Maskini rais wanguuu...

Status
Not open for further replies.

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
3,954
2,000
2cp4020.jpg
Kazi ipo... Ni kutoka gazeti la Majira la leo Oktoba 9, 2007
 

Dua

JF-Expert Member
Nov 14, 2006
3,233
2,000
Kweli JK amezoea kupokea vitu ambavyo ni mabomu tu, mawaziri wake ni mabomu hata mfano wa hundi ni bomu tu. Two hundred thousand = 300,000.00.

Mchana kweupe namna hii ni hatari.
 

Mwakilishi

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
484
195
Vipi tena, je ni $300,000 au $200,000? Which is which? Huu sasa sijui ni uzembe au ujinga au vyote kwa pamoja? Yaani hata ku-proofread mbinde? Labda waje Wa-Norway kutusaidia katika hilo pia...
 

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
1,250
Kuna habari kwamba hata wasaidizi wa JK wameshituka baada ya JF kuiweka humu na kuanza kuijadili.... KUMBE WANASOMA JF 24X7....

JK-WB.JPG

Bravo JF
 

omarilyas

JF-Expert Member
Jan 24, 2007
2,130
1,195
Damnnn

Nilikuwa sijagundua..hii kweli ni kubwa lao. Majira nao kwa ukuwadi wao wakadhani wanamsaidia RAIS wetu kumbe wanamuaibisha. I mean wanaiaibisha OFISI YA RAIS..

Kweli miti yote inateleza.
 

Icadon

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
3,583
0
Kiasi kilichotolewa ni.........? Ha ha kumbe hivi ndio wanavyotuibia sio
 

Katibu Tarafa

JF-Expert Member
Feb 16, 2007
975
1,225
sasa nimechoka kabisa,hata kalamavi hana makosa kama mtindo ndio huu,wacha wabunge wa ccm watetee ujinga sio makosa yao.yaani jk na watu wake wanakubali huu ujinga sijui ni wapi pa kukimbilia.mungu tusaidie
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
37,308
2,000
Ni writing error
Hakuna cha writting error wala nini,hii ni aibu tupu maana ianaonyesha jinsi wasaidizi wa muungwana walivyo 'hovyo' kuliko wasaidizi wa rais yeyote aliyetangulia.Mpaka kupiga picha ya makabidhiano ni mambo ambayo yalishaandaliwa sas inakuwaje???...
 

Masanja

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
4,533
2,000
HAKI YA NANI, THIS EXIHBITS THE HIGHEST LEVEL OF INCOMPETENCE! Jamani our President I all along thought ni mtu makini,,,yaani kweli hata yeye hakuisoma? achilia mbali hao wababaishaji wanaoitwa wasaidizi wake? No wonder Karamagi alisain the worst contract than Mangungo wa Msovero na Karl Peters!
 

Ole

JF-Expert Member
Dec 16, 2006
2,160
2,000
Kuna habari kwamba hata wasaidizi wa JK wameshituka baada ya JF kuiweka humu na kuanza kuijadili.... KUMBE WANASOMA JF 24X7....

JK-WB.JPGBravo JF

Hii ndio hali halisi ya mambo ndani ya Bongo land. Ati nini?
 

green29

JF-Expert Member
Jul 4, 2007
311
225
inawezekana kulikuwa na cheki mbili... Yaani Exim wametoa 500,000 kwa maana Scholarship fund iende 300,000 na hizo 200,000 ziwe ni za mazabe... sema muandaaji wa hiyo chakula alikuwa anatetemeka akaibua hadharani!!
 

Kibunango

JF-Expert Member
Aug 29, 2006
7,960
2,000
Maxence,

Ni aibu kwa JK kwa kuto ona hilo kosa, nahisi kabla ya kukabidhiwa hundi hiyo maelezo yaliyosemwa ni 300,000/- USD, hivyo hakuwa na shaka kwani hiyo 300,000/ ipo vilevile kwenye hiyo hundi. Aidha aibu kubwa itakuwa kwa hao CEO kwa kujichanganya kwenye kuandika... Haya mara nyingi huwa ni matokeo ya kufanya vitu kwa haraka haraka...

Kwa upande mwingine, hali ya sasa ya mambo ya serikali ya JK hayapo shwari, hivyo kuweka tafsiri nyingine kubwa ambayo inapendwa zaidi sasa katika masikio ya wengi..
 

Mwanamalundi

JF-Expert Member
Aug 30, 2007
3,124
2,000
Mimi naona aibu si kwa JK pekee, hata huyo mzungu anapaswa kuona aibu vilevile. Lugha iliyoandikwa hapo ni ya kiingereza.

Ni imani yangu kuwa huyo mzungu anaelewa kiingereza vizuri sana. Iweje na yeye pia ashiriki katika utumbo huo. Hii inazidi kuwaonyesha watanzania jinsi hawa wazungu wanavyoshirikiana na viongozi wetu kutuibia raslimali zetu.

Wanaopinga mikataba feki ya Buzwagi, Ushahidi huo hapo juu unatosha kuwafumbua macho.
 

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,709
2,000
Hii ni kali ya mwaka nazania ata hiyo mikataba ya madini hua ina andikwa hivi hivi,mimi niliona ile copy ya buzwagi kweli imeandikwa hivihivi imefutwafutwa sehemu nyingi tena nyingine ni figure kama inavyo onekana hapo.
 

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,812
2,000
Jamani msiniue kwa kicheko, yaani nimecheka leo na machozi yanatoka. Bahati niko peke yangu ofisini maana kuna mtu angeniona angefikiri nimechanganyikiwa.

Yaani mungu wangu matatizo ya kukimbilia kila opportunity ya kupigwa picha.

JK una kazi baba mwaka huu, hao watu wote unaoongozana nao, wanafanya nini?

JF babu kubwa!!!
 

G.MWAKASEGE

Senior Member
Jun 29, 2007
153
0
This Is Totally Lack Of Seriousness,ila Unaweza Kuta Iyo Imefanywa Technically Kama Mchanga Wa Macho Then Baadae Waseme Ni 200,000 Sio 300,000 Ili Kisaliacho Chaenda Kinywani.
Manake Kama Usanii Kwa Level Hii Umepitiliza.kama Vitu Obvious Tuu Hata Proof Reading Hakuna Je Mkataba Ambao Ni Detailed Itawezekana Kweli
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom