Masikini my ex, kweli malipo ni hapahapa duniani

Masikini my ex, kweli malipo ni hapahapa duniani

Kama umeona kuwa yeye anakuzimikia na kagari kako hako ka range rover mueleze ukweli kuhusu hilo gari kuwa si lako halafu mwambie kama kweli anakupenda kwa dhati au anakutamani tu kama wewe unavyomtamani kisha ukiona majibu yake yakoje ndipo upime mwenyewe hapo upate uhakikia upo mwaya okoa mchuma huo uko jahazinini?

ladyfuraha tatizo ni kwamba ntaanzaje kumwambia?
 
Nilimpenda sana huyu binti ila siku isiyo na jina alinimwaga tena kwa mbwembwe. Niliumia sana! almanusura nichanganyikiwe!

Sasa jana mchana nikasema nikimbie Mlimani City kwenda kununua kitu fulani, nikamuazima mwanangu gari lake (Range rover evoque) nikamuachia la kwangu (Hyundai Coupe Sports car).

Sasa wakati napark pale Mlimani nikasikia naitwa, kugeuka nakutana uso kwa uso na huyo bibie!

At first alikua kama ametahayari alivoona nashuka kwenye ile ndinga! Nikasalimiana nae vizuri tu, tukaongozana kuingia Mlimani ndani!

Akaanza kuning'ang'ania, ooh Amicus I missed you, leo sikuachi nakwambia, nikazunguka nae mule ndani, nikawa najiuliza mbona yeye hanunui, alifwata nini M/city? halafu alikua 'restless'. Nikajua kapanic akidhani ule mkoko ni wangu, alizoea kuniona na Hyundai yangu.

Mara ooh naomba tuongozane! wakati hajui naelekea wapi!

Sikuwa mkaidi, nikatoka nae, tukazama kwenye ndinga nikampeleka lunch! akawa analisifia sana gari! wakati tunasubiri msosi akaanza kunisimulia yaliyomsibu huku anabubujikwa na machozi! hadi watu wakawa wanatushangaa! na yeye ameachika almost the same way kama alivyoniacha!

Ananisihi turudiane, sasa naogopa asije akawa ameweweseka na ile range, tukarudiana akaja kuleta wenge tena akijua kwamba ule usafiri si wangu! Uongo haufai, kiukweli me bado nampenda.

Ni kama alikua anatamani kuniuliza kuhusu lile gari ila akawa anashindwa!

Jamani hebu nishaurini mwenzenu, nahisi bado nampenda coz tangu tuachane imepita miezi 6 tu ingawa nilikua nimeshaanza kumsahau. Halafu amezidi kuwa mzuri, amekatika vibaya sana!

Ananisumbua sana kwenye simu wajameni!

Yeye yupo Chuo pale Muhimbili anasomea Udaktari.

Nina uhakika hayumo humu JF coz nilimuuliza jana akasema yeye sio big fan wa mitandao ya kijamii kwasababu mara nyingi anapiga msuli, kwa kifupi shule yake ni ngumu sana.

Jamani nishaurini, kwa wale mtakao-comment naomba muwe serious...nataka kesho asubuhi nimpe jibu.

Haina mc cll
 
Stori nyingine bwana.......umeazima gari la mwanao....hadi mwanao ana gari tena R/Rover Vague maana yake ww ni mtu mzima sana .......umeachana na huyo girl wako miezi6 iliyopita na bado unampenda pamoja na kwamba alikumwaga. Hivi mtu umri wa kwako ni wa kubabaika na mapenzi ya akina girl?????? Yeye yupo chuo mlimani anasomea udaktari..... Udaktari wa binadamu au PhD???????? Kwa vyovyote alivyo, wewe na yeye wote mawenge. Stori yako haiingii masikioni mwa mtu mwenye akiri. Kawatafute mbulula wenzio na uludi ukajipange upya.

hapa unamuonea hajasema huyo msichana wake anasoma mlimani.
bali muhimbili uwe unasoma post kwa utulivu
 
Kwa hiyo ulionewa kwenye icho kibuti sio? Naona umefarijika naye kupigwa cha mbavu. Ila kuachwa sijui kama ntaweza tena na uzee huu kuvumilia... labda apotee kisailensa au tuachane. Ila vinginevyo... its done its done.. onwards onwards... no turning back..

Nimefarijika sana mkuu

Aliniumiza mno huyu binti

Unajua ukiachana na mpenzi wako unawish ukija kuonana nae umkute amechoka

Ukimkuta yuko vzr roho inauma
 
Stori nyingine bwana.......umeazima gari la mwanao....hadi mwanao ana gari tena R/Rover Vague maana yake ww ni mtu mzima sana .......umeachana na huyo girl wako miezi6 iliyopita na bado unampenda pamoja na kwamba alikumwaga. Hivi mtu umri wa kwako ni wa kubabaika na mapenzi ya akina girl?????? Yeye yupo chuo mlimani anasomea udaktari..... Udaktari wa binadamu au PhD???????? Kwa vyovyote alivyo, wewe na yeye wote mawenge. Stori yako haiingii masikioni mwa mtu mwenye akiri. Kawatafute mbulula wenzio na uludi ukajipange upya.

R/Rover Vague ndio kitu gani mkuu?

Au ulikua unamaanisha Vogue?
 
Ok, mrudie na akikupiga tena kibuti baada ya kugunddua (Range rover evoque) si yako kumbe una ile ile Hyundai Coupe Sports car, usisite kuja kutujulisha!

Hahahahah...........Kwa ushauri huu kweli wewe no Bigbro. LIKE.... LIKE......
 
Mkuu huyo mpige chini km alikubwanga achananaye.unaweza ukamrundia akajakukuumiza. Zaidi ya hapo inamaana kipindi uko naye mshikaji naye alikua anamenga mzingo punda nyama huyo atakuzingua zaidi ya hapo

Hata mimi nadhani anaweza akaja kunizingua tena mkuu

I am worried
 
Huyu ndo yule aliyekuwa anasita kumpokea yule mtoto ama? Anyway ,nini ilikuwa sababu ya yeye kukuacha?na leo? Anyway sikiliza moyo wako mapenzi hayanaga ushauri !!!!

U are correct my dear!

Sababu ipo basi?! kuna siku tu alinipigia simu then badala ya kuzungumza yeye akazungumza mwanaume akidai kwamba huyo binti ni mtu wake!

Nikamtafuta binti akakiri kwamba ni kweli anatoka na mtu mwingine!!! niliumia sana
 
Stori nyingine bwana.......umeazima gari la mwanao....hadi mwanao ana gari tena R/Rover Vague maana yake ww ni mtu mzima sana .......umeachana na huyo girl wako miezi6 iliyopita na bado unampenda pamoja na kwamba alikumwaga. Hivi mtu umri wa kwako ni wa kubabaika na mapenzi ya akina girl?????? Yeye yupo chuo mlimani anasomea udaktari..... Udaktari wa binadamu au PhD???????? Kwa vyovyote alivyo, wewe na yeye wote mawenge. Stori yako haiingii masikioni mwa mtu mwenye akiri. Kawatafute mbulula wenzio na uludi ukajipange upya.

mkuu unajua hata mimi nilisoma mara mbili ndio nikamuelewa huyu jamaa....vijana wa siku hizi wakisema 'MWANANGU' wanamaanisha 'BEST FRIEND' sio mtoto wa kuzaa.
 
hahahahhahahaha, inatia huruma sana hasa pale mabinti tunavyoshindwa kujizuia na kushoboka na wanaume wenye maisha mazur. Huwa inanisikitisha kweli. Yaani unashoboka hadi mwenyewe anajua. Tujifunze kujikaza mwenzangu na kujifanya kama umeyazoea hivi na kuona vya kawaida.
Liko wazi mkuu, huyo kapenda range na siyo anataka kurudi kwako kwa mapenzi.

Hata mimi nadhani ni gari limemzuzua
 
Mkuu Amicus Curiae siku hizi unaishi Dar? Nakumbuka uzi wako wa kuachiwa mtoto ubungo maelezo yake yamegongana na ya uzi huu! Au uzi upi kati ya huu na ule wa kuachiwa mtoto ubungo ni wa magumashi?

Mkuu nipo mjini naongeza kisomo
 
Last edited by a moderator:
Tumia akili mkuu ,usitumie hisia, jiulize kilichomkimbiza kwako wakati ule ni kipi na sasa kipi kinachomrudisha? Hakujali kukuumiza, alijali hisia zake. Sasa wewe endelea kumng'ang'ania sisi tunasubiri episode 3, tupo hapa tutakushauri.

Mkuu kama situmii akili natumia nini?

Lugha ya namna hii haifai.
 
Back
Top Bottom