Maswali haya yakipata majibu sahihi, sintofahamu ya uwekezaji bandarini itaondoka. DP World ni kampuni ya kawaida ya biashara, haina tatizo lolote

Misozwe

Member
Dec 23, 2022
21
26
  • Hakuna anayepinga uwekezaji, utaratibu tu ufuatwe
  • Usimamizi wa bandari sio rocket science
  • Upinzani wa kuwekeza kwenye bandari
  • Serikali kukiri kushindwa kusimamia bandari ijiendeshe kwa ufanisi
  • Maswali ya msingi yanayopaswa kujibiwa
  • Uzoefu wa biashara wa DP World sehemu mbalimbali duniani
Jambo la kwanza na la msingi kabisa, kwa maoni yangu na ya wengi, hakuna anayepinga uwekezaji kwenye bandari. Actually, uwekezaji kwenye bandari umechelewa, sana. Uwekezaji umechelewa kwa miaka 60 na zaidi pengine, lakini pamoja na kuchelewa huko, hakuhalalishi mchakato wa uwekezaji ufanywe bila utaratibu na kutowapa nafasi watanzania, ambao ndio wamiliki rasilimali yenyewe ya bandari, nafasi ya kutoa maoni yao. Wananchi walio wengi.

Usimamizi wa bandari sio rocket science. Ni sekta ambayo ilikuwepo hata kabla ya Yesu. Bandari zetu za asili zilikuwepo kabla ya utumwa na ukoloni na ziliweza kuwapokea wageni kutoka ughaibuni; waarabu, wahindi na wazungu waliotuletea vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na nguo, mazao, utamaduni, dini na mambo mengine. Kuna literature ya kutosha online na offline kuhusu biashara, historia na uendeshaji wa bandari dunia nzima. Hivyo basi viongozi wetu na walio kwenye mamlaka na taasisi husika, pamoja na kwamba wana ufahamu mkubwa kuhusu bandari, lakini wasione kwamba sisi wananchi wa kawaida hatuna lolote tunalojua kwa kutotaka at least kusikiliza maoni yetu. Naandika haya nikiwa mwanamchi wa kawaida kabisa ambaye nina maoni yangu na ninayetaka kupata ufafanuzi wa kina kuhusu mjadala mkubwa huu unaondelea kuhusa bandari.

Inasemekana kuna baadhi ya wanasiasa wa upinzani wanatumia mjadala huu kama ajenda ya kujiimarisha kisiasa, sina uhakika na hili kwa sababu sijaona ushahidi wake. Inasemekana kuna wafanyabiashara wanaeneza propaganda mbaya kuhusu uwekezaji huu kwa sababu wananufaika na hali iliyopo sana, sina uhakika na hili kwa sababu sijaona ushahidi wake.

Lakini jambo ambalo nina uhakika nalo ni kuwa, serikali, kwa maana ya uongozi wa bandari pamoja na taasisi zinazoisimamia, imekiri hadharani kuwa wameshindwa kuiendesha bandari kwa ufanisi. Niwapongeze kwa ujasiri huu, sio wengi katika serikali zetu za kiafrika wanaokiri hadharani kuwa wameshindwa jambo. Nawapongeza pia kwa kwenda hatua moja mbele zaidi kwa kwenda kutafuta suluhisho na kulitetea hadharani kwa nguvu kubwa suluhisho hilo. Ni hatua njema, ila sintofahamu imetokea kwa sababu wananchi, wenye mali yao, hawakuhusirikishwa kwenye mchakato tokea mwanzo. Ila, nafikiri halijaharibika neno, nafasi ya kujirekebisha bado ipo.

Kutokana na maelezo hapo juu na yatakayofuata hapo chini; maswali yafuatayo yakijibiwa na serikali, kwa maoni yangu, hakutakuwa tena na hofu wala pingamizi, wananchi tutakuwa tumeelewa: (Kuzingatia IGA, HGA na mikataba ya utekelezaji uwekezaji itakayofuata, pale inapohusika)
  • Ni sababu gani serikali imekubali ku limit options zake kwa kuingia IGA na Dubai kwenye huduma za bandari wakati players wako wengi duniani kama references hapo chini zinavyoonyesha (hasa ya India)
  • Mkataba huu ni wa concession au wa hisa?
  • Kama ni concession, ni ya muda gani? Kote ambako DP World wameingia mikataba ya concession, muda wa mikataba imetanabaishwa bayana.
  • Kama ni hisa, mgawanyo wa hisa ukoje, ni nani na nani wanaingia kwenye huo mgawanyo?
  • Kama ni concession, wanawekeza kiasi gani, kama ni shilingi trilioni 2 zinazosemwa, je wananchi na wafanyabiashara wa Tanzania hawawezi kuwekeza kiasi hicho kwa fedha kwa miaka kumi (kwa sababu tunaambiwa mapato yatafika trilioni 37 kufikia mwaka 2033) na tukaajiri hao wataalamu wa nje waje kusimamia bandari, tuwanunulie mifumo na vifaa sisi tusimamie mambo ya fedha pekee? Kwanini tusiwaulize TICTS ni wapi walipata changamoto tukazitumia kujifunza? Ikiwa watanzania tutashindwa, kwanini serikali isitengeneze kampuni ya ubia na wawekezaji kama ilivyofanyika kwa kampuni za Twiga Minerals na Kabanga Nickel ili kuendesha bandari? Kama tukishindwa hayo mawili kwa nini tusitangaze tenda tupate best value for resourses tulizonazo na kwa masharti yetu wenyewe? Ikishindikana kabisa ndio tuwaite individual companies kama DP World na wengine.
  • Mgawanyo wa mapato unakuwaje? Kwa maoni yangu, haitakuwa na faida iwapo mapato yatafika shilingi trillioni 50 kwa mwaka, halafu mgao unakuwa shilingi trillioni 45 wawekezaji, shilingi trillioni 5 serikali
  • Kwanini mkataba huu unahusisha GATI nyingi na pia na bandari nyingine kwa kampuni moja wakati kwa uzoefu kwingineko hapo chini taratibu haziko hivyo?
Kwenye mradi mkubwa kama huu, kwanini utaratibu wa kawaida wa tenda haukufuatwa? Ni vigezo gani vimetumika kufanya single sourcing? Mbona utaratibu wa tenda ni wa kawaida katika biashara hii kama ambapo DP World imekuwa ikishiriki tenda hizo, na kushinda na kushindwa kama maelezo hapo chini yanavyoeleza?

Wanashinda tenda:
DP World, kampuni inayoongoza ulimwenguni katika kutoa suluhisho bunifu za bandari, imetia saini makubaliano ya kutoa huduma kwa kipindi cha miaka 20 na Serikali ya Angola kwa ajili ya kuendesha Gati la Matumizi Mchanganyiko (MPT) katika Bandari ya Luanda. (DP World signs 20-year concession agreement with Angola)

Kampuni ya Dubai inayosimamia operesheni za bandari imepewa ruhusa ya miaka 25 kukuza na kuendesha kituo kipya cha vifaa (logistics) huko Kigali, Rwanda.
(https://www.rba.co.rw/post/PHOTOS-President-Kagame-inaugurates-Kigali-inland-cargo-handling-facility)

Wanaingia ubia
Muendeshaji wa bandari za Dubai, DP World, umetangaza kuwa serikali ya Ethiopia imechukua hisa za asilimia 19 katika Bandari ya Berbera nchini Somaliland.
Chini ya makubaliano hayo, DP World itamiliki hisa za asilimia 51 katika mradi huo, huku Somaliland ikiwa na asilimia 30 na Ethiopia ikimiliki asilimia 19 zilizobaki
(Ethiopia acquires 19% stake in DP World's Somaliland port)

Wanashindwa tenda:
Baada ya kupoteza mbio za kupata makubaliano ya Bandari ya Kontena ya Jawaharlal Nehru ambapo ilishika nafasi ya nne kwenye mnada uliopita mwezi uliopita, D P World sasa inabaki na nafasi inayojitokeza katika bandari ya Deendayal iliyoko Kandla katika jimbo la Gujarat kuendelea kudumisha ushawishi wake mkubwa kwenye pwani ya magharibi. (D P World, one of top foreign investors in ports, running out of options as contract terms nears end - ET Infra)

Wanapata hasara (wao kuendesha bandari yetu haimaanishi faida iko guearanteed):
Mmiliki wa P&O Ferries aliye na makao yake makuu Dubai amepoteza hadhi yake kama mshirika rasmi katika mojawapo ya miradi mikubwa ya bandari huru ya serikali, baada ya hasira kubwa ya umma kufuatia kufutwa kazi kwa ghafla kwa wafanyakazi 800 mwezi uliopita.Mawaziri wamethibitisha kuwa DP World, kampuni kubwa ya vifaa kutoka Falme za Kiarabu iliyo nyuma ya P&O, haina tena jukumu kuu kama "mshirika" katika bandari huru ya Solent baada ya kujiuzulu kwa mkurugenzi wake wa kibiashara wa Uingereza kutoka bodi ya mpango huo wiki iliyopita. (P&O Ferries owner DP World loses status as partner in Solent freeport)

Dubai Imeuza Hisa katika kwenda Mfuko wa Pensheni wa Canada ili Kupunguza Deni (Dubai Sells Stakes in Key Assets to Canada Fund to Cut Debt)
 
Usitegemee kupata majibu ya hizo hoja toka serikalini, hawako tayari kumfunga paka kengere.
Nahisi Sa100 ndio kashinikiza jambo kwa nia nzuri. sasa waliochini badala ya kushauri taratibu ya kufuata wakasema na iwe hivyo mheshimiwa. Hapo ndipo walipoingiza kinyesi ofisini sasa kuna vundo linanuka. Wanaogopa kusema uvundo wa mheshimiwa. Wanabaki kutetea. jahazi lisizame. Na yeye hataki kuwatosa watu wake kwa kuwa imani kwa wengine hakuna.
 
Hujafatilia vizuri, zabuni zilitangazwa na mpaka kampuni ya India ipo kwenye kinyang'anyiro. Fatilia.

Serikali haikuingia IGA na DP World, serikali imeingia IGA na Dubai.
 
IMG-20230720-WA0039.jpg
 
Back
Top Bottom