Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,987
RAIS SAMIA AWASILI INDIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili jijini New Delhi, India leo tarehe 08 Oktoba, 2023 kwa ajili ya kuanza ziara ya kitaifa ya siku nne nchini humo.
Mapokezi rasmi ya Rais Dkt. Samia yatafanyika tarehe 09 Oktoba, 2023 ambapo atapokelewa na mwenyeji wake Rais wa India, Mhe. Droupadi Murmu kwa pamoja na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mhe. Narendra Modi.
Ziara ya Rais Dkt. Samia nchini India ni mwendelezo wa ushirikiano na uhusiano mzuri wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizi mbili ambapo sekta muhimu nchini kama Afya, teknolojia, kilimo, uchumi wa buluu, biashara, uwekezaji, maji na elimu zinatarajiwa kuwa kipaumbele cha majadiliano wakati wa ziara hii.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiendelea na kazi wakati akiwa safarini kuelekea Mji wa New Delhi nchini India kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa tarehe 08 Oktoba, 2023. Mhe. Rais Samia alitumia usafiri wa Ndege ya Shirika la ATCL ambalo limeanza safari zake kutoka Tanzania mpaka India.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi, New Delhi nchini India kwa ajili ya kuanza rasmi ziara ya Kitaifa tarehe 08 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiangalia kikundi cha ngoma cha asili ya India kikitumbuiza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi, New Delhi-India kwa ajili ya kuanza rasmi ziara ya Kitaifa Oktoba 08, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Watanzania mara baada ya kuwasili New Delhi nchini India kwa ajili ya kuanza rasmi ziara ya Kitaifa tarehe 08 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje ya India Mhe. Dkt. Subrahmanyam Jaishankar mara baada ya mazungumzo New Delhi nchini humo tarehe 08 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wafanyabiashara pamoja na Wawekezaji mbalimbali wa Tanzania wakati akiwa njiani kuelekea New Delhi kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa nchini India tarehe 08 Oktoba, 2023.