Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,921
- 30,266
MIAKA 20 BAADA YA KUFIKA PWANI YA KIPUMBWI: HISTORIA YA KAMBI YA KIPUMBWI KATIKA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
Miaka 20 iliyopita tarehe kama ya leo 9 December, 2003 ndiyo siku Mohamed Omari Mkwawa alipotufikisha mimi na Dr. Harith Ghassany Kipumbwi.
Siku hii iliangukia kuwa siku Tanganyika ilipopata uhuru wake.
Kipumbwi ni kijiji kidogo cha wavuvi kilomita chache kutoka Tanga.
Hapa Kipumbwi ndipo ilipowekwa kambi ya askari mamluki wengi wao Wamakonde waliokuwa wanapewa mafunzo ili washiriki katika mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Historia hii si ngeni kwa sasa kwani Dr. Ghassany kaieleza kwa kirefu katika kitabu chake, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru," (2010).
Lakini kabla ya yeye kufika Kipumbwi na kushuhudia kwa macho yake yale aliyoelezwa na Mzee Mkwawa Tanga mjini kuwa alihusika katika kuwavusha Wamakonde kwa siri kuingia Zanzibar kushiriki katika mapinduzi hii ilikuwa siri kubwa sana.
Sikupata siku kumuona Dr. Ghassany kafurahi kama siku ile.
Kwa hakika kabisa alikuwa na haki ya kufurahi kwani alikuwa amekitegua kitendawili kikubwa; kwanza kuwa kuwa kulikuwa na kambi ya mamluki katika ardhi ya Tanganyika waliovushwa na kuingia Zanzibar kusaidia mapinduzi.
Kafika Kipumbwi na Mzee Mkwawa akatupitisha sehemu zote kuanzia pango la chini walikukuwa wanaficha majahazi yao hadi kutuonyesha mgahawa mdogo walipokuwa wakila usiku kabla ya kuingia katika vyombo na kuanza safari.
Pili Kipumbwi ilisaidia kueleza mauaji yaliyotokea mashamba ambako Waarabu wengi waliuliwa.
Leo naikumbuka siku hii miaka 20 iliyopita na naweka picha tulizopiga Kipumbwi.
PICHA: Picha ya mwisho ni Mzee Mohamed Omari Mkwawa na mkewe.