Marekani yashindwa kutungua balloon la China

Marekani yashindwa kutungua balloon la China

Mchina mweusi acha uongo Marekani hawajataka kulitungua kwakua litaumiza watu na mali na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani alikua aende China lakini baada ya kuona baloon hilo amehairisha na wamewasiliana na China wamesema hilo halipo kwenye uchunguzi wa kichina
Cha kushukuru wamejibiwa kwamba mmeingia taiwan sasa sisi tumekuja kwenu.Dunia miaka hii ina raha sana.
 
Zile panel zina ukubwa wa school bus 3 hawawezi risk kuumiza watu. Na pia hawajui nini kimo ndani.
Hapo wanasubiri litoke nje ya maeneo yenye watu walishushe
 
Mkuu Hilo balloon ni humiliation kwa USA, eanaogopa tu kukiri
US ni wepesi sana kukiri kuliko hiyo China. US mwenyewe anayo mabaluni ya kufika 90,000ft achana na hilo la 60,000ft
IMG_20230204_220632.jpg
Hii sioni kama humiliation, satellites zikipita angani utasema ni humiliation? Hakuna international treaty kusema kuanzia altitude fulani ni international airspace.

Marekani ilikuwa inarusha U-2 spy jets angani zinapita USSR na hakuna mgogoro unatokea mpaka pale USSR walipotengeza missile ya kufikia umbali ule Marekani ikashangaa ndege yake inaangushwa. Na hapo ikatengeneza SR-71 Blackbird ikawa inakimbia kuzidi intercepting missiles za Soviet kwenye anga lao.

Ingekuwa ni ndege iko kwenye 40,000ft hapo ingeleta shida ila low orbiting satellites kama za Starlink, high flying balloons zinapita tu mnapigiana kelele. Kukaa sana angani ndio inakuwa shida
 
Licha ya kujinadi kwamba Marekani ndiyo nchi inayoongoza kwa silaha za kila namba, Marekani wameonyesha week was Yao dhidi ya balloon la wachina ambalo linaendelea kuvinjari na kukatiza maeneo mbalimbali yakuwemo maeneo nyeti kama kambi za jeshi. Licha ya kutuma makombora mazito kutungua balloon hizo jitihada zinaonekana kubonga mwamba.
Balloon Hilo linasemekama kutembea umbali wa futi 120,000 kutoka usawa wa bahari.
View attachment 2506365
View attachment 2506381
Week au weak fala sana wewe hata hujui tofauti ya week na weak unaleta umaku hapa
 
Hii issue nilitegemea kuiona JF. Mwanzoni nilikuwa siielewi nikajipa muda kuijua na ni kubwa tofauti na nilivyotarajia.

Kwanza Marekani haina active anti aircraft missile systems, huwa inaamini hakuna mtu anaweza fanikiwa kuleta ndege kwenye anga lake. Ila ina layel of ballistic missiles defence system na hizi mifumo miwili ni tofauti kabisa.

Hilo balloon liko kama 60,000ft juu na zile panels zina ukubwa wa mabasi matatu kwa makadirio wanayosema. Kwa kuwa wameshaona halina hatari yoyote kwa raia basi hawana haja kushusha mavyuma makubwa kuhatarisha usalama wakati yalivyo juu hayaleti hatari yoyote. Bado wakitaka kulishusha ni ngumu kwa kuwa F-22 pekee ndio fighter yenye uwezo wa manouvre altitude hiyo na upande ule wa Montana hakukuwa na base yenye F-22. Bado shida nyingine ni kwamba hilo ni balloon lenye vyuma chini na air to air missile zinaweza penya kwenye puto zisiwe activated. Ukitumia cannon inabidi uwe na manouvre nzuri kulenga shabaha ila bado shells hazitagonga kitu kizito kulipuka na zitadondokea makazi ya watu. So mara zote US huwa inaziacha balloons zikiwa urefu mkubwa.

Limeonekana kabla halijaingia anga la Marekani ila Pentagon inavyosemekana ilihitaji kujaribu kunasa mawasiliano linayofanya ipate mwanga kidogo kuhusu China inavyowasiliana na satellites zake.

Na nchi zote hizi zina satellites ambazo hupita anga za adui na kuchunguza kwahiyo hakuna maajabu kwa balloon sanasana linaweza nasa mawasiliano kwa ukaribu zaidi na accuracy kubwa ndio maana security measures zimechukuliwa.

Jambo la msingi linaloiumiza kichwa Marekani ni namna gani ya kulishusha bila kuliharibu ili walisome.
Safi akili nyingi, NINI MAONI YAKO KUHUSU UBORA WA TEKNOLOJIA YA CHINA KULINGANISHA NA UKUBWA WA USA.
 
Wanataka walikamate wajue lilikuwa linakusanya nini kumbuka lilikuwa eneo lenye nuclear weapons and facility so debris zinaweza kuleta shida ,wale wanaakili sio nyie wazee wa Papara

USSR

Afu pia biden kaona inaweza kuleta athari kwa raia ndio maana hajafanya maamuzi hayo,wenzetu wanawaza mbele zaidi
 
USA wanachanganyikiwa zaidi kwa kuwa awajui ni namna gani Mchina analicontrol hili baloon- na ukubwa wa hizo pannel za Solar maanake ni kuwa ballon lina tumia umeme mwingi -Ambao unaweza kuwa unatumika na data capturing transmitter pamoja na Comand Unit- So ballon linaweza rudi back to China bila tatizo😁
Sasa mzee balloon gani halina umeme na halina feedback mechanism na halina namna ya kurudi? Yani hapo cha kushangaza ni nini, hivi hujui haya mambo Ujerumani iliyaunda miaka kibao nyuma, Ferninand Zeppelin aliunda vitu vyote ulivyotaja hapa miaka ya 1800 uko. Sasa cha ajabu nini, kuna makampuni mengi tu yenye balloons za hali ya hewa, surveillance na nyinginezo
 
Sasa mzee balloons gani halina umeme na halina feedback mechanism na halina namna ya kurudi? Yani hapo cha kushangaza ni nini, hivi hujui haya mambo Ujerumani iliyaunda miaka kibao nyuma, Ferninand Zeppelin aliunda vitu vyote ulivyotaja hapa miaka ya 1800 uko. Sasa cha ajabu nini, kuna makampuni mengi tu yenye balloons za hali ya hewa, surveillance na nyinginezo
Naamaanisha kuwa hili lipo more advanced sijalishangaa
 
Wakwea madafu bana eti solar,wacheni ujuaji wa kishamba apa
Linayo sola ndio hata serikali ya Marekani imesema lina sola.

Pia panels zake za solar zinaonekana hata kwa macho... Kumbuka sio puto la kupuliza kwa mdomo bali ni jitu kubwa lenye ukubwa wa mabasi matatu
 
Linayo sola ndio hata serikali ya Marekani imesema lina sola.

Pia panels zake za solar zinaonekana hata kwa macho... Kumbuka sio puto la kupuliza kwa mdomo bali ni jitu kubwa lenye ukubwa wa mabasi matatu
Huyu huna aja ya kumjibu ! Anaonekana ana mtindio wa Ubongo
 
ulicho post ni sihasa(uwongo)
kwenye video ndicho kinachojiri, maana kapost mwananchi na flashes za missile zinaonekana
Haya sasa. Wametungua puto lenu. Watu wanatungua ndege inayoenda supersonic speed, sembuse puto lenye spidi ya kobe? Unapokuja na hoja, angalau angalia uwezekano wa unachosema kuwa kweli..

 
Naamaanisha kuwa hili lipo more advanced sijalishangaa
Hilo dude la kawaida mno. Nchi inayoweza tengeneza satellite haitakiwi ishindwe kutengeneza puto rahisi kuliko ndege. Na haijulikani kama lina vitu more advanced kwa kuwa halijashushwa vionekane
 
Safi akili nyingi, NINI MAONI YAKO KUHUSU UBORA WA TEKNOLOJIA YA CHINA KULINGANISHA NA UKUBWA WA USA.
Sasa unalinganishaje samaki na kuku? Kuna uhusiano gani?
 
USAF wamelidungua baada ya kuondoka maeneo ya watu...

Wasingelilipia kwenye maeneo ya watu, maana halikuwa na risk. Ila lingekuwa risky lazima lingepigwa popote pale
 
Back
Top Bottom