Maswali ya kijinga na majibu ya hasira. Ongeza na ya kwako

PNC

JF-Expert Member
Feb 3, 2015
8,107
14,352
Maswali ya kijinga na majibu ya hasira;

1. Mtu anakuona umejilaza na macho umefunga anakuuliza umelala?..... Hapana najaribu kufa.

2. Mvua inanyesha halafu unatoka nje kisha mtu anakuuliza unakwenda na hii mvua?..... Hapana nitakwenda na inayofuata.

3. Rafiki yako anapokupigia simu yako ya mezani afu anakuuliza uko wapi?..... Niko kanisani naombewa.

4. Wanakuona umelowa ukitokea bafuni wanakuuliza umetoka kuoga?...…. Hapana nimeanguka kwenye bakuli la choo.

5. Umesimama nje ya lift kwenye jengo la sakafu ya chini kisha unaulizwa unapanda juu?..... Hapana ninasubiri chumba changu kije kinichukue hapa chini.

6. Unamnunulia mkeo maua anakuuliza hayo ni maua?..... Hapana mke wangu, ni karoti.

7. Uko kwenye foleni ya kulipa tiketi ya kuingia uwanjani kucheki mpira, rafiki yako anakuuliza na wewe unaenda kuangalia mpira?..... Nimekuja kulipa ada ya shule.

8. Ongezea na yako
 
Back
Top Bottom