Ni kweli Karume, Salmin Amour na Wanamapinduzi walioa kwa nguvu mabinti wa Kiarabu baada ya Mapinduzi ya Zanzibar?

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,834
18,835
Nimesoma historia ya Zanzibar imejaa mambo mengi ya giza ila nitajiita kwenye hili moja.

Je ni kweli Karume, Salmin Amour, Natepe pamoja na karibia ya maafisa wote wa baraza la Mapinduzi walioa kwa nguvu mabinti wa kiarabu, na kihindi baada ya mapinduzi ya Zanzibar?

Inasemekana kuwa mke wa Salmin Amour alimtoroka na kwenda kuolewa huko Norway baada ya kuwa kwenye ndoa aliyolazimishwa kwa muda

Na wazazi wa kiarabu waliwekwa ndani na kuchapwa mijeledi baada ya kugoma mabinti zao kuolewa na watu weusi!?
 
Duh...!.
Wana bodi, japo tuko kwenye harakati za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge, kuna swali linanitatiza kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ambapo majibu yake sahihi, pia yanaweza kuwa ni kiashiria tosha cha mshindi wa urais wa Zanzibar, iwapo uchaguzi utakuwa huru na wa haki.

Swali hili lahusu ukweli haswa kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, 1964, baada ya kuibuka kwa kitabu kingine kiitwacho "Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru"
View attachment 2077603
kilichoandikwa na Mwanazouni wa Zanzibar, Dr. Harith Ghassany, kama kilivyofanyiwa mapitio na mwandishi Mohamed Said kwenye gazeti la Al-Nuur la leo.

Ghasanny anasema kumbe Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalitekelezwa na askari mamluki wa Kimakonde (Wakata Mkonge) ambao waliongozwa na Mzee Mohamed Omar Mkwawa (Tindo) chini ya Amiri Jeshi wa jeshi la mamluki hao Victor Mkello (RIP). (kumbe amiri jeshi hakuwa Mganda John Okello pekee, bali pia Mkello yumo?!.

Mamluki hao walitumia zana zao za kukatia mkonge, zile sime za makali kuwili, walizisunda kwenye nguo zao za ndani na kusafirishwa kwa mitumbiwi usiku usiku kupitia Kipumbwi. Jee wale mashuhuda wa Mapinduzi yale Matukufu ya Zanzibar, wanayakubali haya?.

Pia mwandishi anamalizia kwa kusema hata mauaji ya Karume, hayakutekelezwa na wapinga Mapinduzi, bali ni miongoni mwa hao hao wanamapinduzi, baada ya kupishana kauli fulani fulani za uendeshaji wa Zanzibar baada ya Mapinduzi.

Nimesoma kitabu cha John Okello kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar,
View attachment 2077618
yeye anasema yake, vitabu kadhaa vya waandishi wazungu wanasema yao, historia tukuka ya Mapinduzi Matukufuya ya Zanzibar nayo nayo inasema kivyake, hivi hakuna any straight line yoyote kuhusu Mapinduzi hayo, ya Zanzibar?.
Jee yalipangwa na nani? Yalitekelezwaje?.
Nini haswa kilichotokea usiku ule wa Januari 11?.
Nani alifanya nini wapi?
Na mwisho tuzungumzie wafaidika wa Mapinduzi hayo Matukufu ya Zanzibar na bila kuwasahau wahanga wa Mapinduzi hayo ambao kwako yatakuwa sio Matukufu, ni kina nani haswa?, na kama kuleta amani na utangamano wa Zanzibar kuhusu Mapinduzi hayo kutahitajika kuundwa kwa Tume ya Ukweli na Upatanisho, "Truth and Reconciliation Commission" ili waliohasimiana kutokana na Mapinduzi hayo, wapatanishwe kwa maslahi mapana ya Zanzibar?.

Majibu ya maswali haya yatasaidia kujua mustakabali wa matokea ya uchaguzi wa Zanzibar kudhirihisha kuwa Wazanzibari ni wamoja, hakuna kundi la walishiriki Mapinduzi ndio wenye uhalali zaidi kuitawala Zanzibar kuliko wasioshiriki, after all kumbe Mapinduzi yenyewe, yametekelezwa na askari mamluki wa Kimakonde, toka mashamba ya mkonge Tanga!.

Pasco
Rejea za Mwandishi huyu kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
  1. Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila Majibu -1
  2. Neno "Matukufu" Katika Mapinduzi ya Zanzibar, Lilitoka Wapi, na Yana Utukufu Gani?!,
  3. Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa! Walikimbia Wenyewe - Mzee Sukari
Tarehe kama ya leo 11/01/1964 miaka 60 iliyopita, ndio Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalifanyika!. Alfajiri ya Tarehe 12 Januari, 1964 ilikuwa ni kutangazwa tuu!.

Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali
 
Vipi kuhusu hao mabinti wa Kiarabu kuolewa kwa nguvu?
 
Back
Top Bottom