Masharti ya kuwekeza Zanzibar kwa Mtanzania bara na mgeni

aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
662
1,000
"Mgeni sio kwamba ananunua ardhi, na sio kwamba anapewa umiliki wa 100% hapana anapewa kibali cha kuwekeza kwa miaka kadhaa. Kwa mtu anayetoka Tanzania Bara ambaye anataka kufanya Uwekezaji Zanzibar anatumia utaratibu huo huo" Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Ally Mwinyi.

E33C314B-D18B-4DEF-AE7A-3AA9520263FB.jpeg


====

Rais Mwinyi, ametoa ufafanuzi kuhusu suala la uwekezaji kwa wa wageni wote wanaotoka nje ya visiwa hivyo ikiwemo Tanzania Bara kuwa hawataweza kupata umiliki asilimia 100 ya umuliki wa ardhi isipokuwa watakodishiwa maeneo hayo.

Amesema kuwa utaratibu huo upo kwa kufuata masharti yaliyowekwa ya umiliki wa ardhi ambao unataka wazawa kuwa wamiliki pekee wa ardhi.

"Mgeni (anayetoka nje ya nchi) sio kwamba ananunua ardhi, na sio kwamba anapewa umiliki wa 100% hapana anapewa kibali cha kuwekeza kwahiyo anakuwa na hati inayoonyesha kwamba amekodishwa ardhi kwa miaka kadhaa ili awekeze na masharti yanawekwa"

"Kwa mtu anayetoka Tanzania Bara ambaye anataka kufanya Uwekezaji Zanzibar anatumia utaratibu huo huo"

"Kwa upande wa umiliki wa ardhi unabaki kwa Wazanzibar pekee yao kwamba Mzanzibar aliyezaliwa hapa Zanzibar ndiye ana haki ya kumiliki ardhi kwa mujibu wa sheria zetu" Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Ally Mwinyi.
 

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
10,122
2,000
kati ya jambo nitakalounga mkono hata kwa kuandamana ni kwa serikali kuuvunja muungano na kila mtu abaki kwao na nchi yake...

Kuna haja ya kuuvunja huu muungano wale jamaa waendelee na maisha yao na sisi tuendelee na maisha yetu....

Serikali na Watanzania tuache kucheka na wahindi, waarabu na hawa wazanzibar ni moja ya watu tunaowadekeza sana na kuishia kuinyonya hii nchi kwa kivuli cha uzawa ilhali undercover sio wazawa bali they are here to benefit....
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,662
2,000
Huu muungano ni wa ajabuajabu sana.
Mzanzibar anaenjoy fursa zote zinazopatikana katika hii nchi yaani bara na huko Zanzibar tena kwa mambo yote ya muungano na yasiyo ya muungano Ila Mtanganyika fursa zake mwisho chumbe.

Sasa muungano wa hivi una faida gani kwa Mtanganyika?

Tuuvunje tu kila mmoja ajielewe anasimamia wapi!
 

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
10,122
2,000
Hili la Rais Mwinyi ni la kuanza kupigiwa kelele na kila Mtanzania mbara anayejielewa, kifupi tuanze harakati mpya za kuuvunja muungano na kila mtu abaki kwao....Mzanzibar awe na passport yake na mbara awe na paasport, Zanzibar kuingia na kutoka ni Viza kama kawaida....Biashara kufanya waruhusiwe kwa utaratibu kama wa wageni wengine ikiwa pamoja na kuwawekea masharti magumu ya wao kuja kufungua biashara huku....

We favoured them, but they are fucked us hardly.....we should wake up and start to screw them....
 

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
10,122
2,000
Tuache kuwadekeza sasa hawa....wanatupanda vichwani....CCM kama hili linawafavor kwenye siasa zenu sasa hili dubwana ndio litakuwa kaburi lenu..... tutaanzisha anti - Zenji operation huku bara sasa nao wapate pinch....

In reality hawa watu kwanza ni wabaguzi kwenye biashara, they are selfish kweny biashara kuanzia hapa na huko kwao....mbara ni ngumu hawa kufanya nao biashara kwao Zenji, wakija hapa wanatiatia huruma tunawabeba...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom