MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 20,897
- 63,784
Kiukweli hata mimi sipendi kabisa kuona Tanganyika inaendelea kuungana na Zanzibar. Binafsi huwa sioni faida zozote za huu muungano na wala sijawahi kuwaona wazanzibari kama raia wenzangu, nawaonaga sana tu na Wakenya, Wanyarwanda au Waganda. Pande zote mbili za muungano zina malalamiko, zinabaguana na hazipendani hivyo nadhani ni wakati muafaka kabisa wa kuvunja huu muungano na kukubali kwamba jaribio la kwanza la Nyerere limefeli kabisa."Mgeni sio kwamba ananunua ardhi, na sio kwamba anapewa umiliki wa 100% hapana anapewa kibali cha kuwekeza kwa miaka kadhaa. Kwa mtu anayetoka Tanzania Bara ambaye anataka kufanya Uwekezaji Zanzibar anatumia utaratibu huo huo" Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Ally Mwinyi.
View attachment 2028001