He! ati kutumia kinga ni dhambi?? mbona walikuwa wanatumia kabla hawajaoana?? Ilikuwa si dhambi walipokuwa wanazuia nazo mimba ila sasa kuzuia VVU ishakuwa dhambi? Haki ya nani kuna mitihani mingine unaweza kufikiri uko ndotoni! Huyo mke hata kumshambulia naogopa maana sipati picha ndo ingekuwa mimi. Huku una VVU, huku una mshtuko, una huzuni, mtu unayemtegemea akufariji anakukimbia... kwa ufupi bidada yuko kwenye "denial" ndo maana hata anadai mngonoko kama kawa tena bila kinga. Na mantiki yake ni kuwa kama wameshangonoka mwaka mzima bila condom leo maambukizi yatatoka wapi? Kijana nae ana mshtuko. Mi ningemshauri asilale sebuleni. Alale kitanda kimoja na mkewe, tena amkumbatie kabisa maana tatizo la mke ni kubwa kuliko la mume. Huyu dada pamoja na VVU pia ni mjamzito. Hatakiwi kuachwa kulia lia hovyo na kukosa matumaini. Kama wanamjua Mungu basi wanajua hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea. Kaka aache kuhukumu maana hakuna ajuaye mke amepataje VVU. Kokote alikopata, sasa wapo wote ndani, ni mkewe, ndo mama mtoto hivyo. Watulie sana, mi naamini watapata suluhisho pengine hata la kuendelea kuishi pamoja na kungonoka na kuendelea kuzaa. Wakipata suluhisho la kutengana basi nalo liwe la heri limuache kila mmoja akiwa na mzigo mwepesi. Mwambie akae kimya kwa sasa, watafakari wenyewe maana hawawezi kuendelea kuchachawa kama maharage yanayochemka. Ifike mahali watulie waongee na habari ya "Uliutoa wapi" isiwepo labda mwanamke mwenyewe aamue kufunguka kama anajua. Namaanisha maongezi yasiwe ya lawama bali ya kutafuta suluhisho. Huyo Mungu wao wakimrudia na kutubu ni mwaminifu, atawapa nguvu ya kuvumilia na atawapa hekima ya kulimaliza hili jambo. Amen.