Maskini rais wanguuu...

Status
Not open for further replies.
Mwakasege,
Shukran sana na kwa wale waliokuwa wakitetea habari hizi kuwa hayakuwa makosa mtaficha wapi sura zenu?. Wadanganyika waliweza tunga kilichotokea kama vile wao walikuwepo maadam tu kukosha jina ama majina ya wahusika. Hivi kweli tutakuja jifunza kuwa na subira kutafuta ukweli wa swala.
 
'Hundi aliyokabidhiwa Rais ilikosewa'

sogeza Habari Zinazoshabihiana
• Mfanyabiashara wa kiasia abambikiwa hundi ya m.7/- 31.05.2007 [Soma]
• Waliokosa mikopo Chuo Kikuu kulipwa leo 22.09.2006 [Soma]
• Vodacom kuwekeza zaidi ya bilioni 150/- 31.03.2006 [Soma]

Na Mwandishi Wetu

OKTOBA 8 mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete, alizindua Mfuko Maalumu kwa ajili ya Mafunzo kwa Maofisa Watendaji Wakuu wa Serikali.

Katika hafla hiyo, Rais alipokea michango ya hundi tatu tofauti ambapo Serikali ilitoa hundi ya dola 200,000 za Marekani, CEO Roundtable Tanzania dola 200,000 na Benki ya Dunia dola 300,000.

Hata hivyo hundi ya mfano iliyotolewa na Benki ya Dunia, iliandikwa kimakosa huku tarakimu zikitofautiana na maneno kwenye hundi hiyo, badala ya maneno kusomeka Three Hundred Thousand Only (Laki Tatu tu), iliandikwa Two Hundred Thousand Only (Laki Mbili tu).

Waandaaji wa hafla hiyo, kampuni ya Enigma Productions, wameomba radhi kwa makosa hayo ambayo Mkurugenzi wake, Bibi Pauline Rupia-Boateng, alisema jana kuwa hayakukusudiwa.

Haya sasa, yangu macho.
 
Mtoto wa Rupia .......

Makosa yalikuwa makusudi kabisa tena ya kudhalilisha sana. Wasidhani wote wajinga sisi.

Kuna dalili za wazi kabisa za kuonyesha kuwa serikali sio makini. That was another way of sending msgs kwa wasioelewa taratibu kama zile. Na wamefanikiwa kuwateka baadhi ya watu, hata humu JF.

She should learn better ways of doing that!
 
niliwahi soma kitabu toka ghana kiitwacho Beautyful ones are not yet born mwandishi alikosea neno Beautyful badala ya beautiful, kama linavyoandikwa. lengo la makosa katika title ni kutuma ujumbe kuwa kukosea title kulitokana na elimu inayotolewa kuwa insufficient ambayo inasimamiwa na serikali.

Pia ililenga kuonyesha namna serikali ilivyooza sio tu kielimu bali hata kimaadili. Je kwanini bwana Rupia asiwe kama hao wanaoongelewa na hii title?
 
Mushobozi mi pia nilikisoma kitabu hicho A-level miaka ileeee, ambapo mwanzoni nilishindwa kuelewa kwa nini Bw. Ayi Kwei Armah (mwandishi) aliandika neno "Beautyful" badala ya "Beautiful", lakini wakati wa uchambuzi wa kitabu kile nilikuja kuelewa kwa nini ALIAMUA kuandika hivyo.

Yaani kuonesha uozo,ufisadi,kutowajibika,kukosekana umakini na kila ujinga na upumbavu kwa viongozi wa Serikali na sekta ya Umma kwa ujumla.Hivyo basi sioni haja ya kumlaumu huyu binti Rupia kwani yeye na hata wazazi wake wamefaidika na huu mfumo wa kizembe, kifisadi, kinyonyaji, etc kiasi kwamba wanashindwa kuona vizuri kwani ufisadi,tamaa ya fedha,rushwa VIMEWAPOFUA kiasi kwamba hawaoni baya au ovu lolote.

Na kwa viongozi wetu (wanaowakilishwa na Kiwete mwenyewe) inaonesha ni kiasi gani walivyopofuka na kushindwa kuona mambo ambayo yako ndani ya uwezo wao.Wengine hapa walijaribu kuwasingizia wasaidizi wa Muungwana kwamba hawakuwa "makini" kugundua "kosa" lile.

Swali ni je ina maana yeye Muungwana binafsi hana kabisa uwezo wa kugundua makosa ya namna hiyo? Kama hiyo ni kweli basi twafa,kwa maana ni makosa mangapi ambayo yamefanyika nyuma ya pazia ambayo hayajawekwa wazi?

Pia hii inaonesha ni kwa jinsi gani wasaidizi wa Muungwana wanavyoweza kupindisha mambo kwa faida yao binafsi bila yeye kujua na kikubwa zaidi hii scenario inaweza kuelezea kwa nini Karamagi alisign mkataba wa Buzwagi huko UK bila Muungwana "kujua" hali wote walikuwa ziarani "pamoja"...Mungu Ibariki Taznzania...
 
DU hii kweli kali kuliko two hundred thouusand wakati upande mwingine ni 300,000.00. kweli hii ni kali ya mwaka.
 
nimegundua haya ni makosa ya kawaida sana kwa World Bank hebu angalieni hapo chini kwenye hiyo kitu nimetoa kwa website yao? Yaani USD 300 ni sawa na milioni 3.5 za Tanzania? Hawa jamaa nao hawako serious.

Community Projects Uplift Livelihoods in Rural Tanzania



Dar es Salaam , August 13, 2007- An elderly group in Bukabile village, Magu District in Shinyanga region owns six acres of land. The Tanzania Social Action Fund (TASAF) which receives support from the World Bank visited the group and provided an input of US $300 (approximately 3.5million Tanzania shillings) to start horticultural gardening under the income generating activities. The two acres have been cultivated and planted with tomatoes, onions and cabbage. Four months after the intervention, the group generated about US $ 240 (about 2.9m/-) by selling of horticultural products from the two-acre garden. The group was so happy that such intervention managed to uplift the lives of beneficiaries out of poverty within such a short time. The group was also able to get technical skills from the Local Government Authorities (LGA) agricultural extension officers that helped to increase yields. Mr. Bonaventura Mashishanga (62) and father of four says he was able to send two of his children to school from dividend he got from the group. "I will use the skills I got from the group and start my own garden," he said while thanking TASAF for the intervention.

For more information, refer to www.worldbank.org.tz.

Contact

In Dar es Salaam: Ichikaeli Maro-Mzobora
255 22 2163200
imaromzobora@worldbank.org
 
nimegundua haya ni makosa ya kawaida sana kwa World Bank hebu angalieni hapo chini kwenye hiyo kitu nimetoa kwa website yao? Yaani USD 300 ni sawa na milioni 3.5 za Tanzania? Hawa jamaa nao hawako serious.

Mtoto wa Mkulima umenifumbua sana kwa taarifa hii, inaelekea mara kwa mara huwa wanatoa makadirio yao kimakosa hasa pale wanapotoa juu ya maendeleo ya nchi zinazoendelea kiuchumi ambapo wamekuwa wakiiweka Tanzania kama nchi masikini kwa kutoa tarakimu mbaya, kuna njia nyingi sana za kumdumaza mtu mathalani wewe na mwanao, ikiwa kila mara utakuwa unamwambia mwanao kuwa ni mjinga usishangae mwanao akawa mjinga kwa sababu ya kauli yako.

Mbaya zaidi akiweza kujikwamua na hali fulani halafu wewe ukaja na tamko rasmi ukamwambia hata iweje haji kufanikiwa kwa sasbabu hizi na zile kamwe kijana wako hataendelea. Hivi ndivyo World Bank imekuwa ikifanya kwa nchi masikini. Maendeleo halisi ya nchi yetu yapimwe na sisi wenyewe kwa juhudi zetu hawa jamaa hawatatusaidia kitu ng'oooooo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom