhifa ofisini au katika nafasi yako kiuchumi au kisiasa.

8. .MLANGO ULIOFUNGWA:Unapo ota mlango wa ofisini kwako umefungwa dhidi yako inaashiria kupoteza kibali au kufukuzwa kazi.kama ni mlango wa biashara yako inamaanisha kunahatari ambayo itaua biashara yako.

9. JENEZA:Inaonesha kuwa roho ya mauti (kifo)inafuatiria maisha yako au umpendaye (rafiki wa karibu)

10. AGANO:Kufanya agano/kuingia kwanye agano na mtu yeyote ndotoni ni kifungo cha kiroho.

11. .MSALABANI:Inaashilia mzigo mkubwa na shida /taabu.

12. GIZA:Inaashiria kuchanganyikiwa na kurudi nyuma.Iinaashiria kuzolota kiroho.

13. DENI:Kukupa ndotoni au kudaiwa kuashiria kudorora kiuchumi kiasi cha kuonyesha dalili zote za kufilisika.

14. .MBWA:Kucheza au kumbeba mbwa kunaashiria roho chafu (uovu) hasa wa usherati (uzinzi)

15. NDGU ALIYEKUFA:Kuota cha ndugu inaashiria uwepo wa mzimu wa familia.Uwe mwangalifu na ujumbe unaoweza kuonekana kama unapata taarifa muhimu lakini mungu hatumii njia za kipepo kusema na watoto wake SOMA 2WAKORINTHO 11:14 NA MHUBIRI 3:21.

16. KUNYWA POMBE:Kuota unakunywa pombe inaashiria kupenda ya dunia

17. ALAMA ZA KIPEPO:Unapoumizwa ndotoni au unapoamka na kukutwa alama mwilini mwako inaashiria magereza ya kiroho na kutumikishwa na mapepo.

18. PUNDA:Inaashiria ugumu wa mateso au shida katika maisha.

19. MITIHANI:Unaashiria majaribu na hali,kipindi kigumu.

20. KUPAA:Inaashiria kutawaliwa na wachawi,shambulizi la kiroho yaani kwamba huenda utachanganyikiwa.

21. KUVUA SAMAKI:Kuvua samaki inaashiria kuhubiri injili ya wokovu(soul winning)kama ilivyo katika biblia.

22. MOTO:Inaashiria kupoteza na majanga.

23. MAUA:Kupokea maua kutoka jinsi nyingine (kwa ambao hawajaoa au kuolewa)inaashiria kuwa mwenzi wako huenda atakujakuwa huyo huyo kwa maisha yako.

24. KUPIGWA RISASI(KUJERUHIWA):Inaonyesha udhaifu wa kiroho,shambulizina maadui wamejipanga kuharibu maisha yako.

25. KUPIGWA RISASI (ISIKUJERUHI):Inaonyesha ulinzi waakiungu na ushindi juu ya adui zako.

26. KUVUNA:Unapoota unavuna viazi,mihogo n.k.inaashiria Baraka za Mungu.

27. ASALI:Inaashiria Afya na mafanikio maishani mwako.

28. NYUMBA TUPU:Inaashiria hili ngumu na umaskini.

29. KUJIFICHA:Inaashiria maadui wanapigana/wanafuatilia maisha yako lakini uko chini ya ulinzi wa Mungu.

30. SAFARI:Unapoona na kujiona /kuona upo kwenye safari isiyokuwa na mwisho(kikomo)ina maanisha
unachofanya au unachotaka kufanya itakuwa ni kupoteza-poteza muda na nguvu.Hakutakuwa na matunda.

31. KUPOTEZA FUNGUO:Unapopoteza ufunguo wako ndotoni,inaashiria mlango wa Baraka zako
utafungwa.Inaweza hali hiyo ikakuletea hitimisho la mipango chanya,matarijio na matumaini yako kuhusu mafanikio.

32. FUNGUONYINGI:Unapoota na kukuta au kugundua umeshika funguo nyingi,inaashiria Baraka za fursa nyingi zinakusubiri maishani mwako.

33. KUPOTEZA PESA AU MALI: Inaashiria mambo mabaya au wezi wanaweza kuiba pesa au vitu vyako.Inaweza kumaanisha unataka kufanya biashara isiyo sahihi au kuangukia kwenye mitego ya matapeli na makundi ya mafisadi.

34. MZIGO: Kubeba mzigo inaashiria hili mbaya katika mateso na umasikini.

35. PESA: Unapoota mtu anakupa msaada au akukupa pesa bure,inaashiria kibali au neema maalumu na mpenyo wa kipesa mbele yako.

36. .MOCHWARI: Inaonyesha/inaashiria mauti inakufuatilia/ imekuzunguka wewe au mtu uliye muona kwenye hiyo ndoto.

37. UKICHAA: Unapoota umekuwa kichaa ndotoni,inamanisha shetani anataka kusababisha mvurugano katika maisha yako.Inamaanisha shetani anataka/yuko tayari kukudhuru.unapoota unacheza na vichaa au watu wenye ukichaa pia inaashiria shambulizi la kiroho ili kukusambaratishia amani na utulivu.

38. WAHUNI: Unapoota umekimbizwa/umefukuzwa na wahuni,inaashiria nguvu za giza na wachawi wanajaribu kukuharibu(kukuua).

39. RUNGU: Niishara ya nguvu,pia inaashiria ukakamaavu kiroho na ulinzi wa kiungu.

40. NDOA: Unapoona unafunga ndoa na mtu asiyemjua,inaweza kuashiria mume/mke wa kipepo (kama ni mtu unayemjua lakini ameao/ameolewa,ni ishara ya kufanya kosa kubwa/hatari katika ndoa.Kama ni mtu unayemjua vizuri na wote mko na vijana na kama huna tama za mwili kwake (naye)hiyo inaweza kuwa ishara ya mwenzi wa maisha.

41. MIMBA KUTOKA/KUHARIBIKA:Kama mwanake mjamzito ,umeota mimba imetoka/imeharibika,usilichuklie kirahisi,pasipo kuangalia ni nani aliyesababisha hilo,kwani linaweza kutokea kiuhalisia.

42. UCHI/KUVUA NGUO:Inaashiria aibu au fedheha.

43. SIMBA:Kama katika ndoto yako umeshambuliwa na simba na ukafanikiwa kumuua,inamaanisha umemshinda na kumua mtu aliyekuwa anataka kuharibu maisha yako.

44. BUNDI:Kuona bundi ndotoni inaashiria ubaya.ni taarifa kwamba kitu kibaya kitatokea/kinakwenda kutokea.

45. MTU ANAKUFUKUZA/ANAKUKIMBIZA:Kama katika ndoto yako umeota mtu unayemjua amekukimbiza akitaka kukua, mtu huyo anaweza kuwa hana mawazo/makusudi mazuri juu yako.Hata hivyo katika nyakati zingine wachawi hutumia sura ya mtu yeyote kulaghai,ilimradi tu ayaweke maisha yako hatarini.

46. NGURUWE:Ukijiona unacheza na nguruwe au hata kuwaona nguruwe ,huo ni uchafu kiroho,uzembe na kutokuwa makini katika maisha ya kiroho.

47. SHIMO:Inaashiria shetani ana mipango mibaya dhidi yako ili akuharibu.

48. KUCHEZWA NANYOKA:Hiki ni kuashiria kwamba umefungwa/unatawaliwa na Yule nyoka shetani.

49. .KONOKONO:Inaashiria kudumaa na kuzuiliwa kwa (maendeleo)au kukua kwa mtu.

50. SHULE:Unapoota mara kwa mara kurudi shule kusoma au kuwa shuleni,inamanisha unahitaji (mafunzo)kupata/kupitia mafunzo ili kufanya vizuri katika taaluma yako au utumishi wako katika maisha.kurudi shule za chuni au madarasa inaashiria kudumaa,yaani badala au kupiga hutua mbele unaridi nyuma kimaendeleo.

51. NGONO.Kufanya mapenzi na mtu ambaye siyo mwenzi wako wa maisha ni njia ya kwanza inayothibisha kutawaliwa na tama ya mwili,pili inaweza kuwa msukumo wa pepo kama unaendelea kufanya mapenzi na mtu usiyemjua.Roho ya uzinzi imeshakutawala

52. .MAJOKA:Inaashiria imetawaliwa na roho za majini au umeigia/umeingizwa kwenye agano hilo la mapepo/majini ya pwani baharini au mtoni.

53. NYOTA:Inaashiria ukuu.

54. MOSHI:Inaashiria shutuma na majaribu.

55. .RADI:Kamakulikuwa na mvua kubwa iliyoambatana na mawe ngurumo na radi,inaashiria matatizo na kuchanganyikiwa siku za usoni.

56. .KIJIJI:Unapoota kijiji chako mara kwa mara wakati wewe unaishi mjini hali hiyo inaashiria kuwa laana za mizimu zinajitokeza kukurudisha nyuma.

57. .KUNGURU:Inaashiria kifo au mauti mbele yako.

58. PETE YA NDOA(1):Kama mwanandoa umeota unapoteza pete yako ya ndoa,inaweza kuonyesha/kuashiria unahitaji kuwamwangalifu sana (ndoa)pia inaashiria matatizo ya ndoa mbele yako.

59. .PETE YA NDOA(2)Kama umepewa pete ya harusi ukiwa kijana,inaashiria kuolewa hivi karibuni,pia inaweza kumaanisha mtu (mhusika)ni mwenzi wako wamaisha

60. .KUTEMBEA BILA VIATU:Inaashiria shetani anataka kukuchanganya kukupa aibu na hali ngumu (shida au taabu) .

61. CHAKULA; ukiota unakula chakula au nyama, maana yake, unafanya maagano kwenye ulimwengu wa roho, hasa mikataba ya kichawi

Vitu vingi vinaonyesha namna shetani anavyoweza kutumia mlango wa ndoto, kuyashika maisha yako. Hivyo baada ya kupata maarifa haya, omba juu ya kila kitu chakwako kilichoibiwa kwa njia ya ndoto kirudishwe.
 
Mkuu @ Kichuchunge, vipi kama mhusika kaota anakula chakula cha kawaida, tuseme ugali na mboga za majani, itakuwa na tafsiri mbaya? Kwamba ameota anajipalia ugali na mboga za majani kwa hiari yake bila shinikizo lolote, hiyo ndoto ina ubaya wowote?

Kila ndoto insyohusisha chakula ni ndoto mbaya?
 
Mkuu @ Kichuchunge, vipi kama mhusika kaota anakula chakula cha kawaida, tuseme ugali na mboga za majani, itakuwa na tafsiri mbaya? Kwamba ameota anajipalia ugali na mboga za majani kwa hiari yake bila shinikizo lolote, hiyo ndoto ina ubaya wowote?

Kila ndoto insyohusisha chakula ni ndoto mbaya?
  1. Kuota unakula chakula chochote na mboga za majani katika ndoto kunaonyesha kuwasili kwa riziki kubwa na pesa nyingi kwa yule anayeota ndoto.
    Ikiwa mtu anajiona anakula mboga katika ndoto, hii inamaanisha kwamba atapata riziki nyingi na kuishi maisha ya anasa ya mali. Ila anapaswa kutekeleza masharti.
  2. Ikiwa mboga katika ndoto ni safi, hii inaonyesha kuna mambo fulani fulani ukiyafanya kwa siku za karibuni utaboresha sana maisha yako. Hii inaweza kuwa mafanikio ya malengo ya kibinafsi au mpito kwa hatua mpya ya maisha.
  3. Kuota juu ya mboga katika ndoto pia inaashiria mtu anayeota ndoto kuondoa mambo mabaya anayokabili. Badala ya shida na matatizo, mtu huyo atabarikiwa na vitu vyema vilivyojaa riziki na wema. Ila kuna mambo madogo tu ya kufanya.
 
Kuna ndoto nyingine huwa zinajirudia mara kwa mara, unajua kwa nini.

Tunapojikuta tuna zinazijirudia mara kwa mara, inaweza kuonyesha ujumbe muhimu ambao tunahitaji kuelewa.
Ndoto za mara kwa mara zinaweza kuonyesha matatizo yaliyotokea zamani na bado yapo au yana athari katika maisha yetu.

Ndoto zinazojirudia zinaweza kuwa ukumbusho wa matatizo ya zamani tuliyokumbana nayo ambayo hatukuweza kukabiliana nayo vizuri.
Matatizo haya yanaweza kuwa misiba ya kibinafsi, matatizo ya familia, au hata kutendwa vibaya.
Ndoto hiyo inaweza kuwa onyo kwetu kwamba tunapaswa kukabiliana na matatizo haya na kutafuta njia za kupona kutoka kwao.

Ndoto za mara kwa mara zinaweza kuwa matokeo ya wasiwasi wa mara kwa mara na mkazo wa kisaikolojia tunayohisi katika maisha yetu ya kila siku.
Wasiwasi huu unaweza kujidhihirisha katika picha kama vile ndoto zinazojirudia au alama za kutisha.
Lazima tutafute njia za kuondokana na wasiwasi huu na kufikia faraja ya kisaikolojia. Nitafute
 
Unaweza pia kupata utajiri kwa kutumia tafsiri ya ndoto ila tu ukifanya vitu fulani fulani kwa masharti
 
Unaweza pia kupata utajiri kwa kutumia tafsiri ya ndoto ila tu ukifanya vitu fulani fulani kwa masharti
Nimeota Jana nipo sehemu mandhari ya kilele cha mlima nafukua mawe yote ni dhahabu pure ni nini tafsiri ya hii ndoto, pia wiki mbili nyuma niliota kwamba nimepata pesa za Tsh mil 260 ambazo ni sawa na UGsh mil 400 yaani niliziconvert kwenye Ugandan shilling ndo nikapata mil 400 za Uganda nikiwa kwenye ndoto, sasa asubuhi nimeamka nikachukua simu kuangalia mil 260 ya Tz nilipoibadili kwenda pesa ya Uganda nikakuta kweli ni mil 400 nikastaajabu, pia kabla ya hapo niliota nimejisaidia haja kubwa hadi nikashtuka usjngizini ebu nipe tafsiri ya hizo ndoto zote.
 
Sawa nabii mandoto nakuja kwako kununua mafuta ya upako na chumvi ya upako chap weka namba ya simu na location ndugu aposto.
 
Nimeota Jana nipo sehemu mandhari ya kilele cha mlima nafukua mawe yote ni dhahabu pure ni nini tafsiri ya hii ndoto, pia wiki mbili nyuma niliota kwamba nimepata pesa za Tsh mil 260 ambazo ni sawa na UGsh mil 400 yaani niliziconvert kwenye Ugandan shilling ndo nikapata mil 400 za Uganda nikiwa kwenye ndoto, sasa asubuhi nimeamka nikachukua simu kuangalia mil 260 ya Tz nilipoibadili kwenda pesa ya Uganda nikakuta kweli ni mil 400 nikastaajabu, pia kabla ya hapo niliota nimejisaidia haja kubwa hadi nikashtuka usjngizini ebu nipe tafsiri ya hizo ndoto zote.
Maana ya kawaida huonyesha kwamba mwotaji ana tabia ya kupenda vitu na hamu kubwa ya kufikia malengo yake. Ni ukweli kwamba wewe unapenda sana utajiri utajiri mwingi, unapenda kujifurahisha, kumiliki magari ya gharama kubwa, majengo ya kifahari ... Lakini, kuna tofauti nyingi ambazo zinaweza kuwa mbali na maana ya asili. Inaweza pia kushawishi hali, hali yako ya kiuchumi, shida yoyote uliyonayo.
Unahitaji kujua maelezo haya yote kuwa na maana sahihi zaidi ya kile inamaanisha ndoto ya dhahabu au fedha.

Ina maana gani kuota dhahabu?​

Kama vile tunazungumza juu madini yenye thamani kubwa, au ambayo kwako ni ya thamani, itamaanisha kuwa umemkosa mtu aliye na thamani kubwa kwako. Maana hii ni nzuri, sio ya kupenda mali, kwani haihusiani sana na pesa, lakini na thamani unayompa mtu huyo. Inaashiria ukweli kwamba kulikuwa na uhusiano maalum sana kati yako na huyo, ila kwa sababu ya hali tofauti, iliishia kupotea. Inaonyesha pia kwamba haijachelewa sana, na kwamba tunaweza kuirudisha.

Ndoto kuhusu pesa?​

Ndoto yoyote inayohusisha kuokota fedha, haina maana nzuri kama inavyotegemewa.
Fedha ya kuokota haina tofauti na fedha ya wizi, uchungu anaoupata mtu aliyepoteza fedha hauna tofauti na yule aliyeibiwa, hivyo kuokota pesa sio jambo la ushindi sana.
Sasa inapotokea umeota unaokota fedha za noti, maana yake ni kwamba kuna fedha ambazo unazitamani au zitakujia ambazo sio njema, na ni nyingi kidogo ambazo zitasababisha uchungu kwa upande mwingine, na mara nyingi fedha hizo zinakuwa ni za rushwa, au kupewa na mtu aliyeiba, au kupewa na mtu ambaye kazipata kwa njia isiyo halali, iliyosababisha uchungu kwa mwingine.

2) Kuota Sarafu
Unapoota unaokota sarafu, tena wakati mwingine zimejipanga mstari mmoja, tafsiri yake ni hiyo hiyo kama ya fedha za noti, isipokuwa, sarafu inawakilisha uchache wa fedha, maana yake kuna fedha ambazo si nyingi sana zitakujia au zimeshaanza kukujia ambazo si safi.
Fedha za namna hiyo hazina baraka yoyote kutoka kwa Mungu zaidi ya laana.
Hivyo uonapo mazingira kama hayo yanatokea katika maisha yako, mazingira ya kupewa au kupata fedha isiyo halali, iwe nyingi au kidogo, ambayo itasababisha uchungu kwa mwingine mfano ule ule wa mtu aliyeibiwa fedha au kutapeliwa..huna budi kuikwepa na kutafuta jinsi ya kutegua. nitakusaidia huko huko ulipo
 
Ndoto inayohusiana na kung'atwa na nyoka
  • Ikiwa mtu anaota anamuona nyoka na hasogei, basi hii ni ishara ya wema mwingi na riziki pana inayokuja juu yake, na kwamba atapata pesa nyingi hivi karibuni.
  • Ikiwa mtu binafsi anaona katika ndoto kwamba nyoka anamshambulia, basi hii ni ishara ya wapinzani wake wengi na maadui, na lazima awe na tahadhari kali ili asijeruhi au kuumiza.
  • Unapoota ndoto ya kuua nyoka, hii inaashiria uwezo wako wa kuwaondoa maadui zako na kufikia malengo na malengo yote unayotafuta.
  • Nyoka anayemshambulia mwotaji anaashiria ubaya unaomzunguka na ufahamu wake wa kujilinda dhidi yake. Ama kwa yeyote anayeota kwamba anamkata nyoka, hii inathibitisha mema na faida ambazo zitampata katika kipindi kijacho.

Wanawake​

  • Ikiwa msichana ameota nyoka akimng'ata mikononi mwake, basi hii ni ishara ya dhambi nyingi na maafa ambayo anafanya kwa kweli na kutojitolea kwake kwa mafundisho ya dini yake au kutekeleza maombi yake, kwa hivyo lazima amgeukie Mungu pamoja na dua na toba ili aondoe dhambi hizi na awe radhi nazo.
  • Ikiwa mwanamke singo ataona nyoka akimng'ata kwenye mguu, hii ni ishara kwamba hivi karibuni atawaondoa wapinzani na maadui zake wote.
  • Ikitokea msichana ataona nyoka amemkandamiza shingoni, hii inapelekea uwezekano wa kubakwa au kunyanyaswa, Mungu apishe mbali, au atapitia mgogoro mgumu sana katika kipindi kijacho kitakachodumu. naye kwa muda mrefu.
  • Kwa ufafanuzi wa ndoto ni DM nikufafanulie zaidi
 
Niliwahi kuota nina mke wangu tayari,

kajifungua watoto mapacha watatu,

wa kike wawili wakapotea nikabaki na mmoja wa kiume ambaye nikampa jina la Ibrahim.

Yeye alivyozaliwa tu, muda huo akawa anatembea na pia anaongea.

Je, inamaanisha nini hii ndoto?

Kumbuka nipo single Sina hata mke wala mchumba.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom