Mimi nauliza mnisaidie ,Mfano ikatokea Muungano umevunjika kwa hiyo hawa wazenji walioko huku bara watarudishwa kwao ? Vipi kuhusu kuzaliana maana tulishachanganyikana hatari ! Je watu ambao walishawekeza miradi yao mikubwa inakuaje hapo ?
 
Sasa kama hakuna muungano katika ardhi ,basi wazanzibar huku bara tuwahesabu ni wageni,tuanze na bakhresa
 
Vipi hili jeshi lenu mlilolileta lililojaa kila kipembe Na usalama mliowamwaga kila street mtawaondosha lini ??
Dawa ni kushirikiana kuvunja muungano huu muungano wa ki-ngese kabisa wabara na wazanzibari tupinge muungano uchwara
 
"Mgeni sio kwamba ananunua ardhi, na sio kwamba anapewa umiliki wa 100% hapana anapewa kibali cha kuwekeza kwa miaka kadhaa. Kwa mtu anayetoka Tanzania Bara ambaye anataka kufanya Uwekezaji Zanzibar anatumia utaratibu huo huo" Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Ally Mwinyi.

View attachment 2028001
We are reading to much into this!!
Zenj ni ndogo kuliko mkoa wa Kagera,Katavi,au kigoma,idadi ya watu wake ni Sawa na idadi ya watu wa Dar,
Unakuta mtu hana viwanja hata kwenye mikoa mitatu ya Bara!!lakini akikosa kiwanja Zenj,inakuwa nongwa!!
Kungekuwa na Cha upekee sana Zenj,ningeelewa,ardhi ya huku iliyopo ufukweni inauzwa mpaka bilioni moja,
Wangapi wanaweza hii,hata hivyo wabara kibao wapo Zenj,wamejenga na wanamiriki ardhi.
Wewe huna hata viwanja kumi kwenye mikoa mitwno ya Bara,lakini unaona vibaya ukikosa kiwanja Zenj!!??
 
zanzibar ni mke wa tanganyika anahaki ya kutumia mali ya mume wake ila kama inavyofahamika mali ya mke ni ya kwake ila ya mume ni ya familia
 
Hakika huu muungano wetu ni fake!
Muungano gani ambao watu wa upande mmoja hawana haki upande mwingine???
Tena kama ni huyu Mwinyi walimpa hadi jimbo la Rufiji ambalo ni la Tz bara, najiuliza kama mtu wa bara kweli anaweza kwenda kugombea jimbo Zanzbar? Huko tuendako kuna rais atakuja kuwanyang'anya ardhi Wazanzbar wote waliojenga huku bara!
 
Hata ukivunjika muungano Wapemba wako mpaka Handeni, na Mtae wamejenga majumbani na wanamiliki ardhi kubwa tu .
Hao watabaki kuwa wabara baada ya muungano kuvunjika siyo tatizo na kama watachagua kuwa wazenji basi watapaswa kuuza ardhi wanayo miliki bara
 
Na anayetoka nje ya Muungano vipi? I think hakuna tofauti.
Kisha nikuulize tumeushania nini hapo
 
Kwisha habari yenu Ardhi ya ZANZIBAR NI ndogo Sana isipolindwa Kesho na keshokutwa tutakua na uhaba mkubwa WA Ardhi Kwa vizazi vyetu Watanganyika ttzo lenu si Ardhi mnamamia Kwa maelfu ya maekar tatizo lengu ni umaskin WA akili ndio maana mnahama huko kuja kututilia nzi huku
Kulindwa siyo tatizo tatizo ni double standard ilitakiwa na mzanzibari awekewe kiji sheria kidogo kwa bara angalau kuendana na hiyo ya zanzibar .....ilitakiwa mzanzibari asiruhusike kumiliki ardhi ya bara zaidi ya heka moja
 
Asiyemlaumu Nyerere katika hili hana upeo wa historia. Kwa maneno yake mwenyewe, Nyerere alikataa ombi la Karume la kutaka iwe nchi moja na yeye awe rais- eti kwa sababu aliogopa asiambiwe ameimeza Zanzibar! Sikumwelewa kwa kweli. Nadhani zaidi aliogopa Uislamu wa Zanzibar.
Hapo ndipo pekee alipo kosea Nyerere serikali moja ndiyoilikuwa dawa ya muungano
 
Huu Muungano una changamoto nyingi. Wenye mamlaka ya kuwezesha kufanyika mabadiliko wapo kimya. Siku Watanganyika wakija kuamua kuidai Tanganyika yao kwa ngvu, tusije kuja kuanza kumlamu shetani bure. Tunaloweza kulirekebisha leo turekebishe kabla hatujachelewa
Tanzania hatuna viongozi waliopo wapo kusaka tonge tu kusomba pesa za nchi kwa maslai yao na familia zao tu
 
Tafuta asili ya Mwinyi mzee upate majibu ni mtu wa wapi upande wa baba yake..
Ile katika ambayo hata yeye aliikuta kule hakuyaanzisha yeye yale
Kifupi wazanzibar wote ni wabara isipokuwa walichanganya damu na waarabu na wahindi ambao siyo wabara hivyo mwinyi ni mzenji ukitumia hicho kigezo chako utakuta hakuna mzanzibar maana hata karume ni m bara tu
 
Kifupi wazanzibar wote ni wabara isipokuwa walichanganya damu na waarabu na wahindi ambao siyo wabara hivyo mwinyi ni mzenji ukitumia hicho kigezo chako utakuta hakuna mzanzibar maana hata karume ni m bara tu
Ni sahihi na ukweli usiopingika..
Kwa maana kisiwa chochote asili yake ni (migrants) wahamiaji
 
Mhuu, wenye Tanganyika yao wamefufuka haya sii mapya ila kibiriti kimewashwa. Tuwe macho na busara pia tusibomoe kila kitu kwa kauli ambayo sio mpya kwani ipo kwenye katiba ya Zanzibar siku zote.
 
Mhuu, wenye Tanganyika yao wamefufuka haya sii mapya ila kibiriti kimewashwa. Tuwe macho na busara pia tusibomoe kila kitu kwa kauli ambayo sio mpya kwani ipo kwenye katiba ya Zanzibar siku zote.
Hahaaaaaa
 

Similar Discussions

12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom