Maskini rais wanguuu...

Status
Not open for further replies.
Nakuunga mkono. au pia jamaa wasidizi wamepanic kwa jinsi mambo yalivyo kweupe hivi sasa kiasi hata kazi hawawezi thena kufanya.

Au ukiwa rais kila kitu unafanyiwa tu, hata kuona pia huwezi, hata mikataba wanasaini hivihivi wakiamini imeshaandaliwa na kumbe nao mianya ya makosa inapotokea. What a shame!

Nadhani kama ni makosa ni makosa ya wasaidizi wake ambao walipaswa kuhakiki hii dummy check na hata kama hawakugundua mwanzoni basi walipaswa kuligundua hilo wakati wa kukabidhiwa RAIS wetu na kwa kawaida walipaswa kuhakikisha wanacontrol reporting yake. Wanaweza kucontrol Ufisadi wa kina LOWASA tu lakini wanamwacha RAIS wetu aanikwe kiasi hiki?

Kama walishindwa kugundua hili hata wakati wa makabidhianao hivi kweli tuwaamini vipi kwa usalama wa RAIS wetu. Someone pale Magogoni anapaswa kuwajibishwa. Labdawakati wa kufika "mshikaji JAIRO" ambaye ameonyesha kuzidiwa na mzigo wa kazi yake kuonyeshwa kamlango cha kuondokea.

Someone has to pay for this. Siamini watu kama Jairo wana uzito kama wafadhili wa ndani kina Karamagi na RAIS PACHA Lowassa.

Tanzanianjema
 
Mimi nadhani ingawa tunaweza kuona ni jambo dogo lakini ni kubwa:
- Wasaidizi wake wote lazima wawajibishwe in public. This kind of error haiwezi kukukabilika kirahisi
- Mtu wa protocol naye lazima awajibishwe
- Hii iwe fundisho kwa kila kiongozi kwamba this Bongoland DIY, usitegemee wasaidizi

Lakini kwa nini tumwonee Mwungwana, yeye alishasema 'haelewi!' So if chanzo cha umaskini hakielewi basi ni dhahiri kwamba economics and maths are not his strong subjects!
So then why is he the President? That's a question we have to ask ourselves as wapiga kura.

But I think that this is a great photo that made everybody's day!
 
Bubu Msemaovyo uko sahihi kabisa.Hata hivyo hiyo picha yako hapo pembeni walao imenipunguzia hasira nilizonazo kwa watawala.

chakaza acha kuleta utani hapa tunajadili serious issues na mstakabali wa nchi yetu. Kama picha ya Bubu imepoza hasira inawezekana hata kura ulipiga kwa kuangaliapicha za wagombea.

Hapa suala ni kuwa hawa watendaji wetu hawako makini, hawako makini kwa maana kwamba aliyewachagua hakuwa makini katika uteuzi wake. kwa hiyo hii sirikali haiko makini. Kama haiko makini hata vitu wanavyofanya havitakuwa makini.

Hawa jamaa wameandaa hiyo cheque makusudi ku confirm kitu na kweli wamekipata. Kama vitu hivi vinafika hadi ikulu ndo maana tunaona hata watu wasiokuwa wazawa wanaenda ikulu kufanya kazi since there is no seriousness in veting.

Mpo wana JF
 
Presedent Jakaya Kikwete on Monday launched Public Service Scholarship Fund, a brainchild of private sector designed to induce significant improvement amongst servants in service delivery.

The project, dubbed Chief Executive Officers (CEO) Scholarship Fund was officially conceived by the CEO Roundtable as part of private sector initiative to transform mindsets of public servants in the increasingly competitive world economy.


`This is relevant intervention which we need to transform the functioning of public service in our country. It will assist our civil servants change old mindsets of controlling the private sector instead of facilitating or work with it,` President Kikwete said as he officially launched the project.


For the past several years, he said, the government had recorded strides in the public sector reforms, but the transformation of mindsets of public servants has been difficult to attain.


`I am hopeful this project, which targets key leaders in the public service for training and exposure, will help us speed up the desirable changes in the public service,` said Kikwete.


The President described the CEO Scholarship Fund as true demonstration of smart?partnership between the public and private sector.


For his part, leader of CEO, Ali Mufuruki said the three-year project worth US2.23m was initiated by his organisation in partnership with the Government and the World Bank.


The project had also received support from the UNCTAD/Empretec and Best-AC, the advocacy component of the BEST project.


According to Mufuruki, the primary project objective includes effecting change in the way the government does its businesses, particularly its relationship with the private sector both locally and foreign.


This follows a realisation that despite radical and affirmative government initiatives to attract both local and foreign investors, many deep seated problems of mistrust and lack of knowledge amongst public officials remain and will continue to haunt the relationship between public and private sectors.


`We are delighted that this project has been embraced by the Government with such enthusiasm, which is further proof that President Kikwete is serious about deepening the reforms of civil service and transforming mindsets of public servants to the leadership challenge of globalisation,` said Mufuruki.


CEO Roundtable is a policy dialogue forum that brings together CEOs and Executive Chairpersons of leading companies doing business in Tanzania.


Presently, 39 members of the roundtable account for a significant portion of the tax revenue collected by the Government and provide employment to more than 64,000 citizens.


SOURCE: Guardian
 
Hii ni aibu kwa PSU, ina maana hawafanyi pre screening ya vitu vyote anavyokabidhiwa rais? au ndio kuna kamgomo baridi kwenye kitengo chao?
 
Naomba rasmi kuelezea KINACHOFANYIKA. Check ni ya bank moja, lakini watoaji wakiwa wapo zaidi ya mmoja, BANGO (dummy cheque) inawekwa MOJA.

Wa kwanza anaandikiwa anakabidhi, kisha inafutwa na kuandikwa kwa ajili ya wa pili, hivyo hivyo mpaka wa MWISHO.

Kilichotokea ni kuwa baada ya Mufuruki kukabidhi, aliyeandika hakubadili MANENO. Alibadili TARAKIMU tu!!

Ndivyo ilivyofanyika, na ni picha mbili tofauti.

JF tuwe tunafikiria POSITIVELY

FD amejibu vizuri sana. Ile check ni kama "whiteboard" kwenye sehemu za namba na maandishi, inaandikwa na marker pens na kufutwa. Hii sio ile check inayopelekwa benki. Its a dummy check.

Tusipoteze muda na kitu ambacho kimeelezewa clearly. Inaelekea katika shamra shamra na haraka, walisahau kubadilisha maneno. Ni kosa ambalo ni dogo sana, tulalamike kama hela italiwa na sio kwenye dummy cheques.

Mimi binafsi mwanzo nilishtuka lakini nimeelewa...tusikuze vitu out of proportion. Admin nimeomba uondoe ile thread yangu kwani swali limejibiwa.
 
Ni kosa ambalo ni dogo sana, tulalamike kama hela italiwa na sio kwenye dummy cheques.

Mimi binafsi mwanzo nilishtuka lakini nimeelewa...tusikuze vitu out of proportion. Admin nimeomba uondoe ile thread yangu kwani swali limejibiwa.

Hili sio kosa dogo... viongozi wetu ni wachemfu na wamezidi kuchemka mno na lazima waambiwe!

Wewe ndio ulianza conspiracy theories hapa kuwa thisday wamegeuza mambo ili kumuaibisha kicheche rais Kikwete!
Umegundua kuwa utetezi wako wa wezi na wala rushwa ulikufunika hata ukashindwa kuona kitu ambacho ni obvious na ukakimbilia kulaumu media...

hiyo thread itakaa hapo ili uchemfu wako na kikwete wako uonekane for now teh teh teh teh teh teh
 
Hili sio kosa dogo... viongozi wetu ni wachemfu na wamezidi kuchemka mno na lazima waambiwe!

Wewe ndio ulianza conspiracy theories hapa kuwa thisday wamegeuza mambo ili kumuaibisha kicheche rais Kikwete!
Umegundua kuwa utetezi wako wa wezi na wala rushwa ulikufunika hata ukashindwa kuona kitu ambacho ni obvious na ukakimbilia kulaumu media...

hiyo thread itakaa hapo ili uchemfu wako na kikwete wako uonekane for now teh teh teh teh teh teh

Ziwekwe zote mbili mpaka end of time co-admin.
Lilikuwa swali na limejibiwa.
Uchemfu uko kwako...obviously.
 
duuuuu rais amekabidhiwa cheki ambayo ita bounce definately..dishonored cheque..ikifika benk wata comment..refer to the drawer amount in words and digits differs...
 
kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi..

Utakoma kukurupuka next time!

Hao wana jina lao lingine, nimelisahau kidogo lakini maelezo yake ni kwamba, huwa wanakuwa wameshafungwa kabla hata mpira haujaanza kuchezwa....kaaaazi kwelikweli.
 
Bubu Msemaovyo uko sahihi kabisa.Hata hivyo hiyo picha yako hapo pembeni walao imenipunguzia hasira nilizonazo kwa watawala.

Kama tusipokuwa makini kama walivyofanya hivi hasa hawa watendaji wake kuna siku wanaweza kuandika amount kubwa kwa tarakimu halafu kwa maneno wakaandika tusi kubwa wakamkabidhi Rais wetu. Tatizo hapa tulikuwa tunaangalia mjusi tukashindwa kumuona nyoka. We have always to read between lines.
 
"HUNDI ALIYOPEWA RAIS ILIKOSEWA"

Gazeti la majira la Jumamosi ya tarehe 13/10/07 Limetowa maelezo kuhusu Hundi aliyopewa Mheshimiwa Rais.Hundi hiyo ambayo ipo kwenye posts za mwanzo za Thread hii ilileta utata mkubwa,Hapa chini nimeambatanisha Taarifa kutoka kwenye gazeti la Majira;

Nukuu:

OKTOBA 8 mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete, alizindua Mfuko Maalumu kwa ajili ya Mafunzo kwa Maofisa Watendaji Wakuu wa Serikali.

Katika hafla hiyo, Rais alipokea michango ya hundi tatu tofauti ambapo Serikali ilitoa hundi ya dola 200,000 za Marekani, CEO Roundtable Tanzania dola 200,000 na Benki ya Dunia dola 300,000.

Hata hivyo hundi ya mfano iliyotolewa na Benki ya Dunia, iliandikwa kimakosa huku tarakimu zikitofautiana na maneno kwenye hundi hiyo, badala ya maneno kusomeka Three Hundred Thousand Only (Laki Tatu tu), iliandikwa Two Hundred Thousand Only (Laki Mbili tu).

Waandaaji wa hafla hiyo, kampuni ya Enigma Productions, wameomba radhi kwa makosa hayo ambayo Mkurugenzi wake, Bibi Pauline Rupia-Boateng, alisema jana kuwa hayakukusudiwa.

Kwa Hisani ya Majira.
 
Hata hivyo hundi ya mfano iliyotolewa na Benki ya Dunia, iliandikwa kimakosa huku tarakimu zikitofautiana na maneno kwenye hundi hiyo, badala ya maneno kusomeka Three Hundred Thousand Only (Laki Tatu tu), iliandikwa Two Hundred Thousand Only (Laki Mbili tu).

Waandaaji wa hafla hiyo, kampuni ya Enigma Productions, wameomba radhi kwa makosa hayo ambayo Mkurugenzi wake, Bibi Pauline Rupia-Boateng, alisema jana kuwa hayakukusudiwa.


Sasa wanalialia nini? Hawako competent, ndio kazi za kupeana kindugu ndugu na kishkaji matatizo yake ndiyo hayo.
 
Na Mwandishi Wetu

OKTOBA 8 mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete, alizindua Mfuko Maalumu kwa ajili ya Mafunzo kwa Maofisa Watendaji Wakuu wa Serikali.

Katika hafla hiyo, Rais alipokea michango ya hundi tatu tofauti ambapo Serikali ilitoa hundi ya dola 200,000 za Marekani, CEO Roundtable Tanzania dola 200,000 na Benki ya Dunia dola 300,000.

Hata hivyo hundi ya mfano iliyotolewa na Benki ya Dunia, iliandikwa kimakosa huku tarakimu zikitofautiana na maneno kwenye hundi hiyo, badala ya maneno kusomeka Three Hundred Thousand Only (Laki Tatu tu), iliandikwa Two Hundred Thousand Only (Laki Mbili tu).

Waandaaji wa hafla hiyo, kampuni ya Enigma Productions, wameomba radhi kwa makosa hayo ambayo Mkurugenzi wake, Bibi Pauline Rupia-Boateng, alisema jana kuwa hayakukusudiwa.
 
Hawa Tanzania Daima ni kama mambo mengi wanatoa JF

Kikwete ‘abambikiwa' hundi

na Happiness Katabazi

TUKIO la Rais Jakaya Kikwete kukabidhiwa mfano wa hundi yenye dosari kimaandishi, limeacha maswali mengi kutoka kwa wananchi wa kada mbalimbali.

Watu wengi wamekuwa wakipiga simu katika chumba cha habari cha gazeti hili, tangu Rais Kikwete alipokabidhiwa hundi hiyo na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania na Uganda, John McIntire, wakihoji umakini wake pamoja na wasaidizi wake.

Rais Kikwete alikabidhiwa mfano huo wa hundi Jumatatu, Oktoba 8 ikiwa imeandikwa kiasi cha fedha kwa maneno, dola za Marekani laki mbili, lakini kiasi cha fedha kwa tarakimu kikiwa kinasomeka kuwa ni dola 300,000.


Kiasi hicho cha fedha ni msaada kutoka Benki ya Dunia wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kuboresha uongozi Serikalini, hivi karibuni jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya watu waliozungumza na Tanzania Daima Jumapili, wamekuwa wakihoji iwapo tukio hilo lilitokea kwa bahati mbaya au kwa makusudi, ama kwa uzembe?


"Inakuwaje maofisa wa Benki ya Dunia wanamkabidhi Rais wa nchi hundi iliyokosewa kuandikwa, inawezekana kabisa watu hawa walilenga kumdhalilisha rais wetu ili ionekane anaweza kupokea chochote ili mradi kinahusu hela hata kama kina walakini? Au ndio wanataka ionekana kwamba rais wetu hajui kusoma?" alisema mwanasheria mwandamizi wa serikali ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini.


Alisema ingawa Watanzania wanauhitaji msaada huo wa Benki ya Dunia, lakini maofisa hao wanatakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu tukio hilo.


Kwamba kama ikibainika kuwa ni uzembe wao, basi watapaswa kumuomba radhi rais na wananchi anaowaongoza kwa kitendo cha kumkabidhi hadharani hundi yenye makosa ya wazi.


Mwanasheria mwingine alieleza kuwa, wasaidizi wa rais waliokuwa karibu naye siku ya tukio wanapaswa kubebeshwa lawama za kumuacha mkuu wa nchi kupokea kitu chenye makosa na akapigwa picha na waandishi wa habari huku akitabasamu.


Alisema wasaidizi wa rais wameonyesha uzembe mkubwa kwa sababu kazi yao ni kuhakikisha wanamsaidia rais katika kila jambo, ikiwa pamoja na kuhahakisha usahihi na usalama wa vitu anavyokabidhiwa.


Wengine walimwomba kuanzia sasa awe makini na watu wanaotaka kumdhalilisha kwa kumkabidhi nyaraka zilizokosewa.


"Kama wameweza kufanya hivyo hadharani, itakuwaje kwa nyaraka anazokabidhiwa faraghani?...tunampenda rais wetu kwa kuwa ni sisi wananchi ndio tumemweka madarakani, hivyo hatuwezi kukaa kimya huku tukiona anadhalilishwa hadharani.


"Nakuanzia sasa rais wetu na viongozi wengine wa serikali inabidi wawe makini hasa katika utiaji saini na upokeaji nyaraka," alisema Geogre Kahangwa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


Alisema tukio hilo ni kielelezo cha viongozi wetu kuwa hawako makini katika mambo mbalimbali, ni kielelezo cha uzembe na kutosoma kwa makini nyaraka nyeti.


Wengine walikwenda mbali zaidi na kudai kwamba, kama kitu kidogo kama hundi kinapokewa kikiwa na makosa, basi kuna walakini mkubwa katika suala la mikataba, ikidhaniwa huenda mingi inasainiwa bila kupitiwa kwa ufasaha, na hivyo kuliingiza taifa katika hatari ya mikataba inayogeuka kuwa shubiri kwa nchi.


Pamoja na kilio cha wananchi juu ya mikataba mibovu, serikali, licha ya kuahidi kuifumua na kuifanya iendane na wakati, inaonekana kufumbia macho suala hilo.


Mkataba wa mgodi wa Buzwagi unaodaiwa kusainiwa hotelini huko London, Uingereza, ni miongoni mwa mikataba mipya inayotajwa kuwa na walakini.


Maoni ya wasomaji hao yamekuja baada ya vyombo vya habari kuchapisha picha ya Rais Kikwete, ikionyesha akipokea hundi hiyo, jambo ambalo limezua mjadala wa chini kwa chini kutoka kwa wananchi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom