DOKEZO Mara: Adaiwa kujinyonga kwa kamba za viatu katika Ofisi za Kijiji baada ya kukamatwa akidaiwa kutompeleka mtoto shule

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Kuna taarifa mbaya toka Kijiji cha Sota, Kata ya Tai ,Wilaya ya Rorya Mkoani Mara ambapo Afisa Mtendaji wa kijiji hicho na mgambo wake wanatuhumiwa kumpiga hadi kufa ndugu Justine Chagwa Oliech na baadae kutundika mwili wake ndani ya Ofisi ya Mtendaji ili ionekane kajinyonga mwenyewe kwa kamba za viatu.

Taarifa za awali zinasema marehemu alikamatwa na mtendaji kwa tuhuma ya kushindwa kumpeleka mwanae shule kwa kukosa mahitaji ya shule.

Badae inasemekana mtendaji alimtaka marehemu ampe shilingi laki tatu ili amsaidie kumaliza kesi hiyo. Marehemu alipogoma kutoa hizo pesa ndo inasemeka alipokea vipigo vikali toka kwa mtendaji na timu yake hadi umauti kumkuta..

Tukio limetokea leo hii mida ya asubuhi.

================

Jastine Chagwa Oliech ni mkazi wa Kitongoji cha Sidika, Kijiji cha Sota, Kata Tai, Wilaya ya Rorya.
Jastine ni fundi baiskeli, anatengeneza baiskeli Senta ya Magamaga, hapo Sota.
Mke wake ni Mjasiriamali anatembeza mbogamboga na matunda.

Leo asubuhi Jastine alienda anakotengeneza baiskeli Magamaga.
Kufika saa tatu asubuhi Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Sota, alifika kwake na Wagambo 2.
Baada ya kufika wakamwambia kuwa anatakiwa katika Ofisi ya kijiji.

Baada ya kufika Ofisini Mtendaji akamuuliza kwa nini mtoto wako amechaguliwa kujiunga Kidato cha 1 Sota Sec na hajaripoti hadi leo?

Jastine akajibu kuwa hana pesa ndo maana mtoto hajaenda Shule.

Mtendaji akamwambia kuwa anampeleka Mahakamani kwa kosa la kutompeleka mtoto Shule.

Baada majirani wakasema kuwa wamesikia sauti za Mtendaji na Migambo kuwa kaa chini, lala chini, nyama.
Baada ya hapo mke wa Jastine akafika Ofisa ya kijiji kujua makosa ya mmewe.

Mtendaji akamwambia na kumwambia mke wake kuwa bila Tshs 300,000/ mmeo hatoki hapa.

Mtendaji kamwambia kafate pesa. Jastine akamwambia kuwa mtoto hatujampeleka shule kwa sababu hatuna pesa. Hata huko nyumbani hakuna pesa wewe rudi nyumbani ukaangalie watoto.

Baada ya muda M/kiti wa Kijiji (Jairo Hitila), Mtendaji, na Wagambo 2 wakatoka Ofisini na kufunga mlango. Kwa madai ya kwenda kunywa chai.

Mtoto wa Jastine ameolewa maeneo ya Ofisi ya kijiji hapo. Akapata taarifa na kupika chakula ili ampelekee baba yake.

Alipofika Ofisini kwa mara ya pili, akakuta Ofisi imefungwa, na hakuna mtu maeneo hayo.

Ila mlango haukuwa na Kufuli, akasukuma mlango na kumwona baba yake ndani ya nyumba.

Jastine akiwa amepiga magoti na kamba 2 za viatu akiwa ameunganisha na kufunga kwenye kenchi, na tiyari amefariki.

Baada ya hapo akapiga yowe na watu wanakijiji wakafika pale wengi sana.

M/kiti, Mtendaji na wagambo 2 wakatoweka hadi sasa.

Wakapiga simu Kituo cha Polisi Shirati (Kanda Maalum), ni kata inayopakana na Tai.

Wamefika na kuchukua mwili hadi Shirati Hospital.

Mwili uko Shirati Hospital. Familia wameona damu, na majiraha kwa Jastine. Wanataka haki itendeke na ionekane.

Jastine ana mke 1 na watoto siyo chini ya 7.

===========

KAULI YA MKUU WA WILAYA
Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka amesema “Hizo habari hata mimi nimeziona lakini siwezi kuzungumzia kwa kuwa sijapata taarifa rasmi, vyombo vya usalama vinafuatilia, tuvipe muda vitatoa ripoti kamili kama ni kweli.”

TAMKO LA JESHI LA POLISI
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime/Rorya, Godfrey Sarakikya amesema: “Hatujathibitisha mauaji hayo yanayosemwa, tukithibitisha tutatoa taarifa kwa vyombo vya habari.

“Taarifa tuliyoipata kuna mwananchi alikamatwa na Watendaji wa Kijiji akidaiwa kutompeleka mtoto kidato cha kwanza, akiwa kwenye jengo la Kijiji cha Sota, akajinyonga kwa kutumia kamba za viatu vyake, bado tunaendelea kuchunguza.”
 
Kuna taarifa mbaya toka Kijiji cha Sota, Kata ya Tai ,Wilaya ya Rorya Mkoani Mara ambapo Afisa Mtendaji wa kijiji hicho na mgambo wake wanatuhumiwa kumpiga...
Kiufupi Justin atakuwa amejiuwa hapo hakuna kesi sema jamaa wanashikiliwa miaka mingi ila navyo jua kule huwa wanakimbilia kenya haraka sana

USSR
 
Apumzike kwa amani.

Tuzidi kuwa wenye haki na kutenda haki, unapodhaminiwa dhamani yoyote kuwa mwenye haki, haki kumtetea mwenye kuishika.
 
Hii imekuwa too much sasa. Sasa tukimbilie wapi kama wanaopaswa kuratibu amani ndio wauaji wenyewe.

Chimbuko la haya yote lipo juu kabisa. Mungu atusimamie kama taifa.
 
Kiufupi Justin atakuwa amejiuwa hapo hakuna kesi sema jamaa wanashikiliwa miaka mingi ila navyo jua kule huwa wanakimbilia kenya haraka sana

USSR

FpJ7vnuWcAAbZ_x.jpeg
 
Kuna taarifa mbaya toka Kijiji cha Sota, Kata ya Tai ,Wilaya ya Rorya Mkoani Mara ambapo Afisa Mtendaji wa kijiji hicho na mgambo wake wanatuhumiwa kumpiga hadi kufa ndugu Justine Chagwa Oliech na baadae kutundika mwili wake ndani ya Ofisi ya Mtendaji ili ionekane kajinyonga mwenyewe kwa kamba za viatu.

Bwana Justine atakuwa kauwawa.

Mzazi gani asitake kumpeleka shule mwanawe aliyefaulu?

FpJ7vnuWcAAbZ_x.jpeg


Anachodanganywa Rais ni kuendelea kuwakamua wananchi choka mbaya hawa.

Mtawauwa bure hawana kitu. Tozo, afya, Kodi, faini, ushuru, michango nk ukiangalia mtu mmoja mzigo hausemeki!
 
Back
Top Bottom