#COVID19 Mapambano dhidi ya COVID-19: Rais Samia anayo dhamira ya kweli? Kinachoendelea India kinatisha

Ni katika utaratibu ule ule tuliouzoea, mama amekuwa mbobevu wa NGOs. Anawafurahisha wale wenye platform ya kusikika kwa manufaa ya wapiga dili.

Nani mwingine umemsikia anazungumzia korona au vifo vya korona tangu awepo yeye.

Tuliambiwa ile Marathon ya Kili itajibu, tukatishiwa kuwa baada ya maziko ya Mwamba tutaelewa sayansi ya barakoa, mechi za simba na yangu, Mkapa ilijaa yote tukaambiwa tutaokota kama kumbi kumbi.

Leo wooote kimya.
Ficha ujinga wako. Mwaka jana Magufuli alitangaza corona imeisha akapewa na ''kombe'' la ushindi kwa kuishinda corona. Kila mtu akamsifia (wajinga ofcourse ) na wengine wakasema wakawa wana-mock njia zinazochukuwa hatua au watu wanaokufa. Matokeo yake kuanzia mwaka jana mwezi wa 12 mpaka wa tatu corona ikarudi kwa kasi na vifo vikaondoka na watu wengi. Sasa wewe unarudia tena kosa lile lile. Hivi unajua hata India walikuwa wanasema corona imeshapita? Corona ina tabia ya kuja kwa awamu na inapoingia inaingia kimya kimya sana lakini watu wanapoanza kuugua na kufa inakuwa ni kishindo kikuu. Hata Tanzania sasa hivi haiko salama na inaweza kurudi tena tena hali ikawa mbaya mpaka kila mtu akashangaa.
 
Wanapata kigugumizi kwa kufikiria gharama ambazo itawalazimu kuingia wakikubali kuwa chanjo inahitajika!! Jiwe yeye aliamini kuwa angekubali chanjo ingebidi kudivert funds kutoka kwenye Miradi yake ya SGR na stiegler's Gorge, hivyo akakomaa na denial kuwa corona hakuna!! He never thought about the human aspect.

There is another aspect on he health angle; nobody knows the long term side effects of the vaccines hence the hesitancy to accept that they be introduced.!! But studies in other countries have shown that the benefits of vaccination outweigh the risks!! Watu Wengi waliochanjwa hata wakiambukizwa corona hawafi lakini wengi wanaokufa ni wale ambao hawajachanjwa.!!
India ambao wanatengeneza hizo chanjo wanakufa kama kuku wa kideli, pamoja na kutokufuata mashariti yeyote ya WHO bado tunadunda maisha yanaendelea kama kawaida,wacha kutisha watu, mbona Kenya walio nunua vaccines mbona maambukizi yanaendelea? vaccines zenyewe zina effect mataifa mengi yameanza kuzikataa nyinyi mnataka ziletwe huku.
 
Corona ni changamoto sema wabongo toka walivyoambiwa ishu ya nyungu kila siku wanaona mzaha tuu ila hiyo ishu ni hatari mno kuliko maelezo...
Kuna dakatari kafa Kenya kwa korona. Na yeye kama Magufuli alikuwa anaidharau na kusema nyungu inatosha.
 
Nimemzika rafiki mmoja aliyefariki Corona, alikuwa mwumini hodari sana. Nadhani kwa jumla hao masista zaidi ya 50 Wakatoliki waliofariki Januari-Februari mwaka huu wote walisali saaana,.

Hakuna dalili hata kidogo kwamba Tanzania ina pungufu ya vifo kuliko tuseme Kenya, isipokuwa kuficha kwa data.
Kuficha data ni sawa na kufunga macho. Ukifunga macho ni rahisi kusema "Sioni kitu". Hongera!!
Madai yako Uhindi wamepiga chanjo kuliko nchi nyingine ni mfano wa kufunga macho. Hadi mwisho wa Aprili 2021 walitoa chanjo milioni 155 hivi (154,989,635; takriban mil. 25 kati yao walipokea zote mbili, wengine mara ya kwanza tu) ambayo ni idadi kubwa LAKINI si kubwa ukilinganisha na idadi ya watu wao. Maana wote ni BILIONI 1.3, hivyo ni asilimia ndogo. Je unaweza kukadiria mwenyewe? (nikuambie siri: 11% jumla, chini ya 2% waliokamilika) .
Halafu barakoa? Wana mamilioni wenye umaskini mkali hawana barakoa.

Nchi iliyofaulu kuliko zote ni China. Kwa nini? Kwa sababu wanasali? Hapana, wanatisha Wakristo na kuhubiri atheism. Wamefaulu kwa sababu ya kuchukua hatua kali za kidikteta na kutisha watu kila mahali, pamoja na nidhamu ya ajabu.

Usipotaka police state ya kiatheisti una chaguo:
  • ama kufunga macho na kudai eti huoni kitu
  • au kuchukua tahadhari, kubana shughuli kadhaa zisizokwamisha uchumi (kufunga vilabu, kuweka mipaka ya mikutano), halafu chanjo, chanjo, chanjo
Kwahio data za maelfu ya watu waloambukizwa au kufa baada ya kuhudhuria shughuli za msiba wa kitaifa zafichwa?

Na pia data za maelfu ya watu walohudhuria leo sherehe za Mei Mosi ambao watakuwa wameambukizwa baada ya wiki moja nazo zitafichwa?
 
ACHENI KUTISHANA.
UGONJWA upo Huku India kuumwa mnaumwa nyie wa Huku bongo.
Kila MTU apambane na Hali yake
 
Sijaona dhamira ya Mh. Rais maana tangu ameongea kupata washauri amekaa kimya.
Huu ugonjwa sio wa kuundia tume bali unahitaji action.
Na kuonyesha hayuko serious bado maabara ya kupima covid wana fanya biashara na sample za wagonjwa. Huwezi niambia kupima sample ya covid ni 230,000/ wakati majirani zetu wana pima kwa 20,000/
Pia hii ina tunyima watalii maana ukiwaambia kupima covud ni 230,000/ wanasema ni ghali sana na wana ghairisha safari na kwenda nchi nyingine.
Waziri wa afya kakaa kimya tuu hana tamko????
 
Kwahio data za maelfu ya watu waloambukizwa au kufa baada ya kuhudhuria shughuli za msiba wa kitaifa zafichwa?

Na pia data za maelfu ya watu walohudhuria leo sherehe za Mei Mosi ambao watakuwa wameambukizwa baada ya wiki moja nazo zitafichwa?
Mikutano ilikuwa nje. Mwendo wa hewa inapunguza kuongezeka kwa pumzi lenye virusi mahali pamoja. Sitegemei vifo vya maelfu. Makumi hakika. Nategemea zaidi kuona mavuno ya futari za Ramadan.

Kuficha: hadi hospitali haziruhusiwi kupima wenyewe (hospitali kubwa zinaweza) hatuoni data. Wewe uite hali hii "kutuliza umma", mimi nasema "kuficha".
 
Ficha ujinga wako. Mwaka jana Magufuli alitangaza corona imeisha akapewa na ''kombe'' la ushindi kwa kuishinda corona. Kila mtu akamsifia (wajinga ofcourse ) na wengine wakasema wakawa wana-mock njia zinazochukuwa hatua au watu wanaokufa. Matokeo yake kuanzia mwaka jana mwezi wa 12 mpaka wa tatu corona ikarudi kwa kasi na vifo vikaondoka na watu wengi. Sasa wewe unarudia tena kosa lile lile. Hivi unajua hata India walikuwa wanasema corona imeshapita? Corona ina tabia ya kuja kwa awamu na inapoingia inaingia kimya kimya sana lakini watu wanapoanza kuugua na kufa inakuwa ni kishindo kikuu. Hata Tanzania sasa hi haiko salama na inaweza kurudi tena tena hali ikawa mbaya mpaka kila mtu akashangaa.
Si Tanzania tu, nchi nyingi walidhani Corona imeisha na wakalegeza lockdowns.

Baadae wakawa na second lockdown na wengine wamekuwa kwenye third lockdown.

Lockdowns zimewashinda nchi nyingi tu na leo wote wanafikiria kuweka masharti ya kuondoka kwenye hiyo kitu.

India wamefeli wapi ndugu?
 
Mikutano ilikuwa nje. Mwendo wa hewa inapunguza kuongezeka kwa pumzi lenye virusi mahali pamoja. Sitegemei vifo vya maelfu. Makumi hakika. Nategemea zaidi kuona mavuno ya futari za Ramadan.
Lakini India pia walifanya mikutano ya kisiasa nje na pia kuoga maji ya mto Ganges kwenye tamasha la kutambika la Kumbh Mela.

Leo hii watu milioni 19.1 wameambukizwa na zaidi ya 200000 wamekufa.

Yote hayo si yalifanywa nje au ?
 
Hivi ni kweli kabisa Rais Samia ana nia ya kweli ya kupambana na COVID-19?

Sijui kama na nyie mnafuatilia yanayoendelea huko India sasa hivi!

Akina Narendra Modi walikuwa huko West Bengal wanapiga kampeni za kisiasa utadhani hamna kesho. Ona sasa kilivyoumana.

Sasa kweli hiyo kamati aliyoiunda Rais Samia ili imshauri kuhusu corona ndo imemwambia kwamba ni sawa tu watu kwenda na kurundikana hapo uwanja wa Kirumba namna hiyo?

Ona hata hapo walipokaa hao viongozi! Hakuna social distancing. Hakuna barakoa. Hakuna tahadhari yoyote ile ya maana.

Hahahaaaaa…..what is this?

View attachment 1769853
Kufa Ni mara moja. Jikinge na uwapendao
 
Kuna dakatari kafa Kenya kwa korona. Na yeye kama Magufuli alikuwa anaidharau na kusema nyungu inatosha.
Daah huku usipovaa barakoa unaweza kwenda jela mpaka kesho kuingia duka lolote lazima unapewa sanitizer inasaidia sana sana na mambo ya social distance yanasaidia mno na viwanjani washabiki hawaendi ila bongo kila kitu wanachukulia poa tuu..
 
Hivi ni kweli kabisa Rais Samia ana nia ya kweli ya kupambana na COVID-19?

Sijui kama na nyie mnafuatilia yanayoendelea huko India sasa hivi!

Akina Narendra Modi walikuwa huko West Bengal wanapiga kampeni za kisiasa utadhani hamna kesho. Ona sasa kilivyoumana.

Sasa kweli hiyo kamati aliyoiunda Rais Samia ili imshauri kuhusu corona ndo imemwambia kwamba ni sawa tu watu kwenda na kurundikana hapo uwanja wa Kirumba namna hiyo?

Ona hata hapo walipokaa hao viongozi! Hakuna social distancing. Hakuna barakoa. Hakuna tahadhari yoyote ile ya maana.

Hahahaaaaa…..what is this?

View attachment 1769853

Hii tume ya Corona kama imeundwa na zinafanya kazi, basi ina lengo la kuona Mpango anachukua hatamu za serikali hivi karibuni.

Mama akili za kuambiwa hajachanganya na za kwake?
 
Si Tanzania tu, nchi nyingi walidhani Corona imeisha na wakalegeza lockdowns.

Baadae wakawa na second lockdown na wengine wamekuwa kwenye third lockdown.

Lockdowns zimewashinda nchi nyingi tu na leo wote wanafikiria kuweka masharti ya kuondoka kwenye hiyo kitu.

India wamefeli wapi ndugu?
Mbona unadandia bila hata kujua gari linakoenda? Kuweka Lockdown na kulegeza hilo jambo haliepukiki. Na hasa ndiyo njia ya ku deal na corona. Ni vizuri ujue kuwa walikuwa wanajua kabisa corona haijaisha na itarudi tena lakini kila inapopungua masharti yanalegezwa. Kitu ambacho umekwepa kusema ni kuwa pamoja na nchi hizo kulegeza masharti lakini bado kulikuwa hakuna mikusanyiko ya watu wengi na ni baadhi ya masharti tu yalilegezwa. India waliamua kujimwaga kama kila kitu kipo sawa na kukawa na mikusanyiko mikubwa ya kampeni na ya kidini.
 
Hivi ni kweli kabisa Rais Samia ana nia ya kweli ya kupambana na COVID-19?

Sijui kama na nyie mnafuatilia yanayoendelea huko India sasa hivi!

Akina Narendra Modi walikuwa huko West Bengal wanapiga kampeni za kisiasa utadhani hamna kesho. Ona sasa kilivyoumana.

Sasa kweli hiyo kamati aliyoiunda Rais Samia ili imshauri kuhusu corona ndo imemwambia kwamba ni sawa tu watu kwenda na kurundikana hapo uwanja wa Kirumba namna hiyo?

Ona hata hapo walipokaa hao viongozi! Hakuna social distancing. Hakuna barakoa. Hakuna tahadhari yoyote ile ya maana.

Hahahaaaaa…..what is this?

View attachment 1769853
Nakumbuka sana ulivyokuwa unamsifia Magu na sera zake za porini za covid. Uliwazodoa sana CHADEMA walipokuwa wanasisitiza standard measures ambazo umezigusia. Nini kimebadilika mkuu? Si ingefaa sera za nyingi ziendelee?
Hata Magu alipowazodoa wanaovaa Barakoa na kutamba kwamba yeye na wasaidizi wake, mkaona ni poa tu. Vipi tena?
 
Daah huku usipovaa barakoa unaweza kwenda jela mpaka kesho kuingia duka lolote lazima unapewa sanitizer inasaidia sana sana na mambo ya social distance yanasaidia mno na viwanjani washabiki hawaendi ila bongo kila kitu wanachukulia poa tuu..
Wabongo namna tuna laana ya aina fulani. Ila uzuri (japo inasikitisha) ni kuwa yule aliyekuwa analisha watu ujinga wa nyungu alishindwa kuitumia hiyo nyungu alipougua.
 
Mbona unadandia bila hata kujua gari linakoenda? Kuweka Lockdown na kulegeza hilo jambo haliepukiki. Na hasa ndiyo njia ya ku deal na corona. Ni vizuri ujue kuwa walikuwa wanajua kabisa corona haijaisha na itarudi tena lakini kila inapopungua masharti yanalegezwa. Kitu ambacho umekwepa kusema ni kuwa pamoja na nchi hizo kulegeza masharti lakini bado kulikuwa hakuna mikusanyiko ya watu wengi na ni baadhi ya masharti tu yalilegezwa. India waliamua kujimwaga kama kila kitu kipo sawa na kukawa na mikusanyiko mikubwa ya kampeni na ya kidini.
Nimedandia na comment namba 110 hapo juu.

Hivyo naelewa mwenendo wa mada.
 
Ficha ujinga wako. Mwaka jana Magufuli alitangaza corona imeisha akapewa na ''kombe'' la ushindi kwa kuishinda corona. Kila mtu akamsifia (wajinga ofcourse ) na wengine wakasema wakawa wana-mock njia zinazochukuwa hatua au watu wanaokufa. Matokeo yake kuanzia mwaka jana mwezi wa 12 mpaka wa tatu corona ikarudi kwa kasi na vifo vikaondoka na watu wengi. Sasa wewe unarudia tena kosa lile lile. Hivi unajua hata India walikuwa wanasema corona imeshapita? Corona ina tabia ya kuja kwa awamu na inapoingia inaingia kimya kimya sana lakini watu wanapoanza kuugua na kufa inakuwa ni kishindo kikuu. Hata Tanzania sasa hivi haiko salama na inaweza kurudi tena tena hali ikawa mbaya mpaka kila mtu akashangaa.
Ahahahah, na wewe unaijua tabia ya korona tayari. Eti "unajua corona ina tabia ya kuja kwa awamu na inapoingia inaingia kimya kimya".

Nimekuelewa virologist MWEREVU.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom