Maswali ya kijinga na majibu ya hasira. Ongeza na ya kwako

Mtu anakuuliza "umeshakula?" Unamjibu "hapana" anakuambia "ahaaa" alafu anaendelea na mbishe zake..

Tunaitaga mswali ya kiwaki
 
Maswali ya kijinga na majibu ya hasira;

1. Mtu anakuona umejilaza na macho umefunga anakuuliza umelala?..... Hapana najaribu kufa.

2. Mvua inanyesha halafu unatoka nje kisha mtu anakuuliza unakwenda na hii mvua?..... Hapana nitakwenda na inayofuata.

3. Rafiki yako anapokupigia simu yako ya mezani afu anakuuliza uko wapi?..... Niko kanisani naombewa.

4. Wanakuona umelowa ukitokea bafuni wanakuuliza umetoka kuoga?...&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];. Hapana nimeanguka kwenye bakuli la choo.

5. Umesimama nje ya lift kwenye jengo la sakafu ya chini kisha unaulizwa unapanda juu?..... Hapana ninasubiri chumba changu kije kinichukue hapa chini.

6. Unamnunulia mkeo maua anakuuliza hayo ni maua?..... Hapana mke wangu, ni karoti.

7. Uko kwenye foleni ya kulipa tiketi ya kuingia uwanjani kucheki mpira, rafiki yako anakuuliza na wewe unaenda kuangalia mpira?..... Nimekuja kulipa ada ya shule.

8. Ongezea na yako
We jamaa wew,hayo ni majawabu mujarabu
 
8. Upo na demu room, mmeanza kuchezeana, kissing, romance nzito,. Umevua umebaki kifua wazi, ukambeba hadi kitandani. Unamvua nguo anakuuliza unataka kufanya&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];?
Nataka kwenda kufua
We jamaa wew
 
Mko mnapandisha zenu mlima kilimanjaro kwenda kutalii unakutana na best yako kipenzi anakuuliza.

Vp nawewe unapanda???????????

Jibu: Apana mimi naotesha.
 
Nilijikata kiwembe wakati nakata kucha nikaanza kulia kwa sababu maumivu makali, mtu akaniona akaniliuza

Yeye:Na wewe mkubwa ivoo unalia?
Mimi: naimba wimbo wa Taifa
 
Maswali ya kijinga na majibu ya hasira;

1. Mtu anakuona umejilaza na macho umefunga anakuuliza umelala?..... Hapana najaribu kufa.

2. Mvua inanyesha halafu unatoka nje kisha mtu anakuuliza unakwenda na hii mvua?..... Hapana nitakwenda na inayofuata.

3. Rafiki yako anapokupigia simu yako ya mezani afu anakuuliza uko wapi?..... Niko kanisani naombewa.

4. Wanakuona umelowa ukitokea bafuni wanakuuliza umetoka kuoga?...&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];. Hapana nimeanguka kwenye bakuli la choo.

5. Umesimama nje ya lift kwenye jengo la sakafu ya chini kisha unaulizwa unapanda juu?..... Hapana ninasubiri chumba changu kije kinichukue hapa chini.

6. Unamnunulia mkeo maua anakuuliza hayo ni maua?..... Hapana mke wangu, ni karoti.

7. Uko kwenye foleni ya kulipa tiketi ya kuingia uwanjani kucheki mpira, rafiki yako anakuuliza na wewe unaenda kuangalia mpira?..... Nimekuja kulipa ada ya shule.

8. Ongezea na yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom