Kagera: Wananchi kijiji cha Mwemage waishukuru Ofisi ya Mbunge jimbo la Nkenge kwa msaada wa mabati

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Wananchi waishio katika Kata ya Kilimilire Kijiji cha Mwemage Vitongoji Kibeo ( A) Kibeo ( B) Kanyamitwe na Kemitoma Wilayani Missenyi Mkoani Kagera wameishukuru Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Nkenge kwa msaada wa mabati.

Mbunge wa Jimbo la Nkenge Mhe. Florent Kyombo kwa kushirikiana na Viongozi wa Chama na Serikali Kata Kilimilire ofisi ya Mbunge wamekabidhi Wananchi wa kijiji Mwemage/Rwazi mabati yenye thamani ya Tsh 262,500 kwa ajili ya ukamilishaji wa Jengo la Kliniki ya mama na Mtoto

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mara baada ya kukabidhiwa mabati na Ofisi ya Mbunge Wananchi hao walisema kuwa wamepata faraja kubwa baada ya kuona kilio chao kimesikika na kusema kwamba tulikua tunapata shida sana kupata huduma ya Kliniki kutokana na Mvua zinazonyesha mara kwa mara na kusababisha watoto wetu kunyeshewa pamoja na kupiwa jua wakati wa kiangazi.

๐ท๐‘˜๐‘ก. ๐‘†๐‘Ž๐‘š๐‘–๐‘Ž-2025-2030
๐‘€๐’‰. ๐พ๐‘ฆ๐‘œ๐‘š๐‘๐‘œ-2025-2030
๐ฟ๐‘’๐‘ก๐‘–๐‘๐‘–๐‘Ž ๐‘‘๐‘–๐‘ค๐‘Ž๐‘›๐‘– ๐‘˜๐‘–๐‘™๐‘–๐‘š๐‘–๐‘™๐‘–๐‘Ÿ๐‘’-2025-2030

๐“š๐“ช๐”ƒ๐“ฒ ๐“ฒ๐“ฎ๐“ท๐“ญ๐“ฎ๐“ต๐“ฎ๐“ฎ

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom