Mapinduzi ya Zanzibar Januari 1964 yalikuwa ni ushindi na neema kubwa kwa Emirate of Dubai

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,890
109,222
Tukiitazama historia ya Dubai au UAE kwa ujumla, Oman, mwambao wote wa Zanzibar na bandari takriban zote za nchi za mashariki ya kati mpaka India na Asia ya mbali,utakuta kulijuwa na mwingiliano mkubwa wa kibiashara kati yao.

Bila shaka ni historia ndefu sana na ya zamani sana, kwa ufupi, leo tutazame mafanikio na neema kubwa iliyowadondokea Dubai na yalipotokea mapinduzi ya Zanzibar 1964.

Wimbi la awali la wakimbizi wa Zanzibar walianza kumiminika Dubai kati ya mwaka 1964 na 1968, Wazanzibari wengine, kwa mujibu wa data za UNHCR qazanzibari waliendelea kwenda kama wakimbizi baina ya mwaka 1967 mpaka 2013.

Katika miaka hiyo wengi wa watu kutoka Afrika Mashariki nzima wakaanza kumiminika kama wakimbizi Wazanzibari. Sheikh Rashid akaunda kamati ya Wazanzibari, katika wale waliofika mwanzo, waamuwe katika "wakimbizi" wanaokuja Dubai ni wepi Wazanzibari wa kweli wanaostahiki ukimbizi wa Zanzibari. AlhamduliLlah kwa kuwa kulikuwa na mwingiliano mkubwa wa watu wa Afrika mashariki wengi wanzangu na mie wasio na asili ya Zanzibari wskajipatia "status ya ukimbizi". Fsmilis. Nyingu za Dar. Tunafahamiana nao ambao wsliibgianjwente mkumbi huo na siku hizi wameshakuwa raia wa UAE kiuhalali kabisa. (kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani.

Kwanini ikawa ni ushindi na neema kwa Dubai? Historia ya Zanzibar inaonesha wazi kuwa Zanzibar wakati wa mapinduzi ilikuwa ni nchi iliyoendelea sana kielimu na kiuchumi kuliko nchi nyingi duniani.

Sheikh Rashid bin Saeed Al Maktoum, ambae ni babu wa Mfalme wa sasa wa Dubai, aliposhauriwa na mshauri wake wa Kiingereza (Duff) kuhusu wakimbizi wa Zanzibar, hakusita kuwakaribisha na kuwapokea kwa nia njema kabisa.

Kwa bahati nzuri kabisa, wakimbizi wengi wa Zanzibar wa wakati huo walikuwa ni wasomi na wataalam wa biashara na siasa za kidunia.

Wasomi na wataalam hao ikawa ni neema kubwa kwa Ufalme wa Dubai. Ufalme wa Dubai ukajipatia washauri, wafanyakazi na wataalaam mbali mbali wenye utamaduni unaofanana kabisa na wao.

Wazanzibari hao hawakuliangusha jina la Zanzibar, walifanya kazi na biashara zao na. walishauri serikali ya Dubai kwa uaminifu kabisa.

Mapinduzi ya Zanzibar kisiasa yalizaa pia mapinduzi ya kiuchumi Dubai, yenye neema kubwa sana kwa Dubai. "Kufa kufaana".

Itaendelea kidogo kidogo kwa mtindo wa maswali na majibu.

Yeyote anaweza kuongezea nyama kwenye upungufu. Yeyote anaweza kuuliza yanayohusiana na hii mada.
 
1687421173894.png

1960's Dubai Creek, walivyoikuta wakimbizi wa mwanzo mwanzo kutokea Zanzibar 👆🏾

1687421326246.png

1980's Dubai Creek, wakimbizi wa Zanzibar bega kwa bega wakichangia maendeleo ya Dubai👆🏾

1687427077487.png

1990's Dubai, wakimbizi wa kutokea Zanzibar kwenye 60's wengi wao wamezeeka, watoto na wajukuu wakaendelea kuijenga Dubai kama nyumbani kwao, wengi wakazaliwsma hapo. Cha kufurahisha, wazee wao hawakuwacha kuwarithisha lugha mila na desturi za Kizanzibari.
 
Tukiitazama historia ya Dubai au UAE kwa ujumla, Oman, mwambao wote wa Zanzibar na bandari takriban zote za nchi za mashariki ya kati mpaka India na Asia ya mbali,utakuta kulijuwa na mwingiliano mkubwa wa kibiashara kati yao.

Bila shaka ni historia ndefu sana na ya zamani sana, kwa ufupi, leo tutazame mafanikio na neema kubwa iliyowadondokea Dubai na yalipotokea mapinduzi ya Zanzibar 1964.

Wimbi la awali la wakimbizi wa Zanzibar walianza kumiminika Dubai kati ya mwaka 1964 na 1968, Wazanzibari wengine, kwa mujibu wa data za UNHCR qazanzibari waliendelea kwenda kama wakimbizi baina ya mwaka 1967 mpaka 2013.

Katika miaka hiyo wengi wa watu kutoka Afrika Mashariki nzima wakaanza kumiminika kama wakimbizi Wazanzibari. Sheikh Rashid akaunda kamati ya Wazanzibari, katika wale waliofika mwanzo, waamuwe katika "wakimbizi" wanaokuja Dubai ni wepi Wazanzibari wa kweli wanaostahiki ukimbizi wa Zanzibari. AlhamduliLlah kwa kuwa kulikuwa na mwingiliano mkubwa wa watu wa Afrika mashariki wengi wanzangu na mie wasio na asili ya Zanzibari wskajipatia "status ya ukimbizi". Fsmilis. Nyingu za Dar. Tunafahamiana nao ambao wsliibgianjwente mkumbi huo na siku hizi wameshakuwa raia wa UAE kiuhalali kabisa. (kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani.

Kwanini ikawa ni ushindi na neema kwa Dubai? Historia ya Zanzibar inaonesha wazi kuwa Zanzibar wakati wa mapinduzi ilikuwa ni nchi iliyoendelea sana kielimu na kiuchumi kuliko nchi nyingi duniani.

Sheikh Rashid bin Saeed Al Maktoum, ambae ni babu wa Mfalme wa sasa wa Dubai, aliposhauriwa na mshauri wake wa Kiingereza (Duff) kuhusu wakimbizi wa Zanzibar, hakusita kuwakaribisha na kuwapokea kwa nia njema kabisa.

Kwa bahati nzuri kabisa, wakimbizi wengi wa Zanzibar wa wakati huo walikuwa ni wasomi na wataalam wa biashara na siasa za kidunia.

Wasomi na wataalam hao ikawa ni neema kubwa kwa Ufalme wa Dubai. Ufalme wa Dubai ukajipatia washauri, wafanyakazi na wataalaam mbali mbali wenye utamaduni unaofanana kabisa na wao.

Wazanzibari hao hawakuliangusha jina la Zanzibar, walifanya kazi na biashara zao na. walishauri serikali ya Dubai kwa uaminifu kabisa.

Mapinduzi ya Zanzibar kisiasa yalizaa pia mapinduzi ya kiuchumi Dubai, yenye neema kubwa sana kwa Dubai. "Kufa kufaana".

Itaendelea kidogo kidogo kwa mtindo wa maswali na majibu.

Yeyote anaweza kuongezea nyama kwenye upungufu. Yeyote anaweza kuuliza yanayohusiana na hii mada.
Sababu ya kukimbilia dubai ilikuwa ni nini hasa hasa..???
 
katika "wakimbizi" wanaokuja Dubai ni wepi Wazanzibari wa kweli wanaostahiki ukimbizi wa Zanzibari. AlhamduliLlah kwa kuwa kulikuwa na mwingiliano mkubwa wa watu wa Afrika mashariki wengi wanzangu na mie wasio na asili ya Zanzibari wskajipatia "status ya ukimbizi". Fsmilis. Nyingu za Dar. Tunafahamiana nao ambao wsliibgianjwente mkumbi huo na siku hizi wameshakuwa raia wa UAE kiuhalali kabisa. (kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani.
Ukirudi uje kutueleza maana ya haya maneno au au huko shuleni ulienda kusomea ujinga?
 
Sababu ya kukimbilia dubai ilikuwa ni nini hasa hasa..???
Wazanzibari wengi kwanza kabisa walikimblia Mombasa Kenya na baadhi yao Dar es Salaam Tanzania.

Baada ya hapo wakaanza kuondoka na kukimbilia Dubai, Oman, Kuwait, Comoros na Europe. Na nchi zingine kwa uchache.

Sababu kubwa ikiwa ni kubaguliwa na kunyanyapaliwa.
 
Ukirudi uje kutueleza maana ya haya maneno au au huko shuleni ulienda kusomea ujinga?
Hayahusiani na hii mada,lakini, kwanza hywa siweki neno "su".

Hizo sentensu zipo mbili za Kiswahili, moja ya English zenye maana zinazofanana. Hutumia mojawapo kutegemea na maudhui.

1) Hivi huko shuleni mlienda kusomea ujinga?

2) Hakika shuleni ulienda kusomea ujinga.

3) You're an uneducated fool from an uneducated school.

Turudi kwenye mada.
 
Hivyo ndivyo wengi tuliaminisha, nakushauri jisomee utafiti uliofanywa na msomi wa Havard ambae amewahoji walioshiriki mapinduzi mwanzo mwisho. Bofya chini hapo ujisomee:

Iwa hyo unataka kusema wa tanganyika ambao ni sio waislam, ndio walileta mapinduzi ya zanzbar ili kuwaua na kuwa tesa waislam..
 
Sitaki kusema lolote, soma tafiti ya kisomi nimekuwekea link juu kidogo hapo.

Kama hukendi kusoma, ingia youtube tafuta "kwaheri uhuru kwaheri ukoloni" utakikuta kimeongelewa sana hicho kitabu.

Nakushauri pendelea kujisomea.
 
Back
Top Bottom