Mbunge Martha Gwau: Mkoa wa Singida Umetimiza Miaka 60 tangu Kuzaliwa Kwake Tarehe 16 Oktoba, 1963.

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

MBUNGE MARTHA GWAU ANAWAKARIBISHA WANA SINGIDA WOTE KATIKA MAPOKEZI YA RAIS SAMIA MKOA WA SINGIDA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Mhe. Martha Nehemia Gwau anawakaribisha Wananchi wote wa Mkoa wa Singida katika Mapokezi ya ziara ya kikazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkoa wa Singida itakayoanza tarehe 15 Oktoba, 2023 Mpaka tarehe 17 Oktoba, 2023.

Ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkoa wa Singida itaambatana na Sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya kuzaliwa kwa Mkoa wa Singida tangu tarehe 15 Oktoba, 1963 zitakazofanyika katika Viwanja vya Bombadia Mjini Singida, tarehe 16 Oktoba, 2023 kuanzia Saa Kamili Asubuhi

Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya kuzaliwa kwa Mkoa wa Singida (Tarehe 16 Oktoba, 1963) atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Hii ni ziara ya kwanza ya kikazi ndani ya Mkoa wa Singida kwa Rais Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani

Rais Samia Suluhu Hassan kwa mwaka wa fedha 2022-2023 katika Mkoa wa Singida ametoa fedha Shilingi Bilioni 9 zilizotumika kujenga Shule mpya 12, Madarasa, Ofisi za Walimu na Nyumba za Walimu

Aidha, Rais Samia Suluhu Hassan atakwenda Itigi kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Barabara ya Lami kutoka Itigi kuelekea Mbeya. Pia, atakwenda Ikungi kuzindua Vituo Viwili vya Polisi vya Wilaya ya Ikungi na Wilaya ya Mkalama. Rais Samia atazindua Daraja la Bilioni 11 lililojengwa Mkalama.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-10-14 at 19.34.35.mp4
    9 MB
  • WhatsApp Video 2023-10-14 at 19.34.53.mp4
    28.9 MB
  • WhatsApp Image 2023-10-14 at 19.45.06.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-14 at 19.45.06.jpeg
    57.2 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-10-14 at 19.45.06(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-14 at 19.45.06(1).jpeg
    57 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-10-14 at 19.45.06(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-14 at 19.45.06(2).jpeg
    55.6 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-10-14 at 19.45.07.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-14 at 19.45.07.jpeg
    52.9 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-10-14 at 19.45.07(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-14 at 19.45.07(1).jpeg
    55.6 KB · Views: 2
We jamaa kwani katibu wa mbunge gani?

Ama ni mwanahabari maalum wa wabunge wepi?
Naona umeamua kuwasimamia watu kwa kuleta taarifa zao tu. . Uchaguzi na homa zake.
 
Back
Top Bottom