Namwona JPM ndani ya Makonda na Makonda ndani ya JPM

Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
2,626
3,141
Nimefuatilia sana ziara za Makonda. Nilichogundua ni kwamba, ukiachilia mbali siasa lakini kwa zaidi ya 75% Makonda anafanana sana na JPM.

Anafanana katika kusikiliza kero za Watanzania na kuzitafutia ufumbuzi wa papo kwa papo. Lakini pia anakemea uzembe unaofanywa na watumishi wa umma.

Kwa tathmini yangu, Makonda angekuwa na mamlaka kamili ya juu, hali ingekuwa kama ilivyokuwa wakati wa JPM.

Umeme usingekuwa shida kama ilivyo sasa, uzembe makazini usingekuwepo kama ilivyo sasa, dhuluma, ufisadi, wizi, rushwa, ubabaishaji nk. vingepungua sana kama ilivyokuwa wakati wa JPM.

Mungu atusaidie kumpata JPM mwingine ili kuliokoa Taifa hili, kwani mpaka sasa hali inatisha huku mtaani.
 
Back
Top Bottom