#COVID19 Mapambano dhidi ya COVID-19: Rais Samia anayo dhamira ya kweli? Kinachoendelea India kinatisha

Corona ni changamoto sema wabongo toka walivyoambiwa ishu ya nyungu kila siku wanaona mzaha tuu ila hiyo ishu ni hatari mno kuliko maelezo...
 
Hivi ni kweli kabisa Rais Samia ana nia ya kweli ya kupambana na COVID-19?

Sijui kama na nyie mnafuatilia yanayoendelea huko India sasa hivi!

Akina Narendra Modi walikuwa huko West Bengal wanapiga kampeni za kisiasa utadhani hamna kesho. Ona sasa kilivyoumana.

Sasa kweli hiyo kamati aliyoiunda Rais Samia ili imshauri kuhusu corona ndo imemwambia kwamba ni sawa tu watu kwenda na kurundikana hapo uwanja wa Kirumba namna hiyo?

Ona hata hapo walipokaa hao viongozi! Hakuna social distancing. Hakuna barakoa. Hakuna tahadhari yoyote ile ya maana.

Hahahaaaaa…..what is this?

View attachment 1769853
Imekwenda chukua maoni msumbiji maana ni ya saddic!
 
Hii Covid-19 iliyopotea nchini mara tu baada ya kifo cha JPM inafikirisha sana.
Yaaani! Nadhani kuna uhuni mwenda zake alifanyiwa. Kabla ya kifo cha chake mitandaoni kulikuwa na taarifa nyingi kuonyesha watu wengi walikuwa wanakufa kwa Covid-19. Cha ajabu baada ya kuondoka yeye tu ghafla vifo vikapotea.
 
UJINGA . Hatuna Mungu kuliko wengine .
Una uhakika hao wengine wanamtumainia yeye? Unadhani alikuwa mjinga aliposema tusiache kumwomba? Hao wengine wanayakimbia madhabahu corona inapokuja mjini ilhali sisi tunaikimbilia na kuitumainia. Sisi tunamwomba na kumlilia hadharani wakati wa shida ilhali hao wengine hutuita washamba na washirikina tufanyapo hivyo.

Mungu siyo Athumani mjomba. Wao wameamua kumpigia magoti shetani kwa kusema hili si suala la kimungu bali la kisayansi. Sisi tumemchagua Mungu na tulifikia mpaka hatua ya kufanya maombi ya kitaifa! Ni nchi gani nyingine uliiona ikifanya hivyo?

Usimwite mjinga anayemtaja Mungu mzee. Kuna dhambi nyingine mnazichuma bila hata sababu.
 
Mungu wa mbinguni wewe humuamini sis tunamuamini na tunamuishi, ndiyo maana majaribio yote yanashinwa. Mungu akisimama wewe si chochote
Unakosea sana, kwahiyo kwasababu watu wanamtumaini Mungu ndio wasichukue tahadhari?

Mungu anahitaji pia wanadamu watumie vizuri akili aliyowapa na ndio maana aliwapa tofauti na wanyama.

Tahadhari ni muhimu sana.
 
Hivi ni kweli kabisa Rais Samia ana nia ya kweli ya kupambana na COVID-19?

Sijui kama na nyie mnafuatilia yanayoendelea huko India sasa hivi!

Akina Narendra Modi walikuwa huko West Bengal wanapiga kampeni za kisiasa utadhani hamna kesho. Ona sasa kilivyoumana.

Sasa kweli hiyo kamati aliyoiunda Rais Samia ili imshauri kuhusu corona ndo imemwambia kwamba ni sawa tu watu kwenda na kurundikana hapo uwanja wa Kirumba namna hiyo?

Ona hata hapo walipokaa hao viongozi! Hakuna social distancing. Hakuna barakoa. Hakuna tahadhari yoyote ile ya maana.

Hahahaaaaa…..what is this?

View attachment 1769853
Hapo ndio ujue Mungu alishatuponya na corona. Mlundikano haukuanza leo, tunawaamini viongozi wetu. Mbona mwaka 2019 waliamua kugunga shjle na vyuo? Ni kwa sababu waliiona hatafi ya corona. Na kwa nini baadaye waliamua kufungua sbule na vyuo? Ni kwa sababu walijiridhisha kuwa Mungu amesikia maombi yetu na hatari ya corona imeondoka. Usiwapangie wala usilazimishe shida kuwa ipo wakati Mungu alishaiondoa. Kama unaitaka iguate huko marekani, India, Brazil, Mexico na kwingineko.
Usidhani kuwa kinga unayoitaka itaweza kukuokoa kama kweli corona ikitia timu! Fikiri kidogo tu: India ni taifa la kwa za duniani kwa uwezo wakuzalisha chanjo kwa wingi! Na wamechanja watu wengi kiliko nchi yoyote duniani! Wanavaa barakoa muda mwingi Lakini hilo halijawasaidia! Corona ikiwepo huwezi kuitafuta kwa tochi kama washabiki wa corona mnavyoitafuta Tanzania! Mnalazimisha kila anayekufa kuwa kafa kwa corona! Wengine wanaona ni sifa kujitangaza kuwa wana corona!! Ukiita kwako inakuja kweli maana kuna roho nyuma ya corona! Ndiyo maana Tanzania haina nguvu maana hiyo roho ya corona imedhibitiwa kwa maombi na kwa imani kwa Mungu! Hiyo ndiyo tofauti ya Tanzania na mataifa mengine! Hiyo ndiyo siri ya watanzania ukiwamo wewe kuwa salama! Kama wewe hauamini wako watu wanaoamini na kuiombea nchi yetu na wewe kufaidika na majibu ya Mungu!
Rai yangu: Watanzania tumshukuru Mungu na the delete kuiombea nchi yetu. Tunaonewa wivu sana!! Jibu letu ni kwamba, tulimtanguliza Mungu mbele wengine walitanguliza sayansi mbele katika mapambano na corona. Hatukuidharau sayansi lakini sayansi haina majibu yote na changamoto ya corona imethibitisha hilo! Case study ya Tanzania na Marekani/India kuhusu corona inaweka ukweli huu wazi!
 
Kwani kuna COVID-19 kwenye ardhi hii?
Ipo lakini imedhibitiwa na Mungu, haina nguvu kutokana na maombi kwa Mungu. Tulimtanguliza Mungu kwa maombi na haya ndiyo matokeo yake. Wengine walitanguliza sayansi na Mungu akaachwa nyuma. Hao waliotanguliza sayansi mbele ndio wanaotushinikiza na sisi tutangulize sayansi!! Wao haikuwasaidia na haitatusaidia sisi. Hatuidharau sayansi lakini si jibu la mambo yote!!
 
mim natamani mama asiwe anachanganyika na watu saana leo kakohoa. pale kirumba vumb sana nashauri mikusanyiko ipungue ahutubie kwa njia ya video

Sent using Jamii Forums mobile app
Usimwingizie hofu! Yuko salama sana mikononi mwa Mungu. Msiitafute corona kwa tochi! Ikitia timu hutanitachi tochi kuitafuta! Waulize India kama inawezekana kuificha corona! Wana chanjo nyingi kuliko nchi zote lakini pia wana corona nyingi! Chanjo si mwarobaini!
 
Ipo lakini imedhibitiwa na Mungu, haina nguvu kutokana na maombi kwa Mungu. Tulimtanguliza Mungu kwa maombi na haya ndiyo matokeo yake. Wengine walitanguliza sayansi na Mungu akaachwa nyuma. Hao waliotanguliza sayansi mbele ndio wanaotushinikiza na sisi tutangulize sayansi!! Wao haikuwasaidia na haitatusaidia sisi. Hatuidharau sayansi lakini si jibu la mambo yote!!
Nimemzika rafiki mmoja aliyefariki Corona, alikuwa mwumini hodari sana. Nadhani kwa jumla hao masista zaidi ya 50 Wakatoliki waliofariki Januari-Februari mwaka huu wote walisali saaana,.

Hakuna dalili hata kidogo kwamba Tanzania ina pungufu ya vifo kuliko tuseme Kenya, isipokuwa kuficha kwa data.
Kuficha data ni sawa na kufunga macho. Ukifunga macho ni rahisi kusema "Sioni kitu". Hongera!!
Madai yako Uhindi wamepiga chanjo kuliko nchi nyingine ni mfano wa kufunga macho. Hadi mwisho wa Aprili 2021 walitoa chanjo milioni 155 hivi (154,989,635; takriban mil. 25 kati yao walipokea zote mbili, wengine mara ya kwanza tu) ambayo ni idadi kubwa LAKINI si kubwa ukilinganisha na idadi ya watu wao. Maana wote ni BILIONI 1.3, hivyo ni asilimia ndogo. Je unaweza kukadiria mwenyewe? (nikuambie siri: 11% jumla, chini ya 2% waliokamilika) .
Halafu barakoa? Wana mamilioni wenye umaskini mkali hawana barakoa.

Nchi iliyofaulu kuliko zote ni China. Kwa nini? Kwa sababu wanasali? Hapana, wanatisha Wakristo na kuhubiri atheism. Wamefaulu kwa sababu ya kuchukua hatua kali za kidikteta na kutisha watu kila mahali, pamoja na nidhamu ya ajabu.

Usipotaka police state ya kiatheisti una chaguo:
  • ama kufunga macho na kudai eti huoni kitu
  • au kuchukua tahadhari, kubana shughuli kadhaa zisizokwamisha uchumi (kufunga vilabu, kuweka mipaka ya mikutano), halafu chanjo, chanjo, chanjo
 
Unaonaje: vipi kufuata tahadhari zote, bila hofu, kutumia kipaji kikubwa cha Mungu ambacho ni ubongo, kuwaombea wote walioathiriwa, kutekeleza amri ya Yesu kutembela wagonjwa na kuwasaidia, na kumwomba Mungu kwa hekima tusifanye mambo ya kijinga?

(usisahau: Mungu hajatupa kichwa ili kinyozi apate kitu, tumekipewa ili tutumie vema yaliyomo yake! Si mambo ya nje, zingatia yale yaliyo ndani!)
 
Una uhakika hao wengine wanamtumainia yeye? Unadhani alikuwa mjinga aliposema tusiache kumwomba? Hao wengine wanayakimbia madhabahu corona inapokuja mjini ilhali sisi tunaikimbilia na kuitumainia. Sisi tunamwomba na kumlilia hadharani wakati wa shida ilhali hao wengine hutuita washamba na washirikina tufanyapo hivyo.

Mungu siyo Athumani mjomba. Wao wameamua kumpigia magoti shetani kwa kusema hili si suala la kimungu bali la kisayansi. Sisi tumemchagua Mungu na tulifikia mpaka hatua ya kufanya maombi ya kitaifa! Ni nchi gani nyingine uliiona ikifanya hivyo?

Usimwite mjinga anayemtaja Mungu mzee. Kuna dhambi nyingine mnazichuma bila hata sababu.
Ninachokipinga mr/miss Tanzanature ni hicho unachokitetea. Mungu ni wa wote wala si waTz peke yao. Aliewakemea maaskofu na mapadre kuacha kuvaa barakoa yuko wapi ?!.

Sema Sisi wa Africa kuna hali fulani ya hewa inatu favour. Lakini usidanganyike sisi kuwa na Mungu zaidi ya mataifa na mabara mengine.
 
Hii habari imetoka lini? Msitake kupotosha watu, ni wazi Kenya walilegeza masharti kabla hawajajuwa kinacho endelea India - hivi sasa India ndilo Taifa linalo kabiriwa na variant ya COVID ambayo maambukizi ni unique kweli, inakwenda kwenye mapafu moja kwa moja bila ya kukaa kwenye pua na koo kwa muda, haina symptoms zilizo zoloeka na wakati hakuna symptoms kabisa zaidi ya nyumonia kali ndani ya muda mfupi, kibaya zaidi inashambulia mpaka watoto wadogo, kitu ambacho immune system ya watoto ilikuwa na uwezo mkubwa kudhibiti conventional COVID-19 lakini sio variant hii, swali ni: kwa nini? Je, kuna wana sayansi i.e Virologists wanachezea watu akili wakiwa na lengo la kutisha Dunia ili waweze kuuza chanjo zinazo zalishwa na Big Pharma Companies ili zipige hela ndefu, variant ya India inatia shaka sana na kumbuka India ndio imepewa kibari cha Big Pharma Companies kuzalisha chanjo za Oxford-AstraZeneca za kuziuzia third World kupitia WHO, iweje tena leo India hiyo hiyo ndio ikumbwe na virusi ambavyo ni more aggressive and extremly dangerous kama sio mad scientist ndio wanevi-manipulate kwenye maabara yao ili chanjo zao ziuzike fasta baada ya kuleta taharuki Duniani - si watu wa kuaminka hata kidogo.

Tukio hili lisilo la kawaida huko India, sioni kiongozi yeyote Duniani mwenye akili tinamamu anaweza kuruhusu wasafiri kutoka India kuingia/kanyaga nchini mwake, kabla ya tatizo hili hatarishi halijapatiwa ufumbuzi wa kuaminika.
 
Kinachowatatiza watu ni Tanzania kuamua kutofanya au kulazimika kufanya yanayofanyika ulimwenguni kote kuhusu corona. Ni ajabu watu wanalazimisha wasikie case za covid ni ngapi, watu wakae social distance, watu wavae barakoa, serikali iweke lockdown... hivi haya hayajafanyika tangu covid iingie mwanzoni mwa 2020, umesikia wapi mamia wakifa na covid au maelfu kama mnavyodanganywa na western media zenye staged images kuwa kwa siku wanakufa watu 3,000?

Maisha ya Tanzania yamebaki kuwa ya kawaida. Haina maana covid haipo lakini sio sawa kutisha watu kuwa hayo mafua ni threat kwa kiwango hicho. Hivi ni kusema viongozi woote hao wakubwa hawajui hatari iliyopo (kama ipo kwa maana hiyo)? Mh. Rais kukaa vile unataka kusema wao na kamati nzima inayomlinda hawana taarifa za kitaalam na kiulinzi kuwa yuko salama? Usalama wake ni mpaka avae barakoa kama Biden?

Badili mindset u-deal na mazingira halisi tuliyo nayo. Misongamano inayofanyika Tanzania tangu watishie kuwa kutakuwa na vifo vingi umeviona wapi?

Tatizo lipo, lakini sio lazima tulikabili kama wanavyofanya kila mahali duniani, kumfurahisha nani?
 
Tulia tu. Ningeshangaa tusipoona ongezeko la vifo baada ya mikutano mingi ya futari za Ramadan. Haitakuwa vikali hapa kama kwenye nchi baridi (kwa sababu hapa maisha ni zaidi nje ya vyumba vilivyofungwa). Tusipopima labda inawezakana kuificha tena kiasi.
Wizara tayari wametangaza tena kuchukua tahadhari, ila sioni bado amri kwa polisi kuifuatilia. (Mwananchi 30.04.: "Serikali yatoa maagizo vita dhidi ya corona"). Sijui kwa nini wanatumia lugha ya "vita dhidi ya corona" lakini hawafuatilii. Kawaida ya nchi hiyo?
 
Yaaani! Nadhani kuna uhuni mwenda zake alifanyiwa. Kabla ya kifo cha chake mitandaoni kulikuwa na taarifa nyingi kuonyesha watu wengi walikuwa wanakufa kwa Covid-19. Cha ajabu baada ya kuondoka yeye tu ghafla vifo vikapotea.
Yupo mzee mmoja maarufu sana nimemuona hivi karibuni havai barakoa.
 
Back
Top Bottom