Masikini kaka huyu

Masikini kaka huyu

ki ukwel kwa hizo vurugu za huyo mke anaonekana dhahir kua anataka na mumewe kuupata ili wawe sawa kwahyo hata kwa kutumia condom anaeza pia kumnga'ata au vyvyte ili apate contact ya damu
ishaur wangu aendlee kukaa seblen na aende kwa wazaz wa pande zote mbili au kama mke ana ndugu mkubwa tofaut na wazaz amuelezze hiyo case jins ilivyo.
kingne asimuache mkewe kwa faida ya mtoto alie tumbon kwa maana anaweza akazaliwa bila maamumbikizo na pia ili mama asije akamdhuru mtoto
ila kwa situation yake hil swala ni gumu sana atumie busara zaid kuliko hasira.

Yes, ila anahitaji nguvu za mungu, ukifikiria kibinadamu ngumu sana, nimejaribu kuvaa viatu vyake dah!! Only God can save his life
 
Miss chagga hiyo situation ishawahi kunikuta, cha muhimu mwambie kakako arudi kanisani walikofunga ndoa, ila kiufupi hiyo ndoa itavunjwa kanisani maana ndoa ni tendo la kukutana kimwili, bila tendo hakuna ndoa
 
Miss chagga hiyo situation ishawahi kunikuta, cha muhimu mwambie kakako arudi kanisani walikofunga ndoa, ila kiufupi hiyo ndoa itavunjwa kanisani maana ndoa ni tendo la kukutana kimwili, bila tendo hakuna ndoa
asante mkuu
 
Hivi kuna ushirika gani kati ya nuru na giza ni kama kuchanganya chuma na udongo kamwe havishikamani hilo nalo dhambi inamuotea mlango itakuwa kila atakapofungua mlango ataikuta sasa ni swala kufa au kupona au uzima au mauti chagua mwenyewe.
 
yeye anasema anataka haki yake ya ndoa swala la VVU anasema ataponywa na Mungu hata dawa hanywi .. ujue hapa hata mtoto tumboni anamtesa kile kiumbe na kinaweza kufa hanywi dawa kula hataki vizuri ngono ndiyo anataka

Unanifuraisha, eti hataki kula dawa wala chakula anataka ngono, huyo anateswa na psychology tu
 
Mi nadhani afuate ushauri alopewa na wataalamu huko walikoenda kupima coz anaeza kumwacha still yule mwanamke akaishi miaka mingi zaidi yake maybe kaka akapata ajali kesho keshokutwa au hata mwakani akafa na akamwacha mdada.lkn km huyo dada ataendelea kun'gania ku doo bila ndomu basi hakuna jinsi huyo ni muuaji
 
Ana uhakika gani kwamba akitoka hapo ndio atasalimika milele??

Anaweza kuruka mkojo na kukanyaga mavi pia....there are so many possible scenarios za yeye kuambukizwa virusi as long as he lives....ila atleast akiamua kutulia naye na kufuata masharti anaweza kuepuka maambukizi kwa kiasi kikubwa while maintaining his manly honour....

Hivi akiamua kumuacha...akaukwaa pengine, atarudi kuomba msamaha au? Au akikuta kote alikopima ni false negatives virusi havikuwa active bado?

Ingekuwa ni mimi: ntachunguza kama mwanamke alijua hali yake kabla ya ndoa na alifanya makusudi kunificha ili nimuamini, au kama alikiwa anachepuka baada ya ndoa. Kama ni hivyo huyo hastahili kuwa nami.

Kama she is innocent...hakuwahi kuchepuka na hakuwa anaijua hali yake...maana yake she also took the risk being with me na aliniamini....if and only if that is true, I will keep her till death do us part.

mmmmhhh we jamaa una moyo!!!
 
Unanifuraisha, eti hataki kula dawa wala chakula anataka ngono, huyo anateswa na psychology tu
hata mimi naona hivyo na anahisi jamaa asipo ukwaa possibility ya kuachwa ni kubwa mno.. so nahisi anawashauri wabaya
 
hao wanandoa waendelee tu kuishi pamoja, wawe wanatumia kinga.
Lakini wakitaka kupata mtoto tena waende hospitali kwanza wakapewe mbinu. Kuna njia za kupata mtoto bila kuambukizana wala kumuambukiza mtoto.
ninachosema ni ukweli wala sijatunga.
 
kingine unajua mambo ya wanawake kuendeshwa na hisia .. ataanza kuhisi jamaa anachepuka akichelewa ugomvi, akikosolewa ugomvi kuishi naye yataka moyo hasa kama mume na mke... mi sielewi kwa nini atake ngono kwa nguvu
huyoo rafiki ni ndugu yakoooo auu naniliuu!!!!!!!!!! maana naona imekugusa mnoo!!!
 
Ndoa za kikristo unajua tena wif hataki kusikia wala kuelewa

Kwani ndoa ninyororo unaokufunga akili za kuamua? Ndoa ya zote ni lazima wahusika wawe HIV negative(s),sasa kama walifunga ndoa maana yake walipimwa na kukutwa wako salama, kama ni hivyo huwa mwanamke ilikuwaje awe HIV positive kama sio zinaa? Je ukristo unasemaje kuhusu zinaa?
 
Si ndo maana mimi nimegoma kutafuta mchumba ndan ya makanisa ya kilokole,maana wanawake wengi walioko kule ni wale waliostaafu ukahaba,waliostaafu kuua kwa kutoa mimba...awashirikishe washenga na wazee
 
yeye anasema anataka haki yake ya ndoa swala la VVU anasema ataponywa na Mungu hata dawa hanywi .. ujue hapa hata mtoto tumboni anamtesa kile kiumbe na kinaweza kufa hanywi dawa kula hataki vizuri ngono ndiyo anataka
hahahaaa anawashwa sana haponi mpaka akunwekunwe hahaaaa.. hakuna kula wala kunywa mpaka kieleweke hapo.
 
Duuhh kazi kweli kweli, wakati mwingine mimi Huwa naamini hakuna ulevi mbaya kama DINI (mnisamehe kwa hili). Maana humwondolea mtu uwezo wa kufikiri kwa mantiki. Kwa hali ilivyo bora waachane (japo wengine huamini alichokiunganisha Mungu.....)
 
Habari zenu wana Jf,

Ni moja ya rafiki zangu ni kijana mkimya, mpole, mcha Mungu, ana heshima na mpiganaji katika kutafuta maendeleo, katika pilika pilika zake Mungu akampa binti mzuri, mpole, msikivu na mwenye adabu hapa ndipo mwanzo wa misha yao mpaka ndoa. Kwa sasa wana mwaka mmoja ndani ya ndoa yao na Mungu kawamjalia mwanamke kwa sasa anaujauzito wa miezi miwili katika ile hali ya kuugua ugua akaenda hospital.

Kinachosikitisha na kuhuzunisha ni kijana mwezi huu kagundua mkewe ni muathirika (VVU). Huyu rafiki yangu huwa na mwita kaka ili kukata mzizi wa fitina si unajua mabinti tulivyo. Baada ya kugundua hivyo nikaanza kumuuliza je hawakupima wakati wa maandalizi ya ndoa.? Majibu aliyotoa kiukweli ni huzuni eti hawakuona haja ya kupima kisa wote aliona wametulia na hakukuwa na hisia yeyeote ya uchepukaji na pia walikutana Kanisani.

Nilivyo fyoko fyoko nikauliza vipi mlianza kuzini kabla ya ndoa na mlikuwa mnatumia Condom? akaijbu ndiyo ili kuzuia mimba kwa hiyo walivyofunga ndoa tu wakaanza kunjunjana bila Condom bila hata kujua afya ya kila mmoja.


Mungu si nanjilinji bwana wee kijana hajaathirika kapima zaidi ya mara 7 kila akipima anaona negative kawa kama chizi akipita mjini akiona hospital anashuka anapima aamini majibu anayopata.Lakini kutokana na vipimo inaonekana ajaathirika, kaenda hospital na mkewe doctor wamempa namna ya kuishi na mtu wa VVU lakini ameshindwa kinachotokea kijana analala sebuleni mwanamke chumbani.

Kinachotokea mke kawa na gubu anamlazimisha mwanaume mapenzi (ngono) mwanume hawezi, jamani mimi nimeshindwa mshauri zaidi nilimwambia alale sebuleni au Mzungu wa nne mwanamke amegeuka moto anataka ngono bila hata condom. Jamani naombeni anayeweza toa njia nyingine ya kumsaidia kijana ili waishi at least kwa amani mwenye suluhu

Karibuni, ushauri

akatafte mchepuko tu hakuna jinsi hapo
 
Back
Top Bottom