Maombi ya uchunguzi kuhusu uchangishaji fedha kinyume na taratibu kwa ajili ya ukarabati wa nyumba ya mkuu wa wilaya ya Maswa

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
130
Reaction score
118
Kwa Waziri,Mh Mohamed Mchengerwa,Waziri wa TAMISEMI.

Sisi wafanyabiashara wa mji wa Maswa kunapenda kuwasilisha malalamiko yetu kuhusu utaratibu unaoendelea wa kuchangishwa fedha na Katibu Tawala wa wilaya ya Maswa,Athuman Kalaghe kwa ajili ya ukarabati wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya.

Taarifa tulizonazo ni kuwa mara baada ya Mkuu wa wilaya aliyekuwepo kuhamishwa ilibidi nyumba ifanyiwe ukarabati ili kuruhusu Mkuu wa wilaya mwingine kuingia lakini fedha ya ukarabati ilitolewa na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa.

Tuna wasiwasi kuwa utaratibu huu kwa sababu zifuatazo:

1.Haujaambatana na tangazo rasmi wala kibali kutoka mamlaka za juu (TAMISEMI au Wizara husika).

2.Unakiuka Waraka wa Serikali wa Mwaka 2001 kuhusu marufuku ya michango na misaada isiyo rasmi kwa wananchi.

3.Unapingana na Sheria ya Fedha za Umma (Cap 348), ambayo inataka matumizi yote ya fedha ya umma na shughuli za serikali zifanyike kupitia bajeti iliyoidhinishwa.

4.Unawaweka wafanyabiashara katika hali ya mashinikizo na hofu ya kudhibiwa au kuonewa endapo hawatatoa michango hiyo.

Kwa msingi huo, kwa heshima tunaiomba ofisi yako:

1.Kufanya uchunguzi wa haraka juu ya suala hili.

2.Kuchukua hatua stahiki kwa yeyote atakayebainika kuhusika.

3.Kutoa maelekezo kwa watendaji wote kuhakikisha wananchi na wafanyabiashara hawachangishwi kinyume na utaratibu wa kisheria.

Tuna imani kubwa na uongozi wenu katika kusimamia haki, uwajibikaji na utawala bora.
 
Ni Maswa peke yake ndo mnakarabati nyumba ya mkuu wa wilaya. Duniani hakuna wanafanyabiashara wanaojenga majengo ya serikali kwa hela za kuchangishwa.
 
Back
Top Bottom