Mbunge Aisha Ulenge: Rasilimali Watu Wanawake Waingie Kwenye Tasnia Zenye Wanawake Wachache Ili Jinsia Zote Zishiriki Katika Maendeleo Endelevu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
944

MBUNGE Aisha Ulenge Amesema Rasilimali Watu Wanawake Waaingie Kwenye Tasnia Zenye Wanawake Wachache Ili Jinsia Zote Zishiriki Katika Maendeleo Endelevu

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga, Mhe. Mhandisi Mwanaisha Ng'anzi Ulenge Amesema tunapokwenda kuzalisha Rasilimali watu na kuilea Rasilimali watu ya Taifa ni lazima kuhakikisha na Wanawake waingie katika taaluma au tasnia ambazo zina Wanawake Wachache.

Mhandisi Ulenge Amesema kuwa lengo la kuhusisha Rasilimali Wanawake katika sekta ni kuhakikisha Jinsia zote zinashiriki katika maendeleo Endelevu ya Taifa letu na maendeleo Endelevu ya Dunia (No one should be left behind in contributing sustainable development)

Mhandisi Mwanaisha Ng'anzi Ulenge Amesema hayo katika kilele cha Hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Katika Makao Makuu ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari tarehe 09 Machi, 2024

Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mhandisi Zena Ahmed Said Amesema Watumishi wanawake wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Makao Makuu na Bandari ya Dar es Salaam wahimizwe kufanya kazi kwa bidii, weledi, uaminifu na uadilifu mkubwa ili kufikia malengo binafsi ya Taasisi na Taifa kwa ujumla.

Aidha, Mhe. Mhandisi Aisha Ulenge amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa TPA Ndg. Plasduce Mkeli Mbossa kwa kuhakikisha Wanawake ni sehemu ya mafanikio ya Bandari kwa mikakati yake ya kuwajengea uwezo wakinamama wa TPA.

Wakati wa hafla hiyo pia Viongozi hao walipokea Kombe lililotwaliwa na Timu ya Mpira ya Netiboli ya TPA, Bandari Queens baada ya kutwaa Ubingwa wa Ligi Daraja la Pili na kupanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza Taifa.
 
Back
Top Bottom