"aisifuye mvua imemnyeshea" si za nyuma kidogo nilifanikiwa kwenda kwenye ofisi moja ya kinyozi kwa ajili ya kwenda kutengeneza nywele zangu na pia uso.hivyo nikamweleza kinyozi aina ya mnyoo niliotaka naye pasipo bugdha akanitendea kwa kadri ya matakwa yangu.
pembeni yangu wakti huo wote wa tukio lile likiendelea walikuwa wameketi wadada masham sham wanne wakiwa kwenye sofa za pale ofisini. ni kwa nadra sana walikuwa wakiongea....aghalabu walikuwa wakitumia simu makini zao nyie mnaita smartphone. basi kinyozi alipomaliza kuninyoa aliinuka dada mmoja kipusa kweli kweli aliyekuwa amevalia siketi nyepesi fupi iliyokuwa juu ya mapaja yake "fahari ya macho haifilisi duka" na kuona si kuchukua.so nilifanikiwa kuona.alikuwa mashallah mtoto wa kike yule.
yule dada alikuja kunisemesha kimahaba masikioni " uncle twende huku" akiwa ameniinamia na kuniwekea mkono wake mmoja begani mwangu. hali ile ilinishtua kidogo sababu sikuona sababu ya kuninong'oneza na zaidi zaidi kunishika begani.basi nikainuka kumfuata huku akitingisha sehemu yake ya nyuma kma bata atembeavyo.siku fanya hiyana kumfuata kwenye chumba husika ambako tulikuwa sisi wawili tu. nikajisemea moyoni "fuata nyuki ule asali"
dada aliniomba nikae kwenye kiti cha mlazo... nilikaa pasipo ukaidi.akaniweka kitaulo shingoni na kuanza kunipaka mafuta ayajuaye yeye... asalaleeehhh... yule dada alikuwa anani sawijisha usoni kwa mikono yake laini huku kichwa changu amekiweka usawa wa maziwa yake.yaani sasa nimeegemezwa kwenye maziwa yake.huku akipumua kwa ukaribu kabisa usoni pangu.bahati nzuri hakuwa na pumzi mbaya.she had a very nice breath. "kweli baniani mbaya kiatu chake dawa" pamoja na nia yake ovu ila alibarikiwa hilo jambo zuri kiukweli
yule dada alikuwa akionesha ufundi wake wa kunitomasa kwa kunizungushaia vidole masikioni,mashavuni na shingoni huku kifua chake pia kikihusika kwa nafasi kubwa kukishikilia kichwa changu kisitoke katika himaya yake.kiukweli ulikuwa ni wakati wa mateso makubwa kwangu. nami nilipiga moyo konde nikasema hapa leo ni vita kati yangu na shetani.nikasema kimoyomoyo nitamchosha shetani ile mbaya then round ya mwisho namgonga TKO.yule dada aliendelea kunishawishi sana kwa kila kitendo alichofanya alikuwa kabisa namwona akifanya kwa kufuata maelekezo ya mama/shangazi yake shetani.nikawa najisemea "maji ya moto hayaunguzi nyumba"
na muda mwingine alikuwa anauliza "upo ok?" au hapo "nakushika vizuri" akitaka kupata maoni yangu.nami nlishaamua kupigana vita hivi kimya kimya.nilikuwa natikisa kichwa tu huku nikilani jinsi ambavyo huyu dada aliamua kunifanyia ufirauni wake pasipo kujali kuwa mimi sikufuata hayo mengine.mwishowe kabisa alimaliza kuniosha na kuniuliza" kuna kingine ungependa nikufanyie" nilimjibu tu "hamna" maana niliona "ni kheri nusu shairi kuliko shari kamili "sikutaka huduma yake nyingine so nikafanikiwa kumwondoa kwa TKO round ya 12. nikatoka mimi mbabe...
wanawake... jaribuni sana kujifunza kuwanawisha waume zenu, jaribuni kwenda nao barbershop naamini kuna wanaume wengi wanategeka kwa style hii ya wadada hawa ambao binafsi kipindi cha nyuma nimeshawahi kuwala wawili. wadada wa aina hii hii. na yule mmoja ambaye alimgombanisha ustaadhi na fisi. ni wadada hawa hawa wa barbershop. ni kama wamefundishwa na mama yao shetani namna ya kuwatega wanaume... sasa hapa nawaambia tu kuwa "mchelea mwana kulia atalia yeye" msije sema tulikuwa hatuyajui haya. sababu wahenga walisema "mdharau mwiba mguu huota tende"