Dah...hii kitu isikieni tu mazee...mi nilienda Parlour moja mitaa ya K'ndoni jiran na makaburini....ni hatareeeeeee..
Kwanza kufika tu mapokezi nikakutana na warembo kibao..wananipokea kwa bashasha sana..walikuwa kama sita hivi.wenyewe wakanambia chagua unaemtaka...mi nukijua ni huduma ya massage tuuuu...mara nikaambiwa niende bafuni kuna maji ya uvuguvugu,mara nikapelekwa chumbani...mafuta ya cloves yana uvuguvugu,powder na mazaga kibao..nikaulizwa "tuanze na soft au hard massage?"....kidume sijui lolote.
Nikakandwa huku na kule...vidole masikioni...mara nikapewa massage ya kichwa...walltaah kichwa kikawa chepesiiiiiiiiiiiiiiiiiiii......
Akili imekuja kurudi nipo Magomeni Usalama konda ndo ananidai nauli...nacheki mfukoni nimebakiwa na jero,wakati parlour niliingia na elfu sitini...hata sijui nilizitoaje,akili inakumbuka swali la mwisho lilikuwa nikuwekee mziki gani...nikajibu slow jams,chumba gizagiza ni mwanga wa mshumaa tu...kaa hujawahi enda haya maeneo usiridie tena kujarbu wala usithubutu katuuuuuu
..