Rais Samia: Mwalimu Nyerere aling'atuka ili kuruhusu Mageuzi ya Kiuchumi na hayati Mwinyi alipewa Kazi ya kuleta Mageuzi!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,980
Rais Samia amesema baada ya Rais Mwinyi kuingia madarakani Gazeti la Economist la UK liliandika " Rais Mwinyi hawezi kuleta nafuu yoyote kwenye Uchumi dhaifu sana wa Tanzania kwa sababu Mwinyi ni Mtu wa Nyerere"

Ambacho The Economist hawakukijua ni kwamba Nyerere aling'atuka ili kuruhusu Mageuzi ya Kiuchumi na hayati Mwinyi alipewa Kazi hiyo, amesema Rais Samia

Source:TBC
 
Mwalimu alikuwa ni kichwa Cha pekee sana ,Tanzania tunayoiona Sasa ni kazi ya akili yake tukatae tukubali huo ndio ukweli mchungu.
Kichwa kwenye Nini?

Nyerere ndiye aliyeharibu Uchumi wa Nchi hii Kwa maamuzi yake ya hovyo kwenye Ujamaa, Utaifishaji Mali, Kuminya Uhuru wa kujieleza, kuua Elimu, kuingiza nchi kwenye vita ya Kagera bila sababu na hata kuiingiza nchi kwenye gharama za Ukombozi Kusini mwa Afrika bila sababu za Msingi
 
Kumbe ndio maana Mwl. aliendelea kuwa M/kiti wa chama. Mzee wetu Mwinyi alipewa kazi ngumu sana lakini aliiweza. Kwenye hotuba moja ta Mwl. nakumbuka aliwahi kusema hawezi kuwa geuka kuwa jiwe sijui alikuwa anamaanisha nini.
 
Sasa mbona yeye Samia hataki kuleta Mageuzi ya kweli badala yake ni KUHADAA Umma wa Watanzania?
 
Rais Samia amesema baada ya Rais Mwinyi kuingia madarakani Gazeti la Economist la UK liliandika " Rais Mwinyi hawezi kuleta nafuu yoyote kwenye Uchumi dhaifu sana wa Tanzania kwa sababu Mwinyi ni Mtu wa Nyerere"

Ambacho The Economist hawakukijua ni kwamba Nyerere aling'atuka ili kuruhusu Mageuzi ya Kiuchumi na hayati Mwinyi alipewa Kazi hiyo, amesema Rais Samia
Source:TBC
Ni kweli. Hawa The Economist ni media ya kibeberu, siku zote wanatusema vibaya na walimwandama sana Magufuli, ila Samia walimfagilia. Samia tumaini jipya Tanzania: The Economist baada ya kumsakama sana Magufuli, sasa angalau lina matumaini na Samia, laanza naye vizuri na hapa TZ Trends & Analysis: Hoja 30 za The Economist Kumhusu President Samia. Kuna za Kweli, za Uongo na Uzushi na Kutaka Kumpangia Watakacho Mabeberu, Jee?

Hata mimi nimemfagilia Mwinyi Buriani Mzee Ruksa!. Ni Deng Xiaoping Wetu wa Mageuzi ya Kiuchumi, Demokrasia, Haki za Binaadam na Uhuru wa Habari. Asante kwa Ruksa Zako, Pumzika!.
P
 
Back
Top Bottom