Uchaguzi 2020 Marekani: Kuanzia leo, tunaweka vizuizi kwa waliohusika na kuvuruga Uchaguzi nchini Tanzania

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,448
16,312
Kupitia akaunti yake ya Twitter, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Mike Pompeo ameandika "Kuna matokeo ya kuingilia mchakato wa kidemokrasia. Kuanzia leo, tunaweka vizuizi vya visa kwa wale wanaohusika na uvurugaji wa uchaguzi nchini Tanzania. Tunabaki kujitolea kufanya kazi pamoja kuendeleza demokrasia na ustawi wa pande zote kwa nchi zetu zote mbili."

59548241-158E-4D33-92EC-C088798C7252.jpeg


Soma pia: Visa Restrictions on Tanzanians for Undermining the Democratic Process and Human Rights - United States Department of State
___________________________________________________

Marekani imetangaza kuwawekea vikwazo vya vya kuingia nchini humo maafisa wa Tanzania ambao nchi hiyo inawatuhumu kwa kile wanachokitaja kuwa kuharibu uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka 2020.

Maofisa hao wanatajwa kuhusika kuingilia mchakato wa uchaguzi na kuminya utekelezaji wa demokrasia.

Hata hivyo taarifa hiyo ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani haijabainisha ni viongozi gani hasa kutoka Tanzania waliowekewa vikwazo vya kuingia Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, Waangalizi wa uchaguzi na mashirika ya kiraia wanadai kuwepo kwa udanganyifu katika uchaguzi huo pamoja na uvunjifu wa haki za binadamu wakati na baada ya uchaguzi.

Marekani inasema kuzimwa ama kuzimika kwa mitandao, kuminywa kwa waandishi wa habari na nguvu kubwa iliyotumiwa na jeshi la Polisi kunafanya uchaguzi huo kutokua huru na wa haki.

Katika uchaguzi huo, baadhi ya wagombea kutoka vyama vya upinzani walienguliwa kwa sababu mbalimbali na wengine kukamatwa.

Tume ya uchaguzi nchini humo na hata Serikali kupitia waziri wake wa mambo ya nje, Palamagamba Kabudi ilieleza kwamba uchaguzi ulikua huru na wa haki.

Marekani inasema pamoja na hatua hii iliyochukua dhidi ya maafisa wa Tanzania, inaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya hoja hiyo, huku ikisema haitasita kuchukua hatua zaidi dhidi ya wale wanaominya demokrasia na kuvunja haki za binadamu.

''Tunaitaka Tanzania, kuwachukulia hatua wale wote waliohusika kuvuruga uchaguzi, kufanya vurugu na kuleta vitisho'' ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Juhudi za kumpata msemaji wa serikali ya Tanzania kuzungumzia suala hilo mpaka sasa hazijazaa matunda, na tutaendelea kuwatafuta kwa ajili ya kuzungumzia suala hilo

Haya ni moja ya maamuzi ya mwisho ya utawala wa rais Donald Trump ambaye amebakiza saa chache kuachia mamlaka ya urais. Mpaka sasa haijafahamika iwapo utawala wa rais mpya Joe Biden kama utatekeleza maamuzi hayo. Tayari ofisi ya Biden imetangaza kuwa itatengua sera kadhaa za Trump mara tu baada ya kuingia ofisini kesho.

BBC.
 
Kwani demokrasia yetu lazima ifanane na yao? Nyerere alisema, democracy is not like a bottle of Cocacola that you can just import from some other place, democracy should be self grown to suite the needs of our country, they can shove their sanctions up their stinky azz holes
 
Kwani demokrasia yetu lazima ifanane na yao? Nyerere alisema, democracy is not like a bottle of Cocacola that you can just import from some other place, democracy should be self grownto suite the needs of our country, they can shove their sanctions up their stinky azz holes
Usimfananishe Nyerere na vidubwana vya ajabu. Nyerere aliishi na mataifa makubwa kwa akili licha ya kutofautiana nao kiitikadi.
 
Back
Top Bottom