Ziara ya Rais Samia India: Mambo yanayomtofautisha na wapiga porojo wengine

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,100
49,795
Ziara ya Rais Samia Nchini India imekuwa ni ziara yenye mafanikio makubwa kwake binafsi in personal Kwa Kutunukiwa tuzo lakini Kwa Taifa kutokana na kusainiwa Kwa Hati 14 katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi na Kijamii.

Nitatoa mfano wa sekta ya Kilimo.Kupitia ziara hiyo Serikali ya Tanzania imefanikiwa kupata mambo yafuatayo,

1.) Imepata soko la zao la Mbaazi Tani 200,000 Kwa mwaka.
Mpaka hapo wakulima mna uhakika wa soko kubwa zaidi tofauti na awali.

Ikumbukwe mwaka huu wakulima wameuza mbaazi zao wastani sh.1900-2100 Kwa gunia Moja la kilo 100 sawa na kati ya sh 190,000-210,000 pesa ambazo zimeenda Kwa mkulima Moja kwa Moja.

Kabla ya Rais Samia mbaazi ilikuwa ni zao lilokufa Kwa kuwa aliyekuwepo alivuruga uhusiano na India Kwa sababu anazozijua yeye.

2). Serikali ya India kama mnunuzi Mkuu wa Korosho ghafi ya Tanzania imekubali kufuta Ushuru wa Asilimia 35% ambao expoeters Wetu walikuwa wanatozwa Kwa kuuza korosho iliyobanguliwa.India waliweka hiyo Ili Kulinda viwanda vyao vya kubangua korosho.

Hii Sasa inaenda ku make dream come true Kwa kusapoti lengo la Serikali la kuwa na kongani ya viwanda vya Korosho Mtwara na hivyo kufuta kabisa kuuza korosho ghafi by 2026.



Mpaka hapo tutakuwa na uhakika wa value addition na soko la korosho.Nawakumbusha pia korosho zilidoda awamu Ile mpaka kufikia kuleta maigizo ya eti jeshi kununua korosho😁😁 na pia wale Jamaa walikataa kununua korosho Kwa watu binafsi.

3. Serikali imeingia memorandum of understanding na Serikali ya India ambapo Wataalamu wao watakuja kufanya feasibility study Kwa Ajili ya kutoa maji Ziwa Victoria hadi Dodoma maalumu Kwa Ajili ya Kilimo kikubwa Cha Umwagiliaji.

View: https://www.instagram.com/reel/CyRJv1kt0_i/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==

Hili linaanzia mara Moja na likifaulu tunaenda kuwa na Kilimo kikubwa Cha Umwagiliaji kwenye Mikoa yote ambako mradi utapita Hadi Dodoma.

Mwisho Rais Samia alifanya Mkutano mkubwa na wawekezaji na wafanyabiashara wa India na kuwataka kuchangamkia Fursa ya uchumi ambapo Serikali ya Mama inapanga kuongeza uwekezaji mara 10 by 2025.


India ndio Taifa linaongoza Kwa idadi ya watu na linaongoza Kwa Ukuaji wa Uchumi na miaka 10 litakuwa zaidi ya China.

My Take
Samia ndio mama wa Uchumi na hakuna Rais wa Tanzania kabla yake amewahi fikia viwango vyake,probably baada yake itatuchukua miaka Mingi kumpata Rais wa Vitendo tofauti na porojo na propaganda tulizozoea.



IMG-20230920-WA0072.jpg
 
Ukisoma india bora kusoma UDOM.
Vijana wengi wa kiume hufia India ukiuliza unaambiwa Ajali.
Kumbe kumla mhindi ni nongwa
Hayo ni matatizo Yako binafsi,kaka yangu amesoma huko na kahotimu,Jamaa yangu kasoma huko kahitimu mbona hayakuwakuta unayoyasema? Punguza umbumbu
 
Back
Top Bottom