Wadada, niulizeni kitu chochote kuhusiana na huduma za salon, hair & nails

MillionHairs

JF-Expert Member
Jul 31, 2013
803
406
image.jpg image.jpg image.jpg

Wapendwa ndugu zanguni hasa wadada.. Kama kuna kitu au vitu vilikuwa vinakutatiza kuhusiana na swala zima la urembo wa salon, basi chukua nafasi hii kuniuliza swali lolote lile linalohusiana na huduma za salon.

Hair Reluxer
Hair treatment
Hair special treatment
Misuko
Hair designing &
Beauty clinic (full package)

Je, una tatizo lolote la nywele zako za asili? Au una tatizo lolote la kucha zako za asili? Yaliyo ndani ya uwezo wangu nitayajibu na yale ambayo yatakuwa nje ya uwezo wangu basi nitayaacha.

"UZURI UNAZALIWA NAO ILA UREMBO NA USAFI WA MWILI UNAJIPA MWENYEWE"

Pia kuna vitu kama;
Skin waxing
Detoxfication
Body scrub
Facial
Face mask
Body massage
Pedicure & manicure
Hand Gel colors & aqrilic extension nails
Kope na kutinda nyusi

Hivi vyote hapo juu tunaviita Beauty clinic…So kama una chochote kutoka kwenye package hiyo usisite kuniuliza pia.
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    436.4 KB · Views: 5,175
  • image.jpg
    image.jpg
    362.2 KB · Views: 4,419
  • image.jpg
    image.jpg
    544.6 KB · Views: 4,172
  • image.jpg
    image.jpg
    495 KB · Views: 4,014
Mimi niliweka Dr miracles Regular no lye relaxar,nataka nihamie olive oil normal no lye relaxar,je kuna ubaya-?
 
Mara kwa mara huwa nawashwa hasa katikati cha kichwa hata kama hamna mba na hii hupelekea nywele za eneo hilo kukatika kabisa utadhani nimenyolewa nimetumia mafuta mengi tu bila mafanikio je tatizo ni nini au ni dalili za upara? Kwa ujumla nywele zangu ni kavu na zinakatika kwa haraka
 
Mimi niliweka Dr miracles Regular no lye relaxar,nataka nihamie olive oil normal no lye relaxar,je kuna ubaya-?
Hakuna ubaya...lakini je hiyo Dr miracle mara ya mwisho umeweka lini? Hiyo Olive oil yakupasa uweke baada ya miezi miwili
au mitatu tokea uachane na hile ya kwanza.

Swali: nywele zako ni laini au ngumu?
 
Nina relaxer na sasa nataka kubadili na kuweka curl je ni muda gani natakiwa kusubiri kabla ya kuweka hiyo curl
 
Chocolate,
Hakuna cha upula wala nini...sema tu hizo nywele zako hazijapata chakula kizuri zikashiba. Kuna treatment fulani nitakuelekeza na mafuta yake ya kupaka...within 3 month utakuwa na msitu wa nywele.

By the way kwa sasa unazilisha chakula gani? (Product)
 
Nina relaxer na sasa nataka kubadili na kuweka curl je ni muda gani natakiwa kusubiri kabla ya kuweka hiyo curl
Kwanza yakupasa kusubiri hadi hiyo reluxer inakwisha yote kama siyo kupotea kabisa kwenye nywele zako then zikishaota nywele zako za asili ambazo hazina dawa ndipo unaruhusiwa Curl au permanent curl
 
Kwanza yakupasa kusubiri hadi hiyo reluxer inakwisha yote kama siyo kupotea kabisa kwenye nywele zako then zikishaota nywele zako za asili ambazo hazina dawa ndipo unaruhusiwa Curl au permanent curl
Hapo kwenye bold ndio hasa hitaji langu. Nina zaidi ya 4 months toka niweke relaxer , je kama nitazikata zenye dawa na kubaki na natural hair itawezekana????Ili hizo zitakazobaki ndio niweke permanent curl au natakiwa kusubiri zaidi
 
Ni mafuta gani yanafaa kufanyia massage hasa kwa nyumbani?
Mkuu sorry for my late reply bado niko kazini na busy kidogo...so tuvumiliane.

Okay, unapenda massage gani? thai,soft,au hard massage? Nijibu ili nijue ni mafuta gani yakupasa utumie.

Mwisho...unasumbuliwa na sehemu gani mwilini kiasi kwamba unahitaji massage? I mean viungo
 
Hakuna cha upula wala nini...sema tu hizo nywele zako hazijapata chakula kizuri zikashiba. Kuna treatment fulani nitakuelekeza na mafuta yake ya kupaka...within 3 month utakuwa na msitu wa nywele.

By the way kwa sasa unazilisha chakula gani? (Product)

Nitashukuru sana kupata hiyo treatment pamoja na hayo mafuta. Kwa sasa ninatumia product za olive
 
Back
Top Bottom